Uongozi wa rais jakaya kikwete na nadharia za ndege watatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa rais jakaya kikwete na nadharia za ndege watatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAKOLE, Aug 19, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kuna kisa maarufu cha ndege watatu ambacho kinafafanua aina sahihi ya Uongozi wa Raisi wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndege hao ni Bata, Kuku na Hondohondo.


  Ndege hawa wana sifa zinazowatofautisha kwa namna wanavyowalea vifaranga wao. Kwa uongozi wa JK, Vifaranga hapa nitawafananisha na wananchi na Ndege (Mzazi) nitamfananisha na Kiongozi wetu.


  Kuku;
  Katika kuilea familia yake huwa na kawaida ya kutangulia mbele kasha vifaranga wake hufuata kwa nyuma huku mama yao akiwaongoza pahala pa kuelekea. Katika uhalisia, kiongozi wetu anapaswa awe mbele nasi wananchi tumfuate kwa maana yeye ndiye ajuaye wapi tunaelekea. Sidhani kama kiongozi wan chi yetu anaangukia katika kundi hili.


  Bata;
  ndege huyu anayo kawaida ya kubaki nyuma wakati vifaranga wake wakitangulia. Hii inamaanisha kuwa mama bata huelekea kule watoto wake wanapoelekea. Katika hali halisi wananchi tungekuwa tunamwongoza raisi wetu kule ambako sisi tunataka kwenda. Hapa pia ninayo mashaka kama ndivyo ambavyo raisi wetu anatuongoza.


  Hondohondo;
  Ndege huyu wakati akitembea na vifaranga wake, yeye huwa katikati na vifaranga humzunguka. Katika uhalisia huu ni uongozi shirikishi. Kila kifaranga pamoja na mama yao anayo nafasi ya kuongoza msafara. Hapa wananchi kama vifaranga sanjari na kiongozi wao wanayo nafasi sawa katika uongozi. Nadharia hii pia nna mashaka nayo kama ndiyo inayofuatwa na raisi wangu hapa kwetu.


  Ipo mifano ya matukio ambayo natilia mashaka staili ya Uongozi wa raisi wangu. Matukio hayo ni kama yafuatayo:


  Wakati Fulani kulitokea mgogoro kati ya serikali na Walimu,
  Raisi wetu aliingilia kati na kuwakaripia walimu na hata kudiriki kuwaita Mbayuwayu. Hii ilikuwa ni katika awamu ya kwanza ya uongozi kama sijakosea. Alichofanya raisi ni kuwaita Wazee wa Dar es Salaam kuongea nao kuhusu kadhia hii, wazee ambao sidhani kama uhusika wao katika kadhia yenyewe ni mkubwa kiasi hicho. Wananchi walitegemea Rais awaite walimu wenyewe ili atoe karipio lile.


  Mabadiliko ya katiba;
  wakati Waziri mhusika wa Katiba Celina Kombani pamoja na Mwanasheria mkuu wakati Fulani walipinga kabisa uwezekano wa kuibadili katiba ya Tanzania kwa kuuhadaa umma kuwa ni gharama kubwa na ikizingatiwa kuwa katiba iliyopo madarakani haina mapungufu; Raisi alikuja na msimamo ambao ndio yalikuwa ni matarajio ya wananchi kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba.


  Vijana na Ajira; Edward Lowasa alipiga kelele wakati Fulani kuhusu kundi kubwa la vijana kukosa ajira na kutangaza kuwa ni bomu, Waziri anayehusika na Kazi na ajira alikuja juu katika hotuba yake akisema kuwa huo ni uzushi kwani ajira zipo na vijana wanaajiriwa. Kauli hii ilipingwa na hata vijana wenyewe. Siku chache baadae Raisi anakuja na hotuba iliyounga mkono kauli ya Lowasa kuwa suala la ajira nchini ni “time bomb” akipingana na mmoja wa viongozi aliowateua.

  Kadhia ya Malawi;
  Bernad Membe, Waziri wa mambo ya nje, katika Hotuba yake bungeni hivi karibuni aliongea kwa hasira na mkazo hata wananchi wakajua kuwa sasa nchi inaingia vitani na Malawi kuhusiana na mgogoro wa mpaka. Maoni mbalimbali yalitolewa. Wananchi tulisubiri tamko la rais wetu lakini hatimaye Raisi amehakikisha kuwa Tanzania kamwe, haitaingia vitani na Malawi.


  Swali ambalo huwa najiuliza bila ya kupata majibu ni kuwa kati ya nadharia za ndege watatu, raisi Jakaya Kikwete nimuweke kwenye nadharia ya ndege yupi?
   
 2. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Nadharia ya BUNDI ikoje!?? inaweza ikafaa zaidi
   
 3. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Dah, hiyo sijaipata. Ngoja niipekue ianweza ikamfaa ki ukweli
   
Loading...