Uozo mwingine wa CCM: Ofisi ya Pinda yatajwa ufisadi wa sh. 2.3 billioni

Haji Salum

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
1,022
394
Rujewa. Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeingia kwenye kashfa ya ufisadi wa Sh2.3 mil za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali baada ya viongozi wa CCM wilaya hiyo kuitaja waziwazi kwamba wanahusika katika kashfa hiyo ilitokea mwaka 2011/12.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo alimweleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea wilaya hiyo jana kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ni moja ya kikwazo kitakachosababisha CCM iwe na hali ngumu wilayani humu kutokana na kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa ufisadi huo.

Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo zilichakachuliwa kwa ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na kwamba mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri hiyo kwani madiwani sita walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM kwa tuhuma za kushirikiana na watendaji katika kutafuna fedha hizo

Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa karibnu na kwamba lazima zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani.

Source: Mwananchi
 
Mkuu slaa aliiba zaidi ya milioni 100 ambazo hadi leo hajawajibishwa aliweza kujikopesha kinyume na utaratibu zaidi ya min 80 akanunua nyumba mbweni hizi mbona husemi.
 
Mkuu tufanye uchambuzi na ruzuku za vyama zinavyoliwa na kutumiwa vibaya cdm wakiongoza na kutaka kutonywa kabla ya kukaguliwa.
 
Huu ni ukame wa fikra! Kwa hiyo unataka kusema unahalalisha wizi ndani ya CCM kwa vile mahali pengine kuna wizi pia? By the way mambo ya Slaa yameingiaje hapa?
 
Mkuu tufanye uchambuzi na ruzuku za vyama zinavyoliwa na kutumiwa vibaya cdm wakiongoza na kutaka kutonywa kabla ya kukaguliwa.
Duh! Kazi kweli kweli!!! Wewe ndiye umetumwa na CCM ili uwawakilishe hapa JF? Umeielewa thread lakini? Au ili mradi tu upate elfu saba ili watoto waende choo?
 
Hivi Kinana haamini kwamba CCM ina hali mbaya hadi akashuhudie mwenyewe?...
 
Mkuu slaa aliiba zaidi ya milioni 100 ambazo hadi leo hajawajibishwa aliweza kujikopesha kinyume na utaratibu zaidi ya min 80 akanunua nyumba mbweni hizi mbona husemi.
tunaomba tuthibitishie hilo mkuu kwa kutuweke akaunti au cheki au ofisi ilivunjwa nk. Otherwise yatakuwa ni majungu...
 
Back
Top Bottom