Najaribu pia kutetea
1. Aliyeteuliwa labda alisoma hgk
2. Mleta mada ulikosa hiyo nafasi huenda wewe shulen n mvivu mleta majungu tu kujifanya kujua kuwapa shida tu wakuu wa shule lkn mkisikia fursa macho mbele
3. Kama Mwl aliyeteuliwa n mpiga kazi kwa weledi haina shida hata kama hakusoma kisw si ipo marking scheme? Pepa lenyewe form two.
Kweli kabisaBila shaka huu uzi umeletwa na mwalimu ambaye alitegemea ateuliwe ila hakupewahio chance,
Duuu! Kwa kweli utasubiri sana maana wewe ni mwanaharakiti upumbavu. Kibaya zaidi unajiona hukosei. Jitathmini ndugu utabaki kulaumu miaka yote kujifanya huzitaki mbichi hizo kumbe unalala kuziwazia.Mkuu Lundavi inaonekana akili yako imeenda likizo, hakuna mtu asiyefanya kazi tatizo linabaki kwa baadhi ya wakuu wa shule wanatumia nafasi zao vibaya kwa kuwabeba baadhi ya walimu wanaowalamba miguu na kuwakandamiza wengine wenye kujielewa .Yawezekana una conflict of interest.
Inamaana huyo mwalimu hajasomea kiswahili?Mkuu wa shule moja ya sekondari ya kata kwa makusudi ampeleka mwalimu wa somo la Geography akasahihishe mtihani wa Taifa wa kidato cha pili somo la Geography huku akiwaacha walimu wa somo husika.Huu ni mwendelezo wa vitendo vya rushwa na upendeleo vilivyokithiri kwa baadhi ya wakuu wa shule.
Shule hiyo ya kata ipo Bagamoyo mjini kilometa 3 kutoka Bagamoyo mjini kuelekea Dar es Salaam.Inapatikana karibu na Check point ya askari na maafisa wa TRA.
Hivi hawa baadhi ya wakuu wa shule mbona wanajisahau sana ? Kwa nini wanakiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kukumbatia uovu ?
Nina imani na serikali ya mh.Rais John Pombe Magufuli itaondoa uozo huu na kuendelea kujenga misingi bora ya nchi.