Uozo Ndani ya Polisi: Wanachi wamechoka; Jisomee huu Mkasa

Polisi ni uozo uliokithiri, wanalazimisha hadi rushwa ya shs elfu moja!sijui hii ni njaa au tabia na kamfumo ka kila mtu kufanya anavyoweza chini ya manifesto ya ccm, make haka kautaratibu kamezoeleka!dawa ni kubadilisha uongozi na kuwa na viongozi walio serious sio hawa ambao wameshindwa kwa kila kitu!najisikia vibaya kuitwa mtanzania wa sasa!!!!!!!!!!!!!
Wapigwe tu risasi maana hakuna namna nyingine.
Freedom is coming tomorrow
 
Hawa polisi wetu kwa uonevu sina hamu nao.
Nakumbuka siku moja nimesimamishwa na polisi wa ubungo external barabarani. Ile napunguza mwenda nisimame jamaa wa bodaboda yuko high speed kagonga gari yangu kwa nyuma afu kaanguka mwenyewe kwenye mtaro. Yule polisi alichofanya ni kuchukua leseni yangu na funguo za gari eti nimesababisha ajali kwa hiyo nimpeleke hospitali na kutengeneza pikipiki yake.nilibishana naye sana kwani yeye polisi ndiye alinisimamisha na bodaboda ndiye alinigonga kwa nyuma. Polisi kanisumbua tangu saa 4 asubuhi hadi 12 jioni hataki kunirudishia leseni na funguo. Nilivyoona mambo yangu yanazidi kuchelewa ilibidi nikubali kugharamia matengenezo ya bodaboda. Hata hivyo polisi alinilazimisha kutoa rushwa ya laki 2 ili anirudishie leseni na funguo ingawa gari hakuikuta na kosa lolote. Yaani ile siku ilinitoka kama laki 4 hivi.

Tangu siku hiyo nimeapa polisi akinisimamisha, nitasimama kama hamna namna nyingine ya kuwakimbia. Ule msemo wao wa tii sheria bila shuruti hauna mantiki tena kwangu.
 
Wafe tu manyang'au hao.sio msiba wa kitaifa ni msiba wa familia zao. Walichowahi nifanyia polisi sina huruma nao hta kiduchu.
 
We bila sha
Sina shaka kuwa mtoa maada na wafaasi wake ni vibaka.Je, hiyo tuhuma mliambiwa au mlishudia? Mwanaharakati halisi ni muungwana, muuwazi ,mzalendo na ufanya utafiti kabla ya kuripoti taarifa.Huwezi ukahukumu Jeshi zima la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa kosa la mtu mmoja.Tuacheni unafiki na uzushi.Mara ngapi polisi wameuawa wakilinda maisha yetu na mali zao?Ni taasi au wizara gani duniani isiyokuwa na mapungufu hasa ukizingatia kuwa na huko misikitini na makanisani kumejaa kashifa?
Bila shaka we ni mmoja wao,nahic 2,kama c mmoja wao naomba yakukute siku moja.
 
Ukisikia uonevu wa polisi Tanzania basi hii hapa ni ya mwaka! Chama cha CCM inabidi ijipange kuhususiana na watendakazi wake. Raia hawatawavumilia tena. Kesi za uonevu na unyanyasaji zimezidi! . Kuna mshikaji wangu mmoja anaishi huko majuu marekani. Alikuja likizo kumuona mkewe. Wife akawa anaendesha gari maeneo ya Ubungo, ghafla polisi akawasimamisha na kumuomba leseni. Baada ya huyo mama kumpa leseni, huyo polisi hapo hapo akasimamisha madereva wengine watatu. Ghafla alifika dada mwingine, matokeo yake akamsimamisha, na kuingia kwenye gari lake na kuongozona naye akidai wanakwenda kituoni. Hapa ana leseni ya watu wanne. Hao wengine wote wakaambiwa wamfuate kkwenda Ubungo Bus Terminal Police. Walipofika hapo kituoni, polisi mwenyewe hakawa hayupo kumbe lile gari alilopanda alimalizana na dereva wake njiani. Basi wote waliokuwa wakidai leseni zao wakaondoka.

Baada ya kurudi kesho yake, huyo traffic akawa hayupo tena, jamaa na mkewe wakaondoka. Baada ya wiki tena, huyo mama akarudi mtu mzima akarudi kutafuta leseni yake, bahati nzuri akamkuta yule polisi sasa. Akaambiwa atoe laki tatu ili asamehewe Tsh. 300,000. Mama akashtuka aksema hana hela, basi wakamuomba laki na nusu. Mama akakataa, basi hapo hapo. Wale polisi wakaamua kumbambia kesi ya kutanua na kumuingiza mama wa watu Sero na waalifu wengine vibaka, majambazi nk... (hii ni wiki moja baadae, na mama kaja mwenyewe kutafuta leseni yake). Huyu mama alikuwa na $1,900 taslimu siku hiyo alizoachiwa na mumewe kwa ajili ya shuguli zao a kimaendeleo. Basi wakati wa kuzikabidhi hizo hela, akaomba kumjua jina anayekabidhiwa. Kosa kuuliza, akabambikiziwa kesi nyingine ya kashfa dhidi ya polisi na tayari hapa walishagawana hizo $1,900. Mama wa watu, mtu mzima akakaa sero kwa siku nzima bila kosa akiambiwa kesho anapelekwa mahakamani, mtu aliyeondoka nyumbani kwake kuja kuchukua leseni yake aliompa polisi kwenye routine check ya kwaida, matokeo yake kuswekwa ndani.

Bahati yake ikawa kuomba simu yake kuwataarifu ndugu zake kuhusu mkasa uliomkuta. Baada ya kumpigia mumewe, bahati nzuri mume ana ukaribu na Kamanda Kova. Mume akampigia Kova, naye Kova kampigia mkuu wa trafiki wa mkoa haraka haraka kuzima hii kashfa. Sasa kumbe shemeji yake huyu dada ni mtu mkubwa sana TAKUKURU. Shemeji mtu wa TAKUKURU akaenda moja kwa moja hadi Ubungo Terminal Police Station. Polisi wakawa hawajui nani kaja pale wakaanza kumchimba mkwara, kumbe wanachimbia bosi mkubwa sana wa taukururu. huyu bosi wa TAKUKURU na ile tabia ya kulindana na wakuu wa polisi, naye pia kazima hii skendo kutokana na ombi la mkuu wa trafiki..... Mimi niliposimuliwa nikabaki mdomo wazi. Ikiwa watu wakubwa wanafanyiwa hivi watu wa kawaida je? Mimi na wewe tukikamatwa itakuwaje? kwa maana hawa polisi walipoona mambo yamekuwa magumu, wakaanza kumfukuza huyo mama aondoke hapo kituoni haraka sana.... yaani basi tu. Ila najiuliza maswali machache

-Mtu anakuja kudai haki yake, anakamatwa na kuwekwa sero na wahalifu sugu kama majambazi na wauaji?
-Rushwa inakuwa ya kulazimisha, wakuu wanataarifiwa lakini hawachukui hatua, nchi inaelekea wapi?
-Wakuu wao wanataarifiwa kuhusu uhuni kama huu alafu wanazima skendo, bila ya kuwawajibisha hawa polisi wasio na nidhamu? Kova kaletewa kesi kama hii, Polisi wa Ubungo Terminal kufanya uchafu kama huu, alichukua hatua gani dhidi ya hawa vibaka ndani ya jeshi lake, au kuuzima kwa kumuachia huyo mama ndio mambo kwisha, na hela zake je??

C.C.M inafanya nini dhidi ya hawa watendaji wake, has apolisi wasio na nidhamu? Kamanda Lema kayazungumzia haya majuzi Bungeni lakini tunaona wanamagmba hawasikii. Hatutakubali uonevu kama huu, mrudishieni huyu mama hela zake. $1,900 ni nyingi sana kumnyang'angya mtu

IGP Mwema,
Cmdr. Kova,
Fuatilieni huu mkasa na kuwawajibisha hawa polisi wa Ubungo Terminal kabla haujaingia kwenye media. Hii ni skendo kubwa
Mambo kama haya yanawapa sana kick magaidi. Frankly ugaidi tunaulea wenyewe. Our leaders must be serious.Watu waliokata tamaa ni breeding ground nzuri sana ya ugaidi.Hata mpira una "elastic limit."Naomba Mungu tusifike huko.
 
Back
Top Bottom