lendanai
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 365
- 259
Habari,
Nina furaha kubwa kupata fursa hii tena ya kuchangia hoja mbalimbal humu jukwaani lengo ni kushare uzoefu,ujuzi na maarifa. Siku kadhaa zilizopita nilitembelea baadhi ya kata mbalmbali,ndipo nilipokutana na hii kero ya wananchi pale kata ya Olmot. Kwa ufupi iko hivi maafisa watendaji wa kata hii wamekuwa miungu watu kwani wamekuwa na vitisho kwa wananchi wenye matatzo yao hasa hasa hizi migogoro ya mipaka.
Unakuta mtu ana vielelezo zote zinazoonyesha uhalali wa haki yake lakini maafisa hawa hutoa maamuzi kwa upande ambao wamepewa kitu kidogo au rushwa kwa ufasaha. Hii nimeshuhudia live kabisa pale kitongoji cha Nafco kata ya Olmot mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 13 sasa kati ya bwana Saiguran mlalamikaji na bwana Aloyce Meshilieki mlalamikiwa,maafisa watendaji hawa walikuwa kwa mbwembwe nyingi huku wakijitapa kuwa wao ndio Serikali na wana uwezo wa kuamua chochote na mwananchi asifanye lolote.
Pia waliambatana na afisa taarafa ambayo naye alionekana kupendelea upande mmoja wenye maslahi kwao,walitoa uamuzi ambayo ni kama kuwachochea hawa ndugu kwa sababu wamemnyang'anya bwana Saiguran eneo lake lenye ekari tatu na kumkabidhi bwana Aloise.
In term of conflict resolution hii sio sahihi kwa sababu hawa kuangalia hasa chanzo cha mgogoro ni nini wao wamechukulia jambo in power of rules yaani wapi ndio wenye mamlaka,nimejaribu kuangalia chanzo cha ugomvi nikapata haya,.
Kwanza hizi eneo zilikuwa na namba,iko hivi bwana Saiguran shamba lake liko upande wa namba moja na ana vielelezo zote zinazoonyesha haya na bwana Alois yeye shamba lake liko upande wa namba mbili. Utata ulianzia pale bwana Alois aliponunua shamba kutoka kwa mtu mwingine eneo ambalo anaishi yeye na kujikuta anavuka mpaka kitongoji hiki cha Nafco.
Kata ya Olmot imekuwa na migogoro mingi sana ya ardhi inayosababishwa na mipaka kati ya namba moja na namba mbili kutojulikana ilipo hasa,kuna baadhi ya wananchi wanayo ramani kabisa tatizo likaja kuhusu surveyer wa kuwasaidia kusoma hizo coordinate na kumulika bicon za mipaka hii,.
Rai yangu naomba Serikali iingilie migogoro ya kata hii hasa hasa waje na surveyer kabisa ili kuondoa hii kero iliyodumu pale kwa miaka mingi,afisa tarafa ameshindwa hili kabsa na tatzo dogo sana ni mipaka tu basi.
Nawasilisha wadau