Uongozi wa DAWASCO umeshindwa kufanya kazi ipasavyo na kusababisha wakasi wa jiji la Dar Es Salaam kunywa maji machafu

BVR 2015

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
227
410
Wakazi wa Dar es salaam kwa siku mbili mfululizo tunachota maji yaliyo na vumbi katika mabomba ya Dawasco.tunaomba uongozi wa Dawasco iwajibike kwa uzembe wa kushindwa kuyatibu haya maji,wananchi tuna wasiwasi na haya maji yanaweza kuwa na wadudu waenezao magonjwa

16175242031222883850304289948969.jpg
 
Haya maji mpaka tumeshayazoea.
Unataka kuniambia kwamba DAWASCO wamewahi toa maji tofauti na haya?
 
Siku hizi wanaitwa Dawasa.

Hawa jamaa wamekuwa sugu sana kwa wananchi.

Halafu hawanaga lugha Nzuri kwa wateja.

Ni wajeuri kuanzia maboss wao.

Mimi huwa nawashangaa sana au elimu zao wameungaunga?

Kwanini hawaeleweki?!

Hawana customer care kuanzia managers.

Yani wanaona kama kutoa huduma ya maji ni hisani kwa wananchi wakati ni haki yao.
 
Wakazi wa Dar es salaam kwa siku mbili mfululizo tunachota maji yaliyo na vumbi katika mabomba ya Dawasco.tunaomba uongozi wa Dawasco iwajibike kwa uzembe wa kushindwa kuyatibu haya maji,wananchi tuna wasiwasi na haya maji yanaweza kuwa na wadudu waenezao magonjwa

View attachment 1742892
Hii hali hata huku Chato kwa sasa maji ni kama haya na ni zaidi ya haya
 
Back
Top Bottom