Uongozi wa Wilaya ya Kigamboni wawavua ukuu wa Shule walimu shule zilizoshika mkia NECTA

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg
[HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Uongozi wa WILAYA ya Kigamboni umetangaza kuwavua nafasi za ukuu wa shule wakuu wa shule za Kidete na Somangila Day baada ya shule hizo kufanya vibaya zaidi katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016

Chanzo:ITV
 
View attachment 466096 [HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Uongozi wa WILAYA ya Kigamboni umetangaza kuwavua nafasi za ukuu wa shule wakuu wa shule za Kidete na Somangila Day baada ya shule hizo kufanya vibaya zaidi katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016

Chanzo:ITV
Huu ndio wendawazimu sasa wanafunzi hawasomi ,waki adhibiwa wanawafukuza kazi wanafunzi
 
Ni moja ya njia za kuongeza uwajibikaji, kwa nini shule zingine zimefanya vzr? kwa nini wao tu? hongera sana WILAYA YA KIGAMBONI
 
View attachment 466096 [HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Uongozi wa WILAYA ya Kigamboni umetangaza kuwavua nafasi za ukuu wa shule wakuu wa shule za Kidete na Somangila Day baada ya shule hizo kufanya vibaya zaidi katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016

Chanzo:ITV
Jamani tatizo si WALIMU WAKUU.Tazizo ni MFUMO wa ELIMU yetu ni MBOVU.
Ndo maana jirani zetu Wakenya wameamua kuuacha mfumo huu wa MITIHANI ya KUKARIRI na inasikika wataanza mwezi wa 5 mwaka huu kama PILOT project ya kutumia CAT Continuous Assessment Test. Kama wanavyofanya ULAYA na Marekani.

CAT ina maana KILA mtoto ana HAKI yakufika elimu ya SECONDARY na hata CHUO KIKUU kulingana na UWEZO wake KADRI alivyofanya MITIHANI ya kila mwaka tangu shule ya MSINGI hadi SEKONDARI. Na INDEX namba yake itakuwa ni ILE ILE kuazia shule ya msingi.

Sasa HAPATAKUWA na UDANGANYIFU wowote maana NAMBA ya mwanafunzi itajulikana TANGU akiwa SHULE ya MSINGI hadi CHUO KIKUU.

Na hivyo hakuna mwingine ANAWEZA KUITUMIA maana jina LITAKATAA!

Katika mfumo huu itazingatiwa TALENT/TALANTA pamoja na INTEREST/DHAMIRA ama Mwanafunzi NINI HASA ni UWEZO wake.

Katika hilo inasemekana kuna UWEZEKANO mkubwa wa kupata WANASAYANSI, na WATAALAMU aina tofauti.
Na ifikapo mwakani mwezi wa Januari WATAUSAMBAZA nchi nzima.
Wanavyosema MITIHANI ilikuwa ni MITINDO ya WAKOLONI kupata watu wa kufanya kazi maofisini na si kuwapa UJUZI wa kujitegemea maishani.

KUWAFUKUZA walimu wakuu HAKUTATATUA chochote.SULUHISHO ni kuwa ni lazima MFUMO MZIMA wa ELIMU yetu Tanzania pia UBADILISHWE kulingana na NYAKATI!
 
Hii nchi haina maafisa elimu?
Wakuu wa wilaya hawajui walifanyalo?Ni mkuu yupi wa wilaya aliyetembelea shule hizo mwaka jana au mwaka huu ili kuona vchangamoto na kuzitatua?
Kama hivyo vyeo walipewa na wakuu wa wilaya basi acha tuone.
 
Nimeona mahojiano sehemu ya hao walimu wa hiyo shule moja ya Kigamboni na wanafunzi waliobaki shuleni.

Wanafunzi kwa vinywa vyao wanasema walimu wanajitahidi sana kufundisha,tatizo ni wanafunzi.Na wanasema wanafunzi wengi walikuwa hawana nidhamu kwa kiasi kikubwa.

Na wanasema kama shule itakuwa imeshika mkia,basi tatizo sio walimu bali ni wanafunzi.Huu ni ushuhuda wa wanafunzi wa shule husika na si majirani.

Sasa unapochukua uamuzi wa kuwasambaratisha walimu na wewe kiongozi unabaki...Huu ni unafiki!!Kama kuanza wangeanza na Afisa Elimu wa Mkoa na hata Mkuu wa Mkoa ikibidi.

Kingine walimu wanalalamika kuwa hawa watoto wengi wanatoka maeneo ya Yombo Buzza na Mbagala,ili wafike shuleni mapema inawabidi waamke saa 10 au 11 alfajili na wanafika shuleni saa 3 asubuhi,na wanaondoka saa 8:30 mchana ili wawahi kufika nyumbani.

Kuna siku nilikuwa nimekaa na watoto sebuleni wanaangalia kipindi cha Skonga-EATV,ilikuwa ni hii shule ya Somangila.

Mtoto mmoja akaulizwa,nini maana ya nahau ya "Kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa".....Dogo akajibu kwa kujiamini "Kufanyiwa Masaji"....
 
Acha ujinga wewe ,kichwa chako hakifanyi kazi ,hivi unadhani mwalimu mkuu ndio chanzo...
Siyo hivyo lakini mkuu wa Wilaya anaona hiyo ndiyo tangible action ambayo wakubwa wake wataiona na kumpongeza.
 
Kama hawajawasikiliza walimu hao sababu za shule zao kushika mkia...basi uonevu umefanyika.
 
Back
Top Bottom