Uozo Ndani ya Polisi: Wanachi wamechoka; Jisomee huu Mkasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uozo Ndani ya Polisi: Wanachi wamechoka; Jisomee huu Mkasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Muke Ya Muzungu, Aug 1, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ukisikia uonevu wa polisi Tanzania basi hii hapa ni ya mwaka! Chama cha CCM inabidi ijipange kuhususiana na watendakazi wake. Raia hawatawavumilia tena. Kesi za uonevu na unyanyasaji zimezidi! . Kuna mshikaji wangu mmoja anaishi huko majuu marekani. Alikuja likizo kumuona mkewe. Wife akawa anaendesha gari maeneo ya Ubungo, ghafla polisi akawasimamisha na kumuomba leseni. Baada ya huyo mama kumpa leseni, huyo polisi hapo hapo akasimamisha madereva wengine watatu. Ghafla alifika dada mwingine, matokeo yake akamsimamisha, na kuingia kwenye gari lake na kuongozona naye akidai wanakwenda kituoni. Hapa ana leseni ya watu wanne. Hao wengine wote wakaambiwa wamfuate kkwenda Ubungo Bus Terminal Police. Walipofika hapo kituoni, polisi mwenyewe hakawa hayupo kumbe lile gari alilopanda alimalizana na dereva wake njiani. Basi wote waliokuwa wakidai leseni zao wakaondoka.

  Baada ya kurudi kesho yake, huyo traffic akawa hayupo tena, jamaa na mkewe wakaondoka. Baada ya wiki tena, huyo mama akarudi mtu mzima akarudi kutafuta leseni yake, bahati nzuri akamkuta yule polisi sasa. Akaambiwa atoe laki tatu ili asamehewe Tsh. 300,000. Mama akashtuka aksema hana hela, basi wakamuomba laki na nusu. Mama akakataa, basi hapo hapo. Wale polisi wakaamua kumbambia kesi ya kutanua na kumuingiza mama wa watu Sero na waalifu wengine vibaka, majambazi nk... (hii ni wiki moja baadae, na mama kaja mwenyewe kutafuta leseni yake). Huyu mama alikuwa na $1,900 taslimu siku hiyo alizoachiwa na mumewe kwa ajili ya shuguli zao a kimaendeleo. Basi wakati wa kuzikabidhi hizo hela, akaomba kumjua jina anayekabidhiwa. Kosa kuuliza, akabambikiziwa kesi nyingine ya kashfa dhidi ya polisi na tayari hapa walishagawana hizo $1,900. Mama wa watu, mtu mzima akakaa sero kwa siku nzima bila kosa akiambiwa kesho anapelekwa mahakamani, mtu aliyeondoka nyumbani kwake kuja kuchukua leseni yake aliompa polisi kwenye routine check ya kwaida, matokeo yake kuswekwa ndani.

  Bahati yake ikawa kuomba simu yake kuwataarifu ndugu zake kuhusu mkasa uliomkuta. Baada ya kumpigia mumewe, bahati nzuri mume ana ukaribu na Kamanda Kova. Mume akampigia Kova, naye Kova kampigia mkuu wa trafiki wa mkoa haraka haraka kuzima hii kashfa. Sasa kumbe shemeji yake huyu dada ni mtu mkubwa sana TAKUKURU. Shemeji mtu wa TAKUKURU akaenda moja kwa moja hadi Ubungo Terminal Police Station. Polisi wakawa hawajui nani kaja pale wakaanza kumchimba mkwara, kumbe wanachimbia bosi mkubwa sana wa taukururu. huyu bosi wa TAKUKURU na ile tabia ya kulindana na wakuu wa polisi, naye pia kazima hii skendo kutokana na ombi la mkuu wa trafiki..... Mimi niliposimuliwa nikabaki mdomo wazi. Ikiwa watu wakubwa wanafanyiwa hivi watu wa kawaida je? Mimi na wewe tukikamatwa itakuwaje? kwa maana hawa polisi walipoona mambo yamekuwa magumu, wakaanza kumfukuza huyo mama aondoke hapo kituoni haraka sana.... yaani basi tu. Ila najiuliza maswali machache

  -Mtu anakuja kudai haki yake, anakamatwa na kuwekwa sero na wahalifu sugu kama majambazi na wauaji?
  -Rushwa inakuwa ya kulazimisha, wakuu wanataarifiwa lakini hawachukui hatua, nchi inaelekea wapi?
  -Wakuu wao wanataarifiwa kuhusu uhuni kama huu alafu wanazima skendo, bila ya kuwawajibisha hawa polisi wasio na nidhamu? Kova kaletewa kesi kama hii, Polisi wa Ubungo Terminal kufanya uchafu kama huu, alichukua hatua gani dhidi ya hawa vibaka ndani ya jeshi lake, au kuuzima kwa kumuachia huyo mama ndio mambo kwisha, na hela zake je??

  C.C.M inafanya nini dhidi ya hawa watendaji wake, has apolisi wasio na nidhamu? Kamanda Lema kayazungumzia haya majuzi Bungeni lakini tunaona wanamagmba hawasikii. Hatutakubali uonevu kama huu, mrudishieni huyu mama hela zake. $1,900 ni nyingi sana kumnyang'angya mtu

  IGP Mwema,
  Cmdr. Kova,
  Fuatilieni huu mkasa na kuwawajibisha hawa polisi wa Ubungo Terminal kabla haujaingia kwenye media. Hii ni skendo kubwa
   
 2. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  da m nampa pole sana hyo mama ndo uozo wa nchi yetu
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,435
  Trophy Points: 280
  haya si ndio mambo Lema alikuwa anayaongea bungeni akakatazwa? naibu spika alimwambia asiisome......wanajua kinachoenndelea kwani wanagawana
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  CCM chama cha madhalimu kina yajua yote haya, kimeamua makusudi kuyafumbia macho.
  Wananchi hawana mtetezi wao, machozi yao ni kama ya samaki, yanakwenda na maji.
   
 5. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hili swala ni zito. hata na mimi nimelisikia, Polisi aliyehusika anaitwa Matemate... baada ya kunyimwa rushwa ya tsh. 300,000 wakamsweka huyo mama ndani na kumbambikizia charges nyingine...Kova inabidi ashugulikie hili swala, vinginevyo hata yeye yatamfikia shingoni.

  Kuna vijana wa Kova hata mambo ya ndani wanaongia humu jamvini. inabidi wafuatilie hili swala kabla alijaenda mbali. kuna gazeti linafuatilia hii stori kwani hadi takukuru walifika hapo kituoni.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Ila kama Kova alivyo tajwa kwa jina kwenye huu mkasa ingekuwa vyema na huyo mkuu wa Takukuru atajwe kwa jina.
   
 7. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  unajua takukuru wanafanya kazi gizani hawatajwi majina
   
 8. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  You should have abridged your story. Some find it boring to peruse such lengthy essays.
   
 9. aye

  aye JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  nchi imekwisha kabisa,tatizo wanapeana kazi kwa undugu hao police na kuwekana kwa maslahi yao sehemu za kazi.
   
 10. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  shenzi type
   
 11. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Je, lipi wanalo sema chadema ina chochea vurgu,mambo kama haya wanataka yafumbiwe macho?
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Acha uvivu uliopitiliza wewe, ka story kenyewe kafupi halafu unalalmika? hovyoooo!
   
 13. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina shaka kuwa mtoa maada na wafaasi wake ni vibaka.Je, hiyo tuhuma mliambiwa au mlishudia? Mwanaharakati halisi ni muungwana, muuwazi ,mzalendo na ufanya utafiti kabla ya kuripoti taarifa.Huwezi ukahukumu Jeshi zima la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa kosa la mtu mmoja.Tuacheni unafiki na uzushi.Mara ngapi polisi wameuawa wakilinda maisha yetu na mali zao?Ni taasi au wizara gani duniani isiyokuwa na mapungufu hasa ukizingatia kuwa na huko misikitini na makanisani kumejaa kashifa?
   
 14. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  He! Mkasa huo mbona cha mtoto,c bora huyo mama anakaa mjini,watu kama kova na huyo bw wa takukuru wanapata hata taarifa...chukua huu mkasa nilioukuta mkoani morogoro,wilaya ya ulanga,tarafa ya malinyi,kijiji cha biro...kuna bw m1,msukuma kwa kabila,alifiwa na mtoto wake wa umri wa miaka 2, (niseme tu kwanza hawa wasukuma wanaogopa polisi kuliko simba) kwa mujibu wa mtoa habari wangu kifo cha mtoto huyo kilisababishwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika. Na ukichukulia hawa mabwana wanaishi mbali mashambani. Kuna polisi m1 akasikia jamaa kafiwa akaenda kwa yule mfiwa na kumtetemesha kwa kumwambia yeye ndo kasababisha kifo cha yuke mtoto kwa uzembe wa kutompeleka mwanae haspitali,...basi,akamtaka jamaa ampatie Tsh milioni 2 la sivyo atamfungulia kesi ya mauaji. Msukuma wa watu akapiga hesabu akaomba apewe wiki 1,akauza mazao yake na ng'ombe akampatia polisi yule mshenzi tsh 2ml akatokomea zake. Mtoa habari wangu anadai hata OSS hajui hiyo deal. Imagine ndo wewe mwanao amekufa wanakuja wahuni wanakuchukulia na pesa ...matukio ni mengi!
   
 15. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  hapa simlaumu polisi....bado hatujaliwa...tutaliwa sana kwa sababu hatujishughulishi kujua nini haki zetu... ingekuwa Watanzania wajua haki zako..hii Tanesco ingeshafilisika kwa kulipa watu fidia... wajinga ndio waliwao!!!
   
 16. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145

  acha uvivu wewe angefupisha ungeelewa nini???
   
 17. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,754
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />

  Lazima huyo Baba ana issue sio bure...
   
 18. m

  mbasamwoga Member

  #18
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si mambo ya kuchekesha haya, mambo haya yapo sana.... askari wa usalama barabarani woooote ni wala rushwa mimi ni dereva naapa hawajasingiziwa huo mkasa. Pole sana Makamanda kama Jerry Muro ambao walidiriki hata kuuchokonoa uchafu wao, lkn kwa kudra za kishetani mpango wake uliiingiliwa na mahayawani. POLISI ni zaidi ya miungu watu. eeeh nchi yangu Tanzania nakulilia eeh Kova tunakutegemea. hali ni mbaya huku mabarabarani ndugu yetu. mchangiaji aliyetetea uozo huo wa polisi hana akili timamu, au yuko kwenye mfumo wa kifisadi. ipo siku................................ watalia na kusaga meno
   
 19. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />mkuu acha bwana,jamaa wanaogopa polisi c mchezo, yaani hata wewe ukivaa sare za polisi unachota mzigo. Mfano ng'ombe wa msukuma ale mazao ya mkulima,yasiyofikia hata miche 20 labda ya mahindi, hiyo ishakuwa deal,atakamatwa na atalipishwa si chini ya 300000 ,mgao unapita kwa mwenye shamba na polisi..udhaifu wa hawa jamaa ni kuwa anapesa, lakini hawajui haki zao.
   
 20. A

  Aine JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  very painful!!!!!
   
Loading...