Uongozi wa chuo kikuu na maamuzi ya kijinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa chuo kikuu na maamuzi ya kijinga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtz-halisi, Jan 11, 2012.

 1. Mtz-halisi

  Mtz-halisi Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nikiwa mfanyakazi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam nimesikitishwa sana na maamuzi ya kijinga yanayofanywa na wahesimiwa wetu. tarehe 8/1/2012 nimesoma andiko la vitisho kwa wanafunzi na viongozi wa DARUSO juu ya maamuzi ya mgomo wao kuwadai wanafunzi wenzao waliofukuzwa tena walifukuzwa wakati wakidai haki. andiko lilikuwa la kuwatisha wabunge wa DARUSO pamoja na cabinet nzima kuwa atakayejaribu kugoma atafukuzwa.
  Kitu kibaya zaidi nimeona hii nchi inaongozwa kama haina mwenyewe, unapo ona viongozi wakubwa kama Prof. Mkandara, Prof Mgaya na Maboko wakiamini wanafunzi hawawezi kudai haki wenyewe na wakionekana wanadai haki wanaamini kuna mkono wa wanasiasa hapo pana tatizo. mpaka sasa kichwani mwao wana amini kuna mkono wa CHADEMA. kweli hii ni aibu kubwa sana

  Naomba watu ambao ni wanaharakati tuungane kuwasaidia vijana hawa, naomba UDASA, THTU na RAAW chuo kikuu musimame na vijana hawa, tusiwaachie hawa watu wachache wawacheze vijana wetu.

  Umoja wa vijana CHADEMA,CCM,CUF etc ni muda wa kusimama na vijana wenzenu sasa msisubili mpaka mambo yahalibike.

  kwa hali ninayoiona ni hatari
   
 2. sidimettb

  sidimettb Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu haitaki watu wenye uwezo wa kuchambua mambo na kufikia maamuzi,iko tayari kutimua cream yote wabaki wale ma YES MAN!.

  Ni aibu kwa taasisi kubwa kama hii ya taaluma kuendeshwa kisiasa,tena siasa za udikteta wa chama kimoja.Wapenda haki na maaendeleo popote pale walipo ni lazima kuunganisha nguvu dhidi ya ujuha huu wa Management ya UDSM+Serikali ya CCM!
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kama tunahitaji kusonga mbele basi hatuna budi kutenganisha siasa na sehemu nyeti za taifa kama Vyuo vikuu na mahospitali. Tunahitaji kutengana kabisa na haya mambo ya kijinga.

  Sawa siasa zinagusa kila sehemu, lakini hebu watu sasa waumize vichwa namna ya kuwafanya watu waache kupractice siasa ndani ya hizi sehemu, watu wawe busy kutafuta solution ya matatizo kwenye jamii. Na hili la kila mtu kuwa mteule wa rais linaboa sana, Walipa kodi nao bila kufuatilia fedha zao zinaendaje nalo linaboa sana. We need to make things clear, ili kuziba myanya ya wizi. Hawa vijana wanasomeshwa kwa kodi zetu, wanapofukuzwa maana yake walipa kodi wanakula hasara.
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Yaani ajk aamegeuka mkuu wa UDSM;Mukandara kabaki kutii amri tu toka magogoni!!!
   
 5. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  That is what we call EDUCATED BARBARIANS. Mfano mtu huko darasani unafundishwa jinsi yakubadiri jamii kutoka kwenye uduni kwenda kwenye maendeleo na unaambiwa kuwa mojawapo ya njia sahii ni kudai haki na kutetea wanyonge dhidi ya unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na tabaka tawala.
  Je kwani unavyo weka kwe vitendo kitu unachofundishwa unaonekana kuwa adui?Jamii unayokusudia kuiokoa haikuungi mkono?
  Hapa bila shaka kuna tatizo kubwa ambalo linaweza kutatuliwa kama kuna wenye nia njema na jamii hiyo.UDSM kwa sasa itaonekana mbaya zaidi kuliko vyuo vingine maana mkuu yuku tayari kuiharibu UDSM na kuimarisha UDOM hili historia imtambue kwa visasi vyake. The UDSM ifutike kabisa kwenye ramani ya taaluma.
   
 6. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbuka Proff Mukandara ni mshauri wa rais ktk mambo ya siasa mkuu!napita tu mkuu!
   
 7. babad

  babad Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa aina hii ya maamuzi yasiyoangalia mbele tutaishia kuwa na wasomi waoga wasiojua hata haki zao na namna ya kuzipata.Kama chuo kimewashinda wawaachie wenye busara zaidi wakiongoze
   
 8. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama kuna mtu kanichosha mlimani ni Mukandara, yeye kaamua kuonyesha u-ccm wake badala ya taaluma yake.. aibu sana hii, halafu jingine ni kufukuza wanafunzi na kuhakikisha hawaruhusiwi kujiunga na chuo chochote Tanzania!
   
Loading...