Uongozi wa TANROADS Pwani na Unyanyasaji wa Wafanyakazi, Watatu wasimamishwa kazi

Tatizo kubwa kwa wafanyakazi wengi wa Tanzania hawajui kupigania haki zao, mtu anafukuzwa kazi kienyeji tu bila utaratibu lakini naye anaridhika.
Lakini pia kuna udhaifu mkubwa katika ajira hizi za contracts ambazo mameneja wa tanroads wa mikoa ndio wenye final say kwenye ajira zao. Binafsi sioni sababu ya msingi ya kutowapa permanent contracts kama wanavyofanya kwa wafanyakazi wengine wa mizani. Kwanini weighbridge operators tu ndio waajiriwe kwa contracts?

sasa hapo ndipo pa kuanzia unajua wanawepa kuwa na full responsibility kama wakiwaajairi permanent but wako kazini lazima wawatendee haki wawape ajira ya kudumu na pia iwe na terms zinazokubalika.
 
yote kwa yote pamoja na ukiukwaji mkubwa tena wa makusudi wa kisheria kumkamata na kumuweka ndani mjamzito bila ushahidi wowote tena kumnyima haki yake ya dhamana ni zaidi ya ukatili na haikubaliki.

Taasisi za akina mama na watoto,haki za binadamu lazima zifahamu unyama huu! Chama cha wanasheria wanawake lazima kimsaidie mjamzito huyu kuwafunza adabu wote hasa huyo OCCID wa Kibaha!

Najua wadau wakubwa wa haki za binadamu wanapita hapa,lazima tuadabishane wenyewe hadi nidhamu irudi!!!
 
sasa hapo ndipo pa kuanzia unajua wanawepa kuwa na full responsibility kama wakiwaajairi permanent but wako kazini lazima wawatendee haki wawape ajira ya kudumu na pia iwe na terms zinazokubalika.

Kutokana na uhaba wa ajira uliopo nchini, na kwakuwa vijana wengi elimu yetu imetufanya tuwe tegemezi wa kuajiriwa badala ya kujiajiri, sasa wanajikuta wanakubali kuajiriwa kwa terms ambazo ni mbovu sana kwakweli.

Fikiria mtu anaajiriwa kwa mshahara wa Tsh.121,500/- lakini anajitegemea kwa matibabu, posho ya usafiri, posho ya nyumba, posho ya nauli ya likizo, kwahiyo mwajiri hana responsibilties zozote kwa huyu mwajiriwa, na huyu mwajiri ni serikali sasa hapo ndipo kuna shida kubwa sana, kwamba serikali ndiyo isiyojali kabisa maslahi ya wananchi/wafanyakazi wake tena katika maeneo sensitive kama mizani.
 
Hii mifumo inayochochea rushwa ndiyo tunatakiwa kupambana nayo ili tuikomeshe na kuleta tija na uwajibikaji katika serikali yetu.
Nimeambiwa pale mizani ya kibaha kuna kamera za cctv zinzorekodi matukio yote, magari yanayopita pamoja na watu wanaovyofanya kazi ofisini. Kama kuna tuhuma za rushwa kwanini wasitumie ushahidi wa picha za cctv kubainisha ukweli? hapa lazima kuna mchezo mchafu wanachezewa hawa vijana.

Mkuu kuweka cctv ni hatua nzuri sana ila tunatakiwa kuja na solution kubwa zaidi ya tatizo la rushwa tunapaswa kujenga uzalendo wa hali ya juu kwa hii nchi na kuwafanya watu kuchukuia rushwa kabisa kwa mtoaji na mpokeaji bila hivyo watu watakuja na mbinu tu za kucheza na hizo cctv kwa mfano wanaweza kukupa maagizo ya kumpa rushwa mtu aliye nje ya hilo eneo kwa niaba yao mfano mwenye kiosk karibu au shoe shine tunaona sana hii michezo
 
yote kwa yote pamoja na ukiukwaji mkubwa tena wa makusudi wa kisheria kumkamata na kumuweka ndani mjamzito bila ushahidi wowote tena kumnyima haki yake ya dhamana ni zaidi ya ukatili na haikubaliki.

Taasisi za akina mama na watoto,haki za binadamu lazima zifahamu unyama huu! Chama cha wanasheria wanawake lazima kimsaidie mjamzito huyu kuwafunza adabu wote hasa huyo OCCID wa Kibaha!

Najua wadau wakubwa wa haki za binadamu wanapita hapa,lazima tuadabishane wenyewe hadi nidhamu irudi!!!

Ndio maana niliomba kama kuna mwanasheria hapa JF atusaidie kufafanua kuhusu haki ya dhamana kwa mtuhumiwa, na labda atatusaidia zaidi kuhusu handling ya mtuhumiwa anapokuwa mjamzito tena ujauzito mkubwa kiasi cha miezi saba hivi.
Kama kweli hizi taasisi za kutetea haki za wanawake zinapita humu basi wafuiatilie suala hili polisi kibaha na tanroads kibaha watajua mengi, na huenda wakasaidia sana kuwanusuru akina mama na huu unyanyasaji wa polisi.

Ingawa pia nimependa sana courage ya mume wa yule binti kwa jinsi alivyoweza kukabiliana na OCCID kwa hoja nzito hadi akaamua kutoa dhamana. Tunatakiwa tusiwaogope hawa polisi tujitahidi kuwakabili kwa ujasiri.
 
Mkuu kuweka cctv ni hatua nzuri sana ila tunatakiwa kuja na solution kubwa zaidi ya tatizo la rushwa tunapaswa kujenga uzalendo wa hali ya juu kwa hii nchi na kuwafanya watu kuchukuia rushwa kabisa kwa mtoaji na mpokeaji bila hivyo watu watakuja na mbinu tu za kucheza na hizo cctv kwa mfano wanaweza kukupa maagizo ya kumpa rushwa mtu aliye nje ya hilo eneo kwa niaba yao mfano mwenye kiosk karibu au shoe shine tunaona sana hii michezo

Ni kweli cctv camera haziwezi kumaliza rushwa isipokuwa inasaidia kupunguza, binadamu siku zote ukimkabili kwa mbinu moja anakukabili kwa mbinu ya pili. Katika kesi hii wanaweza wasionekane wakichukua rushwa labda waliwatumia "mashoe shiners" kama unavyosema lakini angalau magari yale yangeonekana yakiingia kwenye mzani na vipimo vyake vingeonekana.
 
Naendelea kufuatilia kuona kama kuna harufu ya undugunization au tatizo ni dini ingawa kwa hawa watatu si wa dini moja, miongoni mwao wapo wa dini zetu mbili kubwa zinazotusumbua hapa nchini.

Hebu chunguza vizuri mkuu, ukikuta majina ya hao vijana yanaishia na Mungi, Maranya, Yakhe, basi ujue tatizo ni undugunaizesheni, hao waliingia kwenye sistim kwa bahati mbaya.
 
Suala la kurenew mkataba nadhani litakuwa gumu kwa mazingira yaliyopo. Sasahivi wanafanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja, na renewable subject to satisfactory performance. Kwa taarifa nilizopata wengi wamekuwa wakifukuzwa bila kumaliza japo huo mwaka mmoja, tena hawa jamaa nimeambiwa hawana muda wa kufanya hearing kwa mfanyakazi anapotuhumiwa, wananchojua ni kufukuza tu.

Kuhusu tuhuma za rushwa kwa wafanyakazi wa mizani zimekuwepo sana lakini viongozi wa tanroads ndio wanaochangia hali hiyo. Fikiria mtu analipwa mshahara wa shilingi laki moja na thelathini na tano elfu (Tsh.135,000/-) kwa mwezi kama gross. Katika hali kama hiyo unategemea wafanyeje kama sio kuwaweka katika mazingira ya rushwa, tena rushwa yenyewe wanashawishiwa na ma transporter.

Lakini vilevile katika hali ya kukabiliana na rushwa mizani sasahivi kumewekwa kamera (cctv cameras) kwahiyo mazingira ya rushwa yamedhibitiwa kwa kiwango kikubwa sana kama si kuisha.

Cha kushangaza kazi ambayo ina temptation ya rushwa kama hiyo unapoamua kulipa mshahara kiduchu kama huo na kutoa mikataba mifupi maana yake unaweka mazingira ya rushwa moja kwa moja. Fikiria hujui hatima yako baada ya mwaka mmoja na pia mshahara unaolipwa haufiki hata tarehe kumi kwa gharama za maisha ya sasa,,, halafu kuna gari imezidisha uzito wanakushawishi uchukue rushwa ya mshahara wa mwaka mzima ndani ya siku moja,,, inahitaji roho ya konokono kukataa
Kwa ujumla job design serikalini iko very poor and subjective, inachochea rushwa na utendaji hafifu. Hopeful huyo meneja wa tanroads ataona aibu, hasa ukizingatia kuwa Dr Magufuli huwa anachungulia huku
 
Hivi hawa wendawazimu wanajua gharam ya kuwasomesha hawa jamaa na kuwepo kwao nje kunaongeza hasara gani?Hawa wanadhani hisia zao kingono,kikabila, n.k ni kubwa kuliko taifa na familia za watu?
 
Mimi sipo sana kwenye uhalifu wa mizani, kwani mimi ni mdau wa usafirishaji na ukweli ni kwamba kuna matatizo ya mfumo wa mizani ingawa kwa sasa umeboreshwa sana lakini bado kuna mapungufu ya utendaji na uongozi, inabidi ifanyike kazi ya ziada huko.

Ntajikita kwenye uonevu wa Polisi. Hao vijana ni bahati yao wamepewa dhamana siku hiyo hiyo. Niliandika humu JF habari ya watu waliokaa siku 9 bila dhamana hapo kituo cha Wazo Hill. Ni uhakika kabisa kuna ukiukaji wa sheria kwenye jeshi la Polisi, hili sipingi.
 
Mkuu matatizo kama hayo yaliwahi kutokea pale nssf, baadhi ya watu walibambikiziwa tuhuma, lakini baadaye iligundulika kuwa majina yao ndiyo ilikuwa tatizo. Dr. Dau nadhani aliwekwa pale na mkulu kwa kazi maalum.

Tusipoupiga vita udini na undugunaizasheni bado hii dhambi itaendelea kuwatesa watanzania masikini wasio na majina!
Mungi,

Mimi naona wewe una chuki binafsi na Dr Ramadhani Dau.

Kwani mimi namjua vizuri sana Dr Ramadhani Dau si tu tumekuwa pamoja UDSM (yeye akiwa mbele) lakin vile vile tukiwa wote tukitokea Kariakoo wakti huo.

Kumbuka huyu ni PhD holder na amefundisha UDSM, amekuwa bandari na baadae NSSF. Anafaa kwa vigezo vyote kuanzia Ilmu yake na hata uzoefu wake.

Lakin msingi mkuu ninaoshindwa kuwaelewa watu kutoka Bara. Tanganyika kuna mashirika mengi sana ya pensheni kama GPF, PPF, LPF,n.k na hata bodi ya uthibiti wa mashirika hayo. Ukiangalia kwa kina viongozi wake wote ni wa kutoka upande wa Pili.

Jamani Shirika hilo moja tu kushika huyu MDINI ndio imekuwa Nongwa.

nafikiri mchaguane sio kwa kigezo cha DINI bali kwa WELEDI. kama una dought na ILMU ya Dr Ramadhani Dau sema tukueleze.

Kumbuka Sumu ya UDINI ni mbaya kuliko bomu la Nyuklia.



 
Mkuu Mwita Maranya nasikia juzi waziri Dr. John Pombe Magufuli katangaza kuwa watu wa mizani ndio vigogo wa kula rushwa! Vipi hapo Kibaha hakuna rushwa?
 
Last edited by a moderator:
Kwanini ni lazima wafanye kazi mizani? Tanzania inatakiwa iketwe sera ya fire and hire. Immediate boss awe na uwezo wa kufukuza na kuajiri. Upuuzi huu wote utaisha. Mwita Maranya acha watu wafanye kazi. Rushwa zao zinztuingiza hasara kwa barabara zetu kubomolewa na magari yenye uzito mkubwa.
 
Back
Top Bottom