Uongozi, Waganga na Wauguzi Hospitali ya wilaya Chato (Kwa Magufuli) Wachunguzwe

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,736
Katika hali ya Kushangaza Hospitali inayotajwa kuwa ni ya Wilaya ya Chato ( kwa Magufuli) kuna utata mkubwa kuhusu wahudumu walioko Hospitali hapo kuwapatia huduma wagonjwa. Wagonjwa wengi wanaotoka pale wanajiuliza ni kwa nini ile isiitwe tu lituo cha afya. Waganga na Manesi waliopo hawana kabisa moyo wa kuwahudumia wagonjwa. Wanaolalamika sana ni wale ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi pindi wanapolazwa kupata huduma ni kwa tabu kwa sababu wao hawalipi. Watu wanapoteza maisha hivihivi.Wanaopata huduma pale au sie wana Chato tuna tabu, anayetaka kuhakikisha aende kimya kimya aingie wodini aone kinachoendelea na ikiwezekana awahoji walioko wodini ndo mtaamini maneno wanayoyasema. Siku hizi hatuna madaktari kama wa zamani. Siku hizi kuna madaktari - maaskari, wauguzi - mgambo. Yaani hawa watu utu hakuna wao wanataka pesa. Hakuna wanachofanya.

Kuna walioshuhudia wagonjwa wakifa kwa Pneumonia, wanajiuliza hospitali ( ya Wilaya) haina Oxygen Machine? Mwingine anatoka Thietre kafunukiwa nguo zake za nyumbani je hakuna hata Shuka safi la hospitali la kumfunika? Ni nini wanataka hawa wauguzi ili wawatibu Watanzania hawa. Mkuu Magufuli alivyokuwa serious kwenye mambo ya utendaji, lakini kwake huku watu wanastarere wagonjwa wanaangaika kisa huduma ni bure ( kwa wanaoishi na vvu), Swali najiuliza hata wale wanaolipa kwani fedha zinaingia mifukoni mwa wauguzi? Si zinalipiwa dirishani? au baadae wanakutana wanagawana? Kwa ujumla huduma ni mbovu anayetaka kuhakikisha hili aende Chato awaulize wananchi, waliowahi kulazwa pale au waliolazwa sasa watakueleza kilio kilichoko hapo lakini Uongozi kimya.

Wito wangu kwa Viongozi wa juu wa Serikali, kama mwananchi njooni mfanye uchunguzi mjionee, hali si Shwari. Fanyeni ukaguzi wa ghafla mtashangaa!!!! Wauguzi ni wengi lakini kinachofanyika hakionekani. Tatizo la nchi hii tukieleza matatizo ya wananchi utasikia wahusika wanasema leta ushahidi. Ushahidi upi? manataka mareremu aliyepoteza maisha kwa kukosa huduma afufuke atoe ushahidi? Kawaulizeni wananchi ndo mpate ushahidi. Ndo maana Msanii aitwaye ROMA aliimba kuwa wagonjwa wanakufa huku doctor anakunywa Valeur. Jamani viongozi chukueni hatua.
 
sio huko tu...nenda ofisi yeyote ya Serikali mikono mitupu uone...utaozea mapokezi...lakini ndo serikali mliyoichagua hiyo baada ya kupewa T-shirt na kofia..
 
Ni kila idara ya huduma siku hizi ni kichefuchefu!...!
Lakini yote haya yamepandikizwa na kukosekana kwa u'serious toka uongozi wajuu!
Kichwa cha Nazi!
 
siku zote huduma zinapokosekana hospital wanaolaumiwa ni wauguzi,madoc, jamani muuguzi atumie mshahara wake kununua dawa,oksijen machine,na mashuka? Doc yupo 1 theatre, opd,wodin,ctc, ataweza at same time? System imeharibika,kila m2 anavuna hata ambapo hapana mavuno,tutapata huduma nzuri kweli? Nguvu tunayo mikonon mwetu,just kuitumia 2. Mnh penyewe somtm watu wanafunikwa nguo zao kutoka theatre.
 
siku zote huduma zinapokosekana hospital wanaolaumiwa ni wauguzi,madoc, jamani muuguzi atumie mshahara wake kununua dawa,oksijen machine,na mashuka? Doc yupo 1 theatre, opd,wodin,ctc, ataweza at same time? System imeharibika,kila m2 anavuna hata ambapo hapana mavuno,tutapata huduma nzuri kweli? Nguvu tunayo mikonon mwetu,just kuitumia 2. Mnh penyewe somtm watu wanafunikwa nguo zao kutoka theatre.

Nyalotsi hapa tatizo ni kubwa mwana huwezi amini yaani hapa kama tatizo ni system ambalo ni political system mbona thread kama hii inahamishiwa kwenye JF doctor as if mimi nimeandika kuwa nina Ugonjwa wa ngono au ugonjwa mwingine naomba tiba. Huyu JF doctor atawafanya nini wauguzi wa Chato.
 
Back
Top Bottom