UPANDE WA PILI WA MAISHA:mbona mtu akifa anaogopwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UPANDE WA PILI WA MAISHA:mbona mtu akifa anaogopwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Teamo, Apr 9, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MABIBI NA MABWANA!
  habari zenu?................

  Pamoja na misukosuko mingi,ugumu wa maisha,tabu za maisha,na uchungu wa maisha..........BADO KILA MTU ANATAMANI KUENDELEA KUISHI,na pengine angependa kuongezewa muda wa kuishi walau dakika moja tu.

  Nimekaa chini nikafikiria sana,kwamba chini ya jua binadamu wengi tunafikiria upande wa kwanza wa maisha ambao unajumuisha hekaheka zote za kidunia(siasa,uchumi,madaraka,maisha,mapenzi,vita,utajiri mkubwa ufisadi nakadhalika)

  Sasa kwenye upande wa pili wa maisha............'KIFO',pana mtihani mkubwa sana.Kwa sababu katika hili asilimia kubwa ya wanadamu HATUJISHUGHULISHI NALO KABISA,na kuna wakati HATUNGPENDA KULIJADILI.

  mimi naomba tuanze kujadili MATOKEO,AU IMPACT..........mtu akishakata roho,ANAOGOPWA KUPINDUKIA.waliopata matatizo ya kufiwa wanaweza kulithibitisha,na anaeandika hii thread NI SHAIDI NAMBA MOJA.

  ..........hata afe baba mzazi,mama,mke,mchumba,au nani unaempenda UNAMWOGOPA SANA,na hungependa kuonana nae tena,hata sura yake ikija njozini unahama kitanda

  Jamani eeh!naomba tujadili,
  KWA NINI MTU AKIFA ANAOGOPWA?
   
 2. P

  Preacher JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante kwa thread yako. Ni kweli hili ni muhimu sana - Unapokuwa HAI unaitwa MTU unapokufa (uhai ukitengana nawe) unaitwa MAITI na unapozikwa unaitwa MAREHEMU. Ukweli ni kuwa MTU NI ROHO (spirit) inayokaa kwenye mwili - ndio maana MAITI ina macho, masikio, pua, mikono, miguu lakini havifanyi kazi - kwani MWILI bila ROHO hauwezi kitu.

  Katika uumbaji MUNGU ALIMPULIZIA SANAMU YA UDONGO PUMZI YAKE IKAWA HAI NA AKAIITA ADAMU - NA PUMZI IKAMHAMISHA ADAMU TOKA KUWA SANAMU NA KUWA MTU - MAITI inaogopewa kwa sababu imebadilika kuwa UDONGO - nani asiyeogopa kushika matope?? Huo ndio mtazamo wangu.

  UNAWEZA HATA KUISHIKA SIKU YA LAST RESPECT (KUOSHA ETC) LAKINI IKIKAA SANA INANUKA, INAOZA - UTHAMANI UNAKWISHA - HATA ICHOMWE MOTO, UZIKWE KWENYE SANDUKU LA KIFAHARI, KWENYE MKEKA (WHATEVER) MTU KESHAONDOKA - HUKO TUENDAKO NI MASWALA YA IMANI - ILA TUNARUDI KWA ALIYETUKOPESHA PUMZI YAKE (ROHO) - NA LEO NI BABA ILA KESHO ATAKUWA HAKIMU KUTOKANA NA MAAGIZO YAKE NA SHERIA ZAKE ALIZOTUWEKEA
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama hujawahi kufiwa kweli utaogopa maiti sana.Lakini ukishafiwa ndiyo utaona tofauti. Woga utakutoka.Kinachotisha ni maiti za watu wanaopata ajali au kuharibika maana inakuwa kama vile unapata uchungu kufikiri huyo mtu alipata maumivu kiasi gani hadi alipokata roho na hasa kama huyo mtu ni wa karibu sana.

  Woga pia unakuja pale mtu unapofikiria kuwa na wewe iko siku utaacha kupumua.Hapo ndipo unapoanza kutafakari maisha yako na hatima yako itakavyokuwa pale utakapoaga dunia.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...:D:):( inachekesha, inafurahisha kisha inasikitisha kwani uliyoyasema ni kweli tupu.

  ...utakuta msiba umetokea watu wameinama kwa huzuni, kina mama wanalia usiku kucha, sasa hapo ghafla 'maiti' anyanyuke kipindi watu wanatoa heshima za mwisho! ...hapatabaki mtu, na hata huyo jabali ambaye atabakia atajitahidi kwa nguvu zote kumlaani/kumkemea shetani huku aking'ang'ana kulifunga jeneza!

  ...ukisawa angani ndani ya zile ndege ndogo na maiti wenu pembeni, (kutokana na thin air pressure), kuna milio mingi ya ajabu ajabu inatokea kwenye jeneza...unaweza tamani ndege itue ushuke!

  ...anyway, yote naamini yanatokana na kulelewa, kukulia na kuishi kwenye jamii inayotishika kirahisi na mambo ya mashetani, majini, misukule na mizimu!
   
 5. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mi nadhani tunaogopa kwasababu hatupendi kuelewa kwamba kifo ni sehemu ya mzunguko wa maisha. Binadamu ni lazima 'a-pass-on' na pale anakua na umbo lingine.

  Maiti tunaigopa labda kwasababu aliyekufa ni mwili usiyo na uhai wowote na pengine siku chache zilizopita huyo mtu alikua anacheka, anaongea etc. Ukifikiria hivyo...mwili unasisimka.
   
Loading...