TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Huu ni mtazamo wangu tu
Baada ya Rais John Pombe Magufuli kuingia Madarakani, Kada wa ACT- WAZALENDO. Prof. KITILA MKUMBO aliwahi kusema, nanukuu: ''WAPINZANI WAKITEGEMEA KUPATA UMAARUFU KWA KUANGALIA MADHAIFU YA CCM, WANAWEZA KUJIKUTA KATIKA KIPINDI KIGUMU' mwisho wa kunukuu. Maneno haya ya Prof. Kitila Mkumbo yalikuja baada kuona mtu ambaye ameshinda urais baada ya uchaguzi uliopita, rais John Pombe Magufuli.
Kasi aliyoanza nayo iliwashtua Wapinzani ambao kile ambacho Rais alianza kupambana nacho(UFISADI) ndiyo uliokuwa wimbo wao wa siku nyingi kuwa walikuwa wanapambana nao. Huku wakisahau kuwa wanaye mtu(LOWASSA) ambaye walifanya kazi nzuri sana kuwafahamisha watanzania kuwa hakuwa mtu mzuri hata kidogo katika dhana nzima ya UADILIFU katika rasilimali za nchi WAKABWATUKA kuwa Rais anatekeleza sera za vyama vyao na kwamba waliokuwa wanatumbuliwa walikuwa wana CCM na kwamba, CCM ndiyo waliyokuwa wakiisoma namba.
Kadri siku zivyokwenda wakajikuta kwa namna moja au nyingine ndugu zao na hata rafiki zao wa karibu nao wanatumbuliwa. kule kubwatuka kuwa rais alikuwa akitekeleza sera za vyama vyao kukayeyuka tukaanza kusikia maneno mara oh, ni NGUVU ZA SODA, mara oh WAFANYABIASHARA WALIOSAIDIA UPINZANI WANAONEWA. Hili la JUZI ndilo kali eti "WATUMISHI WANAFUKUZWA BILA KUPEWA NAFASI YA KUJITETEA" Katika operation tumbua majipu, si ni CCM ndiyo wanaisoma namba? Tangu lini MBOWE akawa na huruma kwa wana CCM wanaoisoma namba kutoka kwa rais anayetokana na CCM?. Juzi wakati Rais akiwahutubia wananchi wa Arusha mbele ya Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, akalitumbua jipu moja kwa maneno kuwa linalalamika wafanayakazi kufukuzwa kwa sababu na lenyewe lilikuwa linufaika na hujuma zilizokuwa zikifanywa na majipu hayo.
Baada ya kuona rais yupo kikazi zaidi na siyo kisiasa, wanataka kumuingiza rais kwenye siasa za maji taka. Rais wa awamu ya tano yuko kwa ajili ya matatizo ya Watanzania. siyo kazi yake kuzilazimisha mamlaka zinazohusika na chaguzi za Zanzibar na mameya kuamua ambavyo kundi fulani la kisiasa linataka iwe wakati kuna sheria na taratibu zinazoongoza chaguzi hizo.
Kama wapinzani wataendelea na mtazamo wa kutaka kutafuta madhaifu ya raia Dr. John Pombe Magufuli huko kwenye chaguzi za kisiasa, hakika nakuona kutetereka kwao siku siyo nyingi. Watanzania kwa muda mrefu sana tulimhitaji rais wa namna hii na yeyote atakayethubutu kumpotezea muda wa kuwatumikia watanzania wanyonge kwa kumuingiza kwenye mambo ya kisiasa wakati wapo watu wa chini yake tena chini sana wa kuyashughulikia, hakika tutampiga mawe huku mitaani. Watanzania wana hamu kubwa sana kuona juhudi za rais za kupambana na ufisadi, zinazaa matunda katika siku za usoni kwa kuongeza thamani ya sarafu yetu, kudhibiti mfumuko wa bei, nafuu ya huduma za jamii kama vyakula, afya, nishati, vifaa vya ujenzi n,k. Watanzania hawana hamu ya kutaka kujua Meya wa Dar es Salaam ametoka CCM, CHADEMA, CUF au ACT-WAZALENDO.
Nawaasa wapinzania wajikite kwenye mambo yenye maslahi kwa mtanzania wa chini ili kumsaidia rais kuipeleka Tanzania hatu moja mbele. kufanya hivyo Watanzania wataona maana nzima ya uwepo wa upinzani. Upinzani wa kweli ni ule utakaoshikamana na yeyote yule kuwaletea wananchi maendeleo na siyo upinzani wa kuamini kuwa wenyewe ndiyo unaweza kuwaletea wananchi maendeleo na kuona wivu pale ambapo mwenye itikadi tofauti na yao akitekeleza kile ambacho wananchi wanakihitahi na hivyo kuhofia kutoweza. Mwananchi hahitahi kuona upinzani unadumu milele hata kama hauna unachokifanya.