Uongozi wa TANROADS Pwani na Unyanyasaji wa Wafanyakazi, Watatu wasimamishwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa TANROADS Pwani na Unyanyasaji wa Wafanyakazi, Watatu wasimamishwa kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwita Maranya, Oct 9, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Salam wanaJF,

  Katika pitapita zangu katika viunga vya TANROADS mkoa wa Pwani nimekutana na sakata hili, nami nikaona niwashirikishe ili kwa pamoja tuone kama kuna jambo tunaweza kuishauri Tanroaads ama wizara ya ujenzi juu ya uendeshaji wa mizani zilizoko maeneo mbalimbali nchini.

  Katika muendelezo wa vitendo vya unyanyasaji kwa wafanyakazi wake hasa wale wa mikataba ambao ni weighbridge operators, uongozi wa TANROADS mkoa wa Pwani unatuhumiwa kuwasimamisha kazi wafanyakazi watatu kinyume na taratibu na kanuni za ajira. Kisa kizima kama nilivyokinasa kiko hivi;

  WAKAMATWA NA POLISI.

  Mnano mwanzoni mwa mwezi wa tisa wafanyakazi watatu, vijana wa kiume wawili na binti Mmoja walivamiwa na kukamatwa na polisi wakiwa kazini mizani ya kibaha majira ya saa 11 jioni. Walipofikishwa kituo cha polisi Kibaha (Tumbi) walielezwa kwamba wanatuhumiwa na mwajiri wao kwa kosa la kula rushwa na kupitisha gari katika mzani wa kibaha, gari zilizodaiwa kuzidi uzito unaokubalika kisheria. Baada ya kumaliza mahojiano na OCCID waliwekwa rumande na kukataliwa dhamana kwa maelezo kwamba bosi wao ambaye ni mkuu wa mizani mkoa wa Pwani bw. Simfukwe aliwataka polisi kutowaachia watuhumiwa hao kwakuwa wangeweza kutoroka. Pamoja na ukweli kwamba binti alikuwa ni mjamzito wa miezi sita au saba hivi lakini walimsweka ndani bila kuzingatia hali yake.

  NDUGU ZAO WAFIKA KUWAWEKEA DHAMANA, WAKATALIWA.
  Baada ya kuwataarifu ndugu zao kuhusu kukamatwa kwao na kuzuiliwa polisi Kibaha, ndugu wa vijana wawili wa kiume walifika polisi Kibaha kuwatolea dhamana lakini walikataliwa kwamba polisi haitawezekana kuwawekea dhamana usiku ule na kuwataka warudi kesho yake, hivyo kuondoka na kuwaacha ndugu zao. Mume wa binti alifika polisi Kibaha muda wa saa 2 usiku ili kumuwekea dhamana mke wake lakini akaelezwa na askari polisi waliokuwepo kituoni muda huo kwamba wasingeweza kutoa dhamana kwa mtuhumiwa kwa muda ule wa usiku. Yule bwana alipojaribu kuwahoji sababu za msingi za kumnyima dhamana mke wake, polisi walimueleza kwamba Mwenye mamlaka ya kutoa dhamana ni OCD ama OCCID, lakini wakamshauri awasiliane na OCCID ambaye ndiye alikuwa anawahoji watuhumiwa wale.

  Yule bwana akampigia simu OCCID (Namba zao za simu zipo pale Counter) baada ya mazungumzo ya muda kidogo OCCID akadai kwamba hataweza kumpa dhamana kwakuwa ilikuwa ni usiku na yeye bado hajawahoji. Yule bwana akamuuliza ni kwa mujibu wa sheria gani anayotumia OCCID kuzuia dhamana ya mtuhumiwa na kudai kwamba hatoi dhamana usiku? Hapa nitaomba wanasheria mtusaidie kama kuna sheria inayozuia dhama wakati wa usiku, ikiwa polisi wanaweza kumkamata mtuhumiwa wakati wowote hata usiku. Baada ya mabishano ya muda kidogo OCCID akakata simu na baadae akawasili kituo cha polisi na kuanza kumhoji Yule bwana kwanini anataka kumfundisha kazi, kukatokea majibizano kidogo lakini hatimaye Yule binti akapatiwa dhamana na wale vijana wawili nao wakaambiwa kama wana wadhamini basi dhamana yao iko wazi, wakawapigia simu ndugu zao waliokuwa karibu na kudhaminiwa usiku kama saa tano hivi na kuwataka warudi kituoni kesho yake.

  WASIMAMISHWA KAZI
  Baada ya kutoka polisi walielekea ofisini kwa bosi wao Mr. Simfukwe ili kujua kinachoendelea. Baada ya kufika ofisini waliambiwa kwamba wamesimamishwa kazi hadi hapo kesi yao iliyopo polisi itakaokamilika, baada ya kuelezwa hivyo wakamuomba barua ya kusimamishwa kazi. Kusikia hivyo ikabidi mkuu wa mizani mkoa, meneja muajiri pamoja na meneja wa Tanroads mkoa waitane kikao cha dharura ili kujua nini cha kufanya. Baada ya kikao hicho wakawataka watuhumiwa wawe wanaripoti ofisi ya mkoa kila siku bila kufanya kazi lakini pia kwa mara ya kwanza wakawaapatia barua na kuwapa siku mbili na kuwataka wajieleze kuhusiana na tukio la magari(malori) mawili yanayosadikiwa kupata katika mzani wa kibaha yakiwa yamezidisha uzito. Wale vijana wakajibu barua zile na kuendelea kuripoti ofisini kwa meneja wa Tanroads mkoa na at the same time wakiripoti kwa OCCID Kibaha.

  WAKAMATWA NA KUHOJIWA NA TAKUKURU
  Wakati polisi wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo uongozi wa Tanroads mkoa wa Pwani wakaamua kuwapeleka vijana wale kuwashitaki katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Pwani. Maofisa wa Takukuru wakawakamata na kuwahoji juu ya tuhuma zinazowakabili, baada ya mahojiano marefu wakawaachia bila masharti yoyote na kuwataka wawe tayari kufika ofisini kwao muda wowote watakapowahitaji kwakuwa walikuwa wanaendelea na uchunguzi wa tuhuma zile.

  AJIRA ZAO ZIKO MASHAKANI
  Takribani mwezi Mmoja tangu wakamatwe, kuhojiwa na polisi pamoja na Takukuru, vyombo vyote viwili vimeshindwa kuwafikisha mahakamani kwakuwa Hakuna ushahidi wowote wa kuwapeleka mahakamani. Pamoja na kukosekana ushahidi wa kuwapeleka mahakamani lakini bado uongozi wa Tanroaads Pwani umeshindwa kuwarejesha kazini na taarifa zilizovuja hivi karibuni ni kwamba wanatafuta sababu za kuwafukuza kazi kwakuwa wanaona itakuwa aibu kwao kwa namna walivyoshindwa kulishughulikia tatizo hilo kwa weledi hadi sasa Polisi na Takukuru wamewaeleza kwamba Hakuna ushahidi wowote wa kuwashitaki.

  UKIUKWAJI WA TARATIBU NA KANUNI ULIOFANYWA NA UONGOZI WA TANROADS MKOA WA PWANI.
  Katika hali ya kawaida baada ya uongozi kupata taarifa/tuhuma za rushwa dhidi ya wafanyakazi wake kitu cha kwanza walitakiwa kuwahoji watuhumiwa, kwa kuwaandikia barua na kisha kufanya nao mahojiano ili kujiridhisha kama kulikuwa na ukweli wowote katika tuhuma hizo. Lakini katika hali ya kushangaza uongozi huo ukaamua kuwakamata na kuwapeleka polisi na kisha Takukuru kitendo ambacho hata maofisa wa polisi na Takukuru wenyewe wamekishangaa, kwamba wamekurupuka kufanya vitu kama watu wasiokwenda shule. Meneja rasilimali watu (HR Manager) haonekani kujua sheria, kanuni na taratibu za kinidhamu kwa watumishi kwani yeye ndiye alitakiwa kuwashauri meneja wa Tanroads pamoja na mkuu wa mizani utaratibu wa kinidhamu dhidi ya wafanyakazi lakini inaonekana naye hana uwezo ama hajui majukumu yake.

  SUALA LENYEWE LILIVYOANZA
  Malori mawili yalipopimwa katika mzani wa kihonda Morogoro yalionekana kuzidisha uzito unaokubalika kisheria na hivyo kutakiwa kulipa faini na kupunguzwa uzito. Dereva na Mwenye malori walishangazwa na kitendo hicho kwani katika mizani za kibaha (Pwani) na mikese (Morogoro) malori hayo yalikuwa na uzito wa kawaida unaokubalika. Lakini uongozi wa Tanroads Pwani wakawageuzia kibao watumishi wao kwamba walikula rushwa na kupitisha malori hayo bila kujiuliza kwamba mzani wa mikese nao ulitoa vipimo vya kuonyesha kwamba magari yale hayakuzidi uzito. Kwa ufafanuzi zaidi mizani za Kibaha na Mikese ni Electronics wakati wa Kihonda ni Manuaal, kwahiyo mara nyingi umekuwa ukiitoa vipimo tofauti na mizani nyingine za electronics.

  Baada ya kufuatilia Kumbukumbu za magari yaliyopita mizani ya kibaha ilionekana gari moja haikupita hapo na hivyo tajiri akabanwa aeleze gari hiyo ilipita wapi kwakuwa tiketi aliyokuwa nayo ni ya gari tofauti na iliyokamatwa kihonda. Mwishowe iliamuliwa tajiri Mwenye malori apigwe faini kwa kuzidisha uzito wa mizigo katika magari yake lakini pia alipigwa faini ya TRESS PASS kwa gari moja ambayo haikuonekana kupata mizani ya kibaha na hivyo suala hilo kuonekana kuishia hapo lakini baada ya wiki moja ndipo mkuu wa mizani Mr. Simfukwe akaibuka na tuhuma dhidi ya wafanyakazi wake.


  HALI ILIVYO KWA SASA
  Bado wafanyakazi hawa hawajui hatma ya ajira zao pamoja na Takukuru na Polisi kuwaambia Tanroads Pwani waziwazi kwamba Hakuna ushahidi wowote wa kutosheleza kuwafungulia kesi. Uongozi wao umeendelea kukaa kimya bila kutoa maamuzi yoyote, wametakiwa kuripoti ofisini kwa meneja wa Tanroads mkoa kila siku za jumatatu hadi ijumaa wanasaini na kuondoka kila siku.

  Ushauri wangu kwa uongozi wa Tanroads mkoa wa pwani wanatakiwa wafanye kazi zao kwa weledi, waache unyanyasaji kwa wafanyakazi wao bali wajitahidi kuwapa morali ya kazi kwani wafanyakazi wengi wanafanya kazi zao kwa wassiwasi na mashaka makubwa kwakuwa kumekuwa na tabia ya kufukuzana kazi kila mara bila sababu za msingi.

  Pia niushauri uongozi wa Tanroads makao makuu pamoja na wizara ya ujenzi, wajitahidi kuwamonitor kwa karibu sana hawa mameneja wa mikoa pamoja na wakuu wa mizani kwakuwa wamekuwa wasumbufu sana kwa wafanyakazi wao. Ni ajabu na kweli kwamba uongozi unafanya maamuzi ya kizembe kama haya ya kuwasimamisha kazi ama kuwafukuza kazi wafanyakazi bila kuwapa haki yao ya msingi ya kuwasikiliza/ kujitetea.

  Naomba kuwasilisha wadau.


  Nakala; TUMBIRI, Matola, Nguruvi3, Mag3, AshaDii, Nicholas, Ngongo, Mungi, Crashwise, Rutashubanyuma, Barubaru, chama, Molemo, Mtambuzi, Asprin, zion gfsonwin, Saharavoice, almasiomary, Ritz, zomba, Ben Saanane, KOMBAJR, MTAZAMO, mgeni wenu, Ng'wanangwa, Ulukolokwitanga, Preta, Riwa, Manumbu, Somoche, Omokora Nyangi, Sabayi, jogi, Dark City, TUNTEMEKE, Invisible
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwita Maranya kuna ushahidi wa kimazingira unatafutwa hapo ili vijana watemeshwe ajira zao,ikiwa Polisi,TAKUKURU wameshindwa kuwafikisha Mahakamani na mwajiri ameshindwa kuwaachisha/kuwafukuza kazi kama kweli upo ushahidi wa makosa yaliyotendwa unategemea nini hapo ?.

  Kama gari limepima mizani ya Chalinze likasafiri umbali wa kilometa 200 au 400 likakutwa limezidisha uzito unaweza kweli kuwalaumu wapimaji wa Chalinze ?.Nimewahi kusafiri na mabus mengi ya Dar kwenda Arusha wakifikia njia panda [Himo] wanawahamishia abiria kwenye mabu madogo kabla ya kupima uzito wakishapita abiria wanachukuliwa tena mbele ya mizani.Hivi ikitokea bus lililofanya utaratibu wa kupunguza abiria baadae likakamatwa mbele ya safari utawalaumu makarani wa mizani ?.

  Nadhani msimamzi wa mizani alitakiwa achunguze kwanza kabla ya kuchukua hatua zozote kuepuka kugandamiza either parties [wafanyakazi au wasafirishaji].
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa la TANROADS na hizi mizani zao ajra huwa zinatolewa kwa kujuana. Hii idara sio equal opportunity employers ndio maana wanafikiri kama wanaweza kuajiri kwa upendeleo wataweza pia kuwatoa kazini kwa upendeleo.
  Hapa huenda haki haitatendeka wakati wa ku renew mkataba wa ajira ya hawa jamaa kwa kuwa huwa wanapewa miezi mitatu...

  But idara ya mizani ni moja ya idara zinazotajwa sana linapokuja suala la kupokea rushwa...
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu matatizo kama hayo yaliwahi kutokea pale nssf, baadhi ya watu walibambikiziwa tuhuma, lakini baadaye iligundulika kuwa majina yao ndiyo ilikuwa tatizo. Dr. Dau nadhani aliwekwa pale na mkulu kwa kazi maalum.

  Tusipoupiga vita udini na undugunaizasheni bado hii dhambi itaendelea kuwatesa watanzania masikini wasio na majina!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa Ngongo usemacho, wasafirishaji wanajua namna ya kukwepa/kupunguza uzito wa magari yao yanapoingia kwenye mizani. Fikiria gari imepita mzani wa kibaha kisha ikapita mzani wa mikese na kuonekana iko sawa lakini ilipoonekana imezidi uzito anaadhibiwa operator wa kibaha.

  Vilevile ukiangalia umbali wa kibaha hadi morogoro ni takribani kilomita 200 hapo katikati chochote chaweza kutokea. Transporter anaweza kuongeza mzigo hapo katikati.

  Lakini pia nimeshangazwa na weledi wa hawa jamaa bila kuwahoji wafanyakazi wao wanakimbilia polisi na takukuru kwa hisia potofu bila ushahidi.
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Suala la kurenew mkataba nadhani litakuwa gumu kwa mazingira yaliyopo. Sasahivi wanafanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja, na renewable subject to satisfactory performance. Kwa taarifa nilizopata wengi wamekuwa wakifukuzwa bila kumaliza japo huo mwaka mmoja, tena hawa jamaa nimeambiwa hawana muda wa kufanya hearing kwa mfanyakazi anapotuhumiwa, wananchojua ni kufukuza tu.

  Kuhusu tuhuma za rushwa kwa wafanyakazi wa mizani zimekuwepo sana lakini viongozi wa tanroads ndio wanaochangia hali hiyo. Fikiria mtu analipwa mshahara wa shilingi laki moja na thelathini na tano elfu (Tsh.135,000/-) kwa mwezi kama gross. Katika hali kama hiyo unategemea wafanyeje kama sio kuwaweka katika mazingira ya rushwa, tena rushwa yenyewe wanashawishiwa na ma transporter.

  Lakini vilevile katika hali ya kukabiliana na rushwa mizani sasahivi kumewekwa kamera (cctv cameras) kwahiyo mazingira ya rushwa yamedhibitiwa kwa kiwango kikubwa sana kama si kuisha.
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naendelea kufuatilia kuona kama kuna harufu ya undugunization au tatizo ni dini ingawa kwa hawa watatu si wa dini moja, miongoni mwao wapo wa dini zetu mbili kubwa zinazotusumbua hapa nchini.
   
 8. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Tatizo la viongozi wa taasisi za Tanzania ni kwamba wanafanya kazi za serikali kama vile kazi za chama, kiushabiki-shabiki hivi, kitendwa-tendwa hivi. Labda kwa kuwa viongozi wetu wengi wamekulia mfumo wa chama kimoja kushika hatamu!
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sub-hanallah,,,dizi zipi HIZO????
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwani wanalipwa MSHAHARA SHILING NGAPI????
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni aibu lakini ndio ukweli wenyewe, wanalipwa shilingi za kitanzania laki moja na thelathini na tano elfu kwa mwezi(Tsh.135,000/-). Ukitoa NSSF 10% ambayo ni sh.13,500 wanakwenda nyumbani na sh.121,500/-
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,834
  Trophy Points: 280
  hivi kwani hawa wafanyakazi wa mizani si wanaajiriwa na tanroads kama permanent employees? na je wao si wako chini ya sheria za utumish wa umma? kwanza naomba nipate jibu hapo kisha nitatoa mchango wangu mwanana. nimesikitishwa sana na hili.
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,834
  Trophy Points: 280
  Mwita Maranya hawa wanaajiriwa chini ya mwavuli wa mashirika ya umma ama chini ya utumish wa umma ama nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. c

  chama JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwita Maranya
  Tanroads yote sijui ni nani asiyekula rushwa; hao wametolewa chambo tu na cha ajabu zaidi hao mameja wa mizani ndio wanawaowapangia wafanyakazi wa mizani kupeleka mgao kila asubuhi; inawezekana kabisa kuna jambo jingine limeshinikiza meneja; hainiingii akilini hata kidogo; rushwa za Tanroads zinaanzia kwenye ajira mpaka kwenye kwenye kupangiwa posts.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Weighbridge operators wote (nina ushahidi kwa mikoa ya Pwani na Morogoro), wanaajiriwa kwa mikataba ya mwaka mmoja ambao unakuwa renewable subject to satisfactory Performance.
   
 16. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,834
  Trophy Points: 280
  sasa inamaana contract zao zinakuwa monitored na organ ipi ya ajira? to me waende kwenye taasisi inayoshughulika na ajira zao wafungue kesi dhidi ya mwajiri wao tena hapo watumie ushauri wa kisheria ili wawee kurecover gharama zao za usumbufu nk yaani wakomae watalipwa tu ni unyanyasaji na wasimwogope mtu.

  unajua wengi wa wafanyakazi katk taasisi za serikali wanaoafanya kama vibarua ama kwa mikataba wanateseka sana. tena huwa wanakosa tu pa kusemea ila kiukweli wanahujumiwa sana na kufukuzwa kazi pasi sababu za msing na kuonewa sana tu.
   
 17. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Tata Mwita Maranya hapa kuna mambo mengi sana yanajitokeza kwa mtazamo wangu
  • Roho Mbaya ya Meneja (Nadhani anawakilisha mabosi wengi wa kiswahili) Wa kuwatafutia sababu tu ya kuwafukuza kazi ili alete ndugu zake au watu anaowajua kwasababu kwa level yake na kama ni manager mzuri alipaswa kuwapeleka polisi akiwa na ushahidi usiokuwa na mashaka yeyote sasa kama Takukuru na Polisi wanakosa ushahidi basi ni wazi kuwa hakuwa na ushahidi wa kutosha na hapo anasahau kuwa anachezea maisha ya watu na familia/ndugu wanao mtegemea
  • Sheria kutofuata mkondo wake,Ni kesi za mauaji na treason tu ndo nadhani hazina dhamana nashangaa kuona polisi wakipokea maagizo toka kwa meneja wa Tanroads hii inaonyesha amewaweka mfukoni kwa pesa zake
  • Suala la Rushwa nchi hii ni kubwa sana haliwezi kuisha kwa kuwatoa kafara watu wachache tu tunahitaji reshuffle ya system nzima usishangae hata huyo meneja mwenyewe ni mla rushwa ila ameamua tu kuwafanyia kitu mbali hao jamaa
  • Itoa picha ya unyanyasaji mkubwa uliwepo kwenye ajira hasa serikalini hii ni kwasababu hatuna sytem nzuri za kukata rufaa
  • Nadhani hao jamaa wanapaswa kujipanga sasa kutafuta kazi nyingine cause ni obvious mikataba yao ikiisha hatapewa mikataba mingine
  • It's good kupiga kelele kwenye forums kama hizi kama ulivyofanya mkuu Maranya hii itasaidia walau kidogo kwa huyo meneja kujipima upya kwasababu nina uhakika kama sio yeye basi mabosi wake watapita tu humu kusoma ila suluhisho kubwa ni kufanya reshuffle ya hii nchi na kuondoa uozo mwingi ulio katika sekta mbalimbali

  Nawasilisha
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa kwa wafanyakazi wengi wa Tanzania hawajui kupigania haki zao, mtu anafukuzwa kazi kienyeji tu bila utaratibu lakini naye anaridhika.
  Lakini pia kuna udhaifu mkubwa katika ajira hizi za contracts ambazo mameneja wa tanroads wa mikoa ndio wenye final say kwenye ajira zao. Binafsi sioni sababu ya msingi ya kutowapa permanent contracts kama wanavyofanya kwa wafanyakazi wengine wa mizani. Kwanini weighbridge operators tu ndio waajiriwe kwa contracts?
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tata Sabayi nimekubaliana kabisa na hoja zako murua kabisa. Tuendelee tu kuyasema haya bila kificho ili hatimaye watanzania wenzetu waweze kujifunza kusimamia na kupigania haki zao.
  Kwa upande wa pili ni muhimuy sana kwa hawa watanzania wenzetu wanaokabidhiwa dhamana ya kuongoza taasisi zetu za umma waonyeshe weledi, vinginevyo serikali yetu pamoja na taasisi zake wanashindwa kuleta tija kwa nchi kama ilivyokusudiwa.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii mifumo inayochochea rushwa ndiyo tunatakiwa kupambana nayo ili tuikomeshe na kuleta tija na uwajibikaji katika serikali yetu.
  Nimeambiwa pale mizani ya kibaha kuna kamera za cctv zinzorekodi matukio yote, magari yanayopita pamoja na watu wanaovyofanya kazi ofisini. Kama kuna tuhuma za rushwa kwanini wasitumie ushahidi wa picha za cctv kubainisha ukweli? hapa lazima kuna mchezo mchafu wanachezewa hawa vijana.
   
Loading...