UOZO WA SERIKALI: Hospital Rufaa Bugando Haina XRAY zaidi ya mwezi wagonjwa wapelekwa Vituo Vya afya

tonnyalmeida

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
226
46
Madaktari wanapogoma wanasababu za msingi, na mojawapo ni la uboreshaji wa Huduma za afya. Unaweza kuamini Hospitali Yarufaa inayohudumia zaidi ya watanzania milion 9 katika mikoa zaidi ya 5 haina huduma za X Ray huku wagonjwa wakipelekwa katika vituo vya afya vya mwananchi na Aghakhan wachache wenye bahati katika Hospitali ya mkoa ambapo ubora wa picha zao unalalamikiwa na madaktari?

Na katika hili HOSPITALI HAINA KOSA kwa sababu ukifuata mkataba wa MoU kati ya serikali na Mashirika ya dini katika uendeshaji wa hospitali hzo imetaja wazi mwenye kuwa MWENYE WAJIBU WA KUTOA VIFAA TIBA NA MISHAHARA YA MADAKTARI ni SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA.

kumekuwa na taarifa zinazoonyesha baadhi ya wagonjwa wamepata madhara
1. wakati wakibebwa kupelekwa kwenye hvo vituo vya afya kupata huduma ya xray
2. kwa kuchelewa kupata huduma za matibabu kwa kufuata huduma mbali pale ambapo madaktari wanahtaji kufanya maamzi ya matibabu kutokana na picha na xray


KWA HILI BADO TUNATAKA KULAUMU MADAKTARI NA HOSPITALI ZETU?


TAFAKARI CHUKUA HATUA 20120229_003.jpg
20120229_001.jpg 20120229_001.jpg
 
Back
Top Bottom