The Spirit of Tanzania
JF-Expert Member
- Mar 7, 2020
- 537
- 928
Nina vijana wangu wamepata nafasi chuo cha afya tanga moja kwa moja kutoka kidato cha nne.
Katika mambo yalilonishangaza ni kama ifuatavyo:
1. Suala la chakula mwanafunzi anatakiwa kujitegemea ila kwenye form ya kujiunga hawajaandika kabisa habari hii.
2. Chuo kutoza fedha ya kujiunga NACTE baada ya kuwa mwanafunzi amefika chuoni hali amechaguliwa moja kwa moja na wizara
3. Baadhi ya walimu hawafundishi kwa kufata vipindi, sasa inafika wakati wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanafundishwa kuanzia asubuhi saa 12 hadi saa 2 usiku, hivi hapa mnaandaa wataalamu wa afya kweli au mnataka kuonekana mmefundisha?
4. Bima ya afya kutotolewa kwa wanafunzi kwa wakati, inafikia muda mwanafunzi anaumwa anatumia gharama zake kujitibu hali amelipia bima ya afya.
5. Form ya kujiunga haiko wazi na ni kama kuna gharama zisizo za lazima, ile form ya kujiunga chuo hiki ni scanned copy, halafu imewekwa kwenye mtandao, mtu wa IT chuo hiki hayuko makini kabisa, pia kuna fedha imeandikwa fedha ya michezo, hivi kweli mnaibia watanzania waziwazi kwa kuita fedha ya michezo? Kama mwanangu hachezi mchezo wowote kutokana na afya yake kwanini nilipie?
TAFADHALI, UONGOZI WA CHUO HIKI ANGALIENI, WAZAZI WENGI TUMEUMIA MWAKA HUU KWA UBOVU WA MUUNDO WENU.