Uongozi wa hospitali ya rufaa Mbeya waomba msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa hospitali ya rufaa Mbeya waomba msaada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jackbauer, Jul 3, 2012.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  [h=6]UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, imeomba serikali kuwapatia haraka iwezekanavyo madaktari wengine kuja kuziba nafasi zilizoachwa na madaktari 72 waliotimuliwa hivi karibuni.

  Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Eliuter Samky alitoa ombi hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliyefika hospitalini hapo kuangalia hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

  Dk. Samky alisema kuondoka kwa madaktari hao kumesababisha huduma katika kitengo cha upasuaji kubakiwa na madaktari bingwa wanne akiwemo na yeye wakati kitengo cha macho hakina daktari kabisa.

  “Kwa kweli hali ya utoaji huduma imekuwa ngumu sana kwani tuna madaktari 39 tu hospitali nzima na Hospitali ya Wazazi ya Meta ina madaktari wawili tu waliobaki. Kwa kweli tunahitaji nguvu ya madaktari wengine kuja kutusaidia,” alisema Dk. Samky.

  Akijibu maombi hayo Kandoro alisema kuwa wanafanya utararibu wa kupata madaktari wa upasuaji kutoka katika hospitali za wilaya za Kyela, Mbozi na Rungwe ili kuwapeleka Rufaa kusaidia kukidhi mahitaji ya wagonjwa.

  Pia aliwaomba wakazi wa Mkoa wa Mbeya kufuata utaratibu wa kitabibu wa rufani ili kupungunza msongamano mkubwa unaoweza kujitokeza katika hospitali za Rufaa na Mkoa kwa kutibiwa katika Vituo vya Afya badala ya kukimbilia hospitali kubwa.-


  Tanzania Daima
  [/h]
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Waambie tayari wako njiani, leo watafika huko.
   
 3. D

  Dr Gustav Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi kwelikweli
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  JK bwana
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huo ndio ujinga serikali ilivyotimua ilitegemea nini?Hapa liwalo na liwe tu.
   
 6. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,278
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  duh!...muhimbili nako hali ni mbaya kuliko hata jana
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  madaktari wa kiajemi wameshafika?
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Wasubiri wataletewa tu.. serikali dhaifu iko kwenye mchakato wa kutafuta madaktari toka nje
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  sijui kandoro anamdanganya nani.sasa huko wilayani itakuaje?
   
 10. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uwezo wao wa kufikiri ndo umeishia hapo mkuu!
   
 11. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Itabidi waajiri na wakalimani, maana hapo lugha gongana!
   
 12. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo ni kweli alivyosema member mmoja kuwa wewe ni mkurugenzi wa mawasiliano pale magogoni?
   
 13. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Wanatoka IRAN angoje kidogo
   
 14. Electron

  Electron Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, halafu bado anasisitiza wafuate utaratibu wa rufaa (rufani), yaani waanzie dispensary, health centre, DISTRICT HOSP, then mbeya rufaa..... ok ameshawatoa Drs wilayani.... nini kitafanyika huko?
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  nawashangaa sana watanzania wanaoshabikia mgomo.
   
 16. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  wengine wanafikiri kabla ya kusema na wasiwasi Rais husema ndiyo huanza kufikiri kwa kina
   
 17. h

  hans79 JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Nendeni na Rungwe nako geti la ushuru wa mazao limekwisha, na bado hadi upuuzi uwatoke.
   
 18. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  Hawa 39 walio baki ni wasaliti wakubwa pumbavu zao wana lialia nini sasa wao si wamejifanya nio marobot wanapiga kazi!
  Wapige kazi sasa wasaliti wakubwa nyie kwani madaktari
  walio fukuzwa si walikua wana dai maslahi ya wote sasa iweje nyie mnajifanya hayawahusu???
  Nyambav!!!!!!!
   
 19. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama imefikia hivyo, ujue kuwa TBC hawawezi kufika huko.
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mgomo wa madaktari hauna tija kwa taifa hasa kwa wananchi maskini.
   
Loading...