Uongozi wa Wilaya ya Kigamboni wawavua ukuu wa Shule walimu shule zilizoshika mkia NECTA

Ni moja ya njia za kuongeza uwajibikaji, kwa nini shule zingine zimefanya vzr? kwa nini wao tu? hongera sana WILAYA YA KIGAMBONI
Kwa yeyote mwenye akili fupi na ndogo kama wewe lazima atakuunga mkono lakini kwa mwenye akili angetafuta kwanza sababu na vyanzo kabla ya kuvua mtu madaraka, kwanza historia ya shule hizo tangu mwanzi zikoje na je tatizo ni mkuu wa shule, wanafunzi,walimu,vitendea kazi na mazingira au nini chanzo baada ya hapo hatua zinachukuliwa?? Hii yote sababu kufanya kazi kwa hisia kuliko utaalamu matokeo yake ndio hayo tunatatizo kubwa sana la ukosefu wa akili na tafakari kwa baadhi ya
viongozi.

Na nina hakika tanzania tuna watu wachache sana tena sana wenye uelewa mpana wa mambo.
Matokeo yametoka jana huo utafiti wa kujiridhisha kuwa mwalimu mkuu ndio chanzo umefanyika sangapi? Hii mizuka hii!!
 
Nimeona mahojiano sehemu ya hao walimu wa hiyo shule moja ya Kigamboni na wanafunzi waliobaki shuleni.

Wanafunzi kwa vinywa vyao wanasema walimu wanajitahidi sana kufundisha,tatizo ni wanafunzi.Na wanasema wanafunzi wengi walikuwa hawana nidhamu kwa kiasi kikubwa.

Na wanasema kama shule itakuwa imeshika mkia,basi tatizo sio walimu bali ni wanafunzi.Huu ni ushuhuda wa wanafunzi wa shule husika na si majirani.

Sasa unapochukua uamuzi wa kuwasambaratisha walimu na wewe kiongozi unabaki...Huu ni unafiki!!Kama kuanza wangeanza na Afisa Elimu wa Mkoa na hata Mkuu wa Mkoa ikibidi.

Kingine walimu wanalalamika kuwa hawa watoto wengi wanatoka maeneo ya Yombo Buzza na Mbagala,ili wafike shuleni mapema inawabidi waamke saa 10 au 11 alfajili na wanafika shuleni saa 3 asubuhi,na wanaondoka saa 8:30 mchana ili wawahi kufika nyumbani.

Kuna siku nilikuwa nimekaa na watoto sebuleni wanaangalia kipindi cha Skonga-EATV,ilikuwa ni hii shule ya Somangila.

Mtoto mmoja akaulizwa,nini maana ya nahau ya "Kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa".....Dogo akajibu kwa kujiamini "Kufanyiwa Masaji"....
Hata wewe naweza kukuuliza nahau moja na usijibu, tumia utaalamu kujadili maswala ya kitaalamu.
 
Na INDEX namba yake itakuwa ni ILE ILE kuazia shule ya msingi.

Sasa HAPATAKUWA na UDANGANYIFU wowote maana NAMBA ya mwanafunzi itajulikana TANGU akiwa SHULE ya MSINGI hadi CHUO KIKUU.
Nimekusoma mkuu, na inawezekana hapa kwetu wanajiandaa kufuata mfumo huo mana naona mwez jan mwishon wamesisistiza watoto wasajiliwe upya kwa majina matatu ambayo watapewa namba za usajili na watazitumia mpk sec. Itasaidia sana
 
Hilo ndio suluhisho la matokeo mabovu?

Wajiandae kuwavua na hao watakaowapa!
DC ndiye anatakiwa avuliwe ukuu wa wilaya kwa kutoshirikisha viongozi wenzake kuandaa mazingira mazuri ya kufundishia na kusoma.
Shule hazina ofisi na samani kwa ajili ya waalimu. Wanafunzi zaidi 100 darasani. Unatarajia nini.
 
tunaposema walimu wana changamotn mnatuelewa, mwalimu graduate na DED GRADUATE halafu unampigisha deki mwalimu! nitakuwa wa mwisho kukubali hayo mazoezi ohoo!
 
Kwa yeyote mwenye akili fupi na ndogo kama wewe lazima atakuunga mkono lakini kwa mwenye akili angetafuta kwanza sababu na vyanzo kabla ya kuvua mtu madaraka, kwanza historia ya shule hizo tangu mwanzi zikoje na je tatizo ni mkuu wa shule, wanafunzi,walimu,vitendea kazi na mazingira au nini chanzo baada ya hapo hatua zinachukuliwa?? Hii yote sababu kufanya kazi kwa hisia kuliko utaalamu matokeo yake ndio hayo tunatatizo kubwa sana la ukosefu wa akili na tafakari kwa baadhi ya
viongozi.

Na nina hakika tanzania tuna watu wachache sana tena sana wenye uelewa mpana wa mambo.
Matokeo yametoka jana huo utafiti wa kujiridhisha kuwa mwalimu mkuu ndio chanzo umefanyika sangapi? Hii mizuka hii!!
well said mkuu. Haya ni maamuzi kurupushi. Angeanza yeye kuresign kwanza, kwa kuwa na yeye alizembea mpaka watoto wakafeli.
 
Nimeona mahojiano sehemu ya hao walimu wa hiyo shule moja ya Kigamboni na wanafunzi waliobaki shuleni.

Wanafunzi kwa vinywa vyao wanasema walimu wanajitahidi sana kufundisha,tatizo ni wanafunzi.Na wanasema wanafunzi wengi walikuwa hawana nidhamu kwa kiasi kikubwa.

Na wanasema kama shule itakuwa imeshika mkia,basi tatizo sio walimu bali ni wanafunzi.Huu ni ushuhuda wa wanafunzi wa shule husika na si majirani.

Sasa unapochukua uamuzi wa kuwasambaratisha walimu na wewe kiongozi unabaki...Huu ni unafiki!!Kama kuanza wangeanza na Afisa Elimu wa Mkoa na hata Mkuu wa Mkoa ikibidi.

Kingine walimu wanalalamika kuwa hawa watoto wengi wanatoka maeneo ya Yombo Buzza na Mbagala,ili wafike shuleni mapema inawabidi waamke saa 10 au 11 alfajili na wanafika shuleni saa 3 asubuhi,na wanaondoka saa 8:30 mchana ili wawahi kufika nyumbani.

Kuna siku nilikuwa nimekaa na watoto sebuleni wanaangalia kipindi cha Skonga-EATV,ilikuwa ni hii shule ya Somangila.

Mtoto mmoja akaulizwa,nini maana ya nahau ya "Kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa".....Dogo akajibu kwa kujiamini "Kufanyiwa Masaji"....
Ukweli utabaki kuwa ukweli watafukuza sana watakuwa hajatatua tatizo hizo hasara za kukurupuka sasa kama walimu wanajitahidi kufundisha kwa bidii pamoja na mazingira magumu wanakuja kufukuzwa wakati mwingine hizi ajira za kuajiriwa ni utumwa.
 
Kwa yeyote mwenye akili fupi na ndogo kama wewe lazima atakuunga mkono lakini kwa mwenye akili angetafuta kwanza sababu na vyanzo kabla ya kuvua mtu madaraka, kwanza historia ya shule hizo tangu mwanzi zikoje na je tatizo ni mkuu wa shule, wanafunzi,walimu,vitendea kazi na mazingira au nini chanzo baada ya hapo hatua zinachukuliwa?? Hii yote sababu kufanya kazi kwa hisia kuliko utaalamu matokeo yake ndio hayo tunatatizo kubwa sana la ukosefu wa akili na tafakari kwa baadhi ya
viongozi.

Na nina hakika tanzania tuna watu wachache sana tena sana wenye uelewa mpana wa mambo.
Matokeo yametoka jana huo utafiti wa kujiridhisha kuwa mwalimu mkuu ndio chanzo umefanyika sangapi? Hii mizuka hii!!
Ingawa kwa hali hii

CSEE 2016 EXAMINATION RESULTS

S2879 KIDETE SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0; DIV-II = 0; DIV-III = 1; DIV-IV = 34; DIV-0 = 95

Na hali nyingine hii

CSEE 2016 EXAMINATION RESULTS

S1965 SOMANGILA DAY SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 0; DIV-II = 0; DIV-III = 2; DIV-IV = 8; DIV-0 = 45

Kweli hapa uchunguzi unatakiwa ufanyike kwanza kabla ya hatua hizo ili kila aliye stahili adhabu aadhibiwe kwa nafasi yake. Kuwavua wakuu pekeyake haitoshi na haita tatua tatizo kabisa,hapo yabidi akili kubwa,
 
Uzembe wa viongozi wa Ccm ndio huo wakifanya vibaya wanawasingizia walimu wakuu kwani ndio wanafeli??? Basi hata mkuu wa mkoa mungu wa Dar avuliwe ukuu wa mkoa aisee
 
Sitaki hata kusoma kilichojiri. Kama huo ndo uamuzi sahihi basi kila mtu kwa nafasi yake awajibike. Haitoshi kuwawajibisha wakuu wa shule tu. Nanyi maafisa elimu ngazi zote Kigamboni ng'atukeni. Utakaliaje hicho kiti kwa wadhifa wako ilihali mambo hayako sawa? Kumbuka utendaji wenu unategemeana sana ili kufikia lengo. Imetosha kwa uonevuu kwa walimu. Sio haki hata kidogoo. Walimu kote nchini pazeni sauti zenu tafadhali. Serikali pia ijitafakari kwani hata hizo shule bora sio zenu. Acheni matamko uchwara

WALIMU SEMENI HAPANA KUUUUBWA KWA UONEVU HUUU

IMETOSHAAAAAA
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli watafukuza sana watakuwa hajatatua tatizo hizo hasara za kukurupuka sasa kama walimu wanajitahidi kufundisha kwa bidii pamoja na mazingira magumu wanakuja kufukuzwa wakati mwingine hizi ajira za kuajiriwa ni utumwa.
Hawajafukuzwa mkuu wameshushwa vyeo
 
kwa hio mimi huwa nashindwa kuelewa ina maana Wakuu wa shule ni chanzo cha wanafunzi kufeli? Na kumbukeni katika elimu kuna kufeli na kufaulu.Kwa mawazo ya WaTz wanajua lengo la shule ni kufaulisha wanafunzi.Elimu ni pana jaman ni zaidi ya kufaulu
 
Back
Top Bottom