Uongozi wa Magufuli utakuwa mbaya sana, ashauriwe haraka

Dj-kobo

JF-Expert Member
May 5, 2013
458
193
Wakuu Wasalaam Kwenu

Leo tuangazie taratibu za uongozi kwanza kwa haraka. Utumishi wa Umma una taratibu zake zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria na sio mtu kuamka na kufanya anavotaka.

Ni ukweli usiopingika kuwa Raisi Magufuli alianza vizuri sana lakini hakuendelea vizuri baada ya sasa kuacha kutekeleza sera za uongozi na kuingia yeye na serikali yake kufanya kazi kwa kuwatisha waandamizi au wasaidizi wa utumishi katika nchi hii na wapo waliosimamishwa na wengine kutimuliwa ambapo hapo baadae uchunguzi ukifanyika wengine watakua hawana hatia kabisa na hivyo watalipwa fidia kubwa.
 
Namuomba na Namshauri ili afanikiwe atumie mbinu ya Spiral Spring System of Leadership hii itamsaidia hasa kama ataweza kuleta katiba mpya ile iliyoasisiwa na warioba akiwa bado hajapigwa na kuvurugwa pale Hotelini siku ya mdahalo
 
Tutamshauri wale wote aliowatumbua kwa kupitisha containers bila kulipia kodi warudishiwe nafasi zao ili aonekani kiongozi mzuri.tutamshauri amrudishe hossea kazini ili aonekani hakandamizi
 
Shamba la bibi sasa linalindwa na kikosi cha makomandoo wakiwa na zana nzito za kijeshi yaani ukigusa hata jani tu unapigwa bomu.
 
Namuomba na Namshauri ili afanikiwe atumie mbinu ya Spiral Spring System of Leadership hii itamsaidia hasa kama ataweza kuleta katiba mpya ile iliyoasisiwa na warioba akiwa bado hajapigwa na kuvurugwa pale Hotelini siku ya mdahalo

Kamshauri mkeo kwanza kisha ndiyo uje hapa
 
nahsi na we ni jipu liko kazini. Mkisikia tingatinga tu yanaanza kuwasha. Ni bora tupate hasara Ya kuwalipa kuliko kuendeleza hasara wanayotusababishia kwa ulafi na uhujumu. Hasara itakuwa yetu sote kama watanzania kwani tumepima na kumpa go ahead kuyatumbua kwa mkono wa chuma. Majipu yote subirini ama yaanze kujikamua taratibu kabla Ya tingatinga letu kujaza mafuta. Wenye mtazamo wako ni mmoja Kati ya milioni moja Ya watanzania
 
Katika yote aliyo fanya wapi amekosea? ulitaka aendelee kuwa vumilia wapitisha makontena bila kulipa kodi au kodi ikilipwa inaingia kwenye mifuko yao? au ulitakata watu wanao jenga mabondeni waendelee ? ulitaka aweke mawaziri walewale wezi wa miaka yote? mtu anajua wizi unao endelea pale bandarini halafu kwa macho makavu anamdanganya waziri mkuu huku ukweli anaujua ulitaka asifukuzwe kazi?

Kuwa objective katika wote walio fukuzwa nani unadhani hakustahili? unaambiwa usiende Nchi za nje unaamua kukaidi amri halali ya Rais halafu uachwe tu??
 
:like1:
 
Sasa apange bei za petrol.disel na umeme vishuke kabisa tuione tz ya nyerere
 
Wakuu Wasalaam Kwenu

Leo tuangazie taratibu za uongozi kwanza kwa haraka. Utumishi wa Umma una taratibu zake zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria na sio mtu kuamka na kufanya anavotaka.

Ni ukweli usiopingika kuwa Raisi Magufuli alianza vizuri sana lakini hakuendelea vizuri baada ya sasa kuacha kutekeleza sera za uongozi na kuingia yeye na serikali yake kufanya kazi kwa kuwatisha waandamizi au wasaidizi wa utumishi katika nchi hii na wapo waliosimamishwa na wengine kutimuliwa ambapo hapo baadae uchunguzi ukifanyika wengine watakua hawana hatia kabisa na hivyo watalipwa fidia kubwa.

hii nayo ni thread? Acheni kuandika kwa mikumbo
 
Back
Top Bottom