Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Mhe. Waziri wa Utumishi, ili kuondoa manung'uniko, upotashaji na sintofahamu iliyotokea baada ya mishahara ya mwezi huu wa June kutoka huku baadhi ya watumishi wakiwa wamepandishwa madaraja na kupata mishahara mipya ila hali wengine hakuna kilichobadilika, nakushauri utoe ufafanuzi wa jambo hili kwa umma.
Msingi wa malalamiko na sintofahamu iliyopo inatokana na kauli yako ya kuhakikisha watumishi wote wanaostahili kupanda madaraja wanapanda na kulipwa mishahara mipya mwezi huu jambo ambalo halikutokea kwa watumishi wote
Inawezekana kuna changamoto zilijitokeza kama vile hela ya kuwalipa iliyotengwa haikutosha tofauti na matarajio yenu au kumekuwa na kasoro nyingine zilizopeleka baadhi ya watumishi(inaonekana ni wengi tu) kutopandishwa. All in all, kwakuwa watumishi hawaelewi, basi malalamiko lazima yawepo, hivyo ni bora kutoa ufafanuzi na kueleza mkakati uliopo kwa wale ambao hawakupandishwa madaraja.
Mpaka sasa teyari kuna maneno mengi: kuna wanaodai mnapandisha kwa awamu, waliobaki watapandishwa mwezi ujao wa July, System imewatema kimakosa baadhi ya watumishi(imewaruka) n.k. Hivyo, utagundua kuwa kuna sintofahamu kubwa tu kuhusu hali hii kwahiyo ni bora serikali ikatoa kauli.
Information ni tiba panapokuwa na sintofahamu.