Uozo: Shida zote nchini gazeti laandika na kutoa kipaumbele habari za Ujauzito wa Mchumba wa Slaa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uozo: Shida zote nchini gazeti laandika na kutoa kipaumbele habari za Ujauzito wa Mchumba wa Slaa!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ta Muganyizi, Jun 1, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Katika hali ambayo imenisikitisha na kunifanya nijiulize mwelekeo wa nchi hii ni pale ambapo katika magazeti ya leo habari za epa, umeme, gavana kubanwa, kesi ya mahalu, Uchumi wa nchi na gavana kuongelea mustakabali wa uchumi wa nchi yetu vimeandikwa na kupewa kipaumbele katika magazeti, wenzetu wale wa magazeti ya Uhuru na Habari leo wametoa kipaumbele kwa habari inayosema kuwa cheti cha ujauzito wa mke/mchumba wa Dr Slaa kina utata mara kingine kinaonesha miezi saba na kingine miezi nane.

  Sasa ninachojiuliza matatizo yote yaliyoko nchini wewe unaona uwaeleze wananchi kuwa mimba ya mchumba wa haijulikani ilitungwa lini!! hiyo inamsaidia nini Mtanzania sasa. Sisi kujua mimba ya fulani iliingia siku hii au ile. Ndo maana president wetu alikuwa haijui Dowans. Mnaconcentrate kwenye mimba za watu na kujua na kufuatilia mambo ya ajabu. Sishangai kwa staili hii mtakapoandika kuwa mwanachama wa chama fulani (mwanamke) mwezi huu hajaingia kwenye MP zake maana nimeshangaa. Nafuu habari ingekuwa hata ukurasa wa pili. lakini ndo iko juu kabisa ili watanzania wajue. Kwa nini msitaje waliorudisha fedha za epa kina nani na hizo fedha ziko wapi.

  Zile habari za ufisadi kama Chadema wamefanya kwa mfano, tuleteeni tujue kama kuna mapungufu hayo kwenye chama hicho au CUF koote tuone kinachoendelea ili tujue kipi cha kufanya kuikomboa nchi. Sasa mimba ya huyo mama sisi tuifanyeje. Nimesikitika sana. Yaani aibu nasikia kwa kweli. Hata rafiki yangu wa nchi jirani kashangaaa kweli kweli. Maskini Tanzania!!! Mimba, mimba, mimba, kipaumbele kwenye gazeti ambalo si la udaku???!! Sasa global publishers waandike nini?
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Sina hamu
   
 3. A

  Aman Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh!.hata mim nimeliona mpwa,nikajiuliza ni ngozi nyeusi zenye matatizo au UTZ,coz kweli unatuandikia mambo ya mimba ya mchumba wa silaa kweli,umasikini utaisha kweli?
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Njaa zinawasumbua hawa wahariri, hapa ni anaandika na kuwaza kwa kutumia tumbo.

  Ukuwadi kwenda mbele.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,606
  Likes Received: 4,732
  Trophy Points: 280
  Ni utaahira wa waandishi na wahariri wao.Nji hii bana,ndiyo maana rais anasema hajui kwanini Tanzania ni masikini,kama daktari hajui ugonjwa wa mgonjwa wake atatoaje tiba?
   
 6. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli inasikitisha mno,tunakoelekea mi cjui,naona kama wingu kubwa sana mbele,mimba au maisha ya mtu labda kala nn au kalala wapi gazetin ambayo cyo udaku ni ulimbuken na fikra ya ajabu sn,c wangeandika basi ya viongozi wao?Sishangai sana maana ni magazeti ya choon ndo yameandika.
   
 7. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hao ndio wanahabari walio karibu kabisa na ccm na jk na ndio maana hana hata cha kuwaeleza Watz mwezi may. ni aibu kubwa watu kuandika habari nyepesi kama hizi na kuacha habari muhimu kwa taifa.
   
 8. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,802
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  waandike bwana! tujue vizuri, anataka kuja kuwa raisi huyu, asije akatunyang'anya wake zetu!
   
 9. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli ndugu yangu hata mimi ninashangaa kama kweli nchi na watu wake wanafikiria mimba za watu badala ya mambo ya maana hatutafika mahali. Mimba ya Mchumba/mke wa Dr. Slaa haina maslahi ya kitaifa bali maslahi wa wanasiasa uchwara. Hatutegemee maslahi ya wanasiasa uchwara yajipenyeze hadi kwenye ulingo wa Magazeti.
   
 10. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Toa ushamba, kama hayo unayoyasema ni kweli basi iwe kwa Dr. Slaa tu kwa sababu hata aliyeko Ikulu tulitakiwa kuanza naye.
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Ta Muganyizi

  ningejua kukugongea thanks kwa kihaya ningefanya hivyo .... ngoja nikupigie ya kizungu
   
 12. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Unanikumbusha maneno ya mwisho ya Baba wa Taifa kabla hajaaga dunia: "Nawasikitikia sana Watanzania wangu"!
   
 13. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  hili si gazeti la serikali? hawaoni hayo matatizo hawa jamaa,ndo maana hata the big gambaz hana la kuzungumza mwezi mei.
   
 14. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  kuna newspaper vendor fulani Arusha stand yupo systematic sana...yeye ameyapanga magazeti yake kwa category (udaku, kiingereza, michezo, kiswahili na dini) sasa nitam-text aliweke hilo gazeti kwenye category ya udaku kuanzia kesho.
   
 15. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Huu ni uhalo...shule mbovu,barabara mbovu,elimu mbovu,watu wanalia na umaskini,umeme haupatikani,hospitali hazina dawa,wanafunzi wanakaa sakafuni,yoooote haya hawayaoni badala yake wanaandika juu ya mimba ya mtu mmoja Tanzania tena headline ya gazeti!!,anyway,waliisha chelewa sanaaa,hawawezi tena kuigeuza kujumlisha kuwa kutoa
   
 16. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  We have got some newspapers to read when we real need to know to which direction is our country heading.
  We have also got some newspapers that we can read when we are tired and we need a loughter.
  (SANI,BONGO,HABARI LEO,UHURU etc)
   
 17. C

  Choro Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BASHE AMESEMA JUZI VYOMBO VYETU VYA HABARI VIMEPOTEZA MVUTO KWA JAMII KWA KUTOA POROJO. Nadhani Bashe ameligundua hilo, hivi bado hajawambia wajilekebishe. Gazeti la Uhuru linazidi kupoteza hadhi yake.
   
 18. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  ni gazeti lipi?
   
 19. m

  mbagasa Member

  #19
  Jun 1, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaiombea hiyo mimba iwe na toto jembe kama baba yake,
   
 20. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  siasa mchezo mchafu....
   
Loading...