Uongozi wa CHADEMA Taifa unaisha muda wake siku ya Ijmaa tarehe 14.09. 2019

M

Morgan Freeman

Member
Joined
Mar 14, 2015
Messages
65
Points
95
M

Morgan Freeman

Member
Joined Mar 14, 2015
65 95
Tumia jicho la tatu kufikiri hilo suala ya kwamba gharama ya kuifuta chadema ni kubwa kuliko kuiacha
Coz kuifuta ni kutengeneza mazingira ya kuwapeleka wote ACT jambo ambalo litakua na impact mbaya bara na visiwani na kuiacha hai ni least coz kazi rahisi ni kuwafitinisha na ACT unawaacha watoane macho nyie mnapeta tu
So Hata iweje kwa sasa msajiri hawezi bet hii kamati
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,699
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,699 2,000
Taarifa nilizodokezwa kutoka ndani ya CHADEMA ni kwamba uongozi wa chama hicho Taifa unaisha muda wake siku ya ijmaa tarehe 14.09. 2019 na kama hawajafanya uchaguzi msajili wa vyama siasa Nchini atalazimika kukifuta chama hicho au kukitaka kisitishe shughuli za kisiasa Nchini.

Hata hivyo viongozi wake akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe na Dr Mashinji wapo kimya na hakuna dalili zozote za kuitisha uchaguzi hivi karibuni jambo litakalohalalisha kufutiwa usajili.
My Take: Yale Yale ya kupuuza katiba ya Nchi.
Ndugu Chadema inaongozwa kwakufuata katiba ya chama hicho na miongozo yake, sio matamanio ya mtu au kikundi cha watu,

Soma katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.3 (a).....

Ukimaliza hapo, pia Kasome Katiba ibara ya 7.3.3

Mamlaka ya kupanga tarehe ya uchaguzi Ndani ya chama inapangwa na nani. ....

Then urudi hapa ukiwa na hoja sio matamanio yako
 
S

shinyangakwetu

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2015
Messages
1,560
Points
2,000
S

shinyangakwetu

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2015
1,560 2,000
Hivi wewe hapa unatetea nini?

Hiyo democrasia mnayolilia kila siku kwa nini msianze kui apply hapo chadema kwanza?

Hata kama huyo mbowe mnampenda vipi kwanini msiwe mnamchagua pindi uchaguzi ukifika?

Hivi chadema watapata akili lini? Kwanini mnawapa ccm sababu ya kuwagonga kila iitwapo leo?
Mbona ninyi mnataka mpoteze watu kisa miaka kumi eti akichaguliwa term ya kwanza kusiwe na wa kumpinga term inayofuata demokrasi ipo?
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
18,220
Points
2,000
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
18,220 2,000
Afrika kuwa na mfumo wa vyama vingi ni bado kabisa, inahitaji miaka 100 ijayo
Chadema wanahubiri kuheshimu katiba na demokrasia kwa wengine ikifika ndani ya chama Chao kuheshimu katiba ya chama Chao na demokrasia ndani ya chama chao wanaingia mitini.
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
18,220
Points
2,000
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
18,220 2,000
Ndugu Chadema inaongozwa kwakufuata katiba ya chama hicho na miongozo yake, sio matamanio ya mtu au kikundi cha watu,

Soma katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.3 (a).....

Ukimaliza hapo, pia Kasome Katiba ibara ya 7.3.3

Mamlaka ya kupanga tarehe ya uchaguzi Ndani ya chama inapangwa na nani. ....

Then urudi hapa ukiwa na hoja sio matamanio yako
Hivyo vifungu ukomo ukifika ndio vinaanza kufanya Kazi au? Mfano uongozi mwisho tarehe 14 Mwezi wa Tisa kwa hiyo katiba ndivyo inavyowataka kuwa Hadi ifikie mwisho kabisa ndio watamke uchaguzi upo au la? Hawawezi tamka wiki mbili kabla au Mwezi mmoja kabla ya tarehe ya mwisho kufikiwa?
 
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Messages
12,790
Points
2,000
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2016
12,790 2,000
Watashinda lakini hawatashinda.

Unaweza kuvuta vyama vya siasa, lakini kamwe huwezi futa fikra za kutaka mabadiliko.
Kada Mbowe na Lissu wanatengeneza makosa ya kiufundi kuua Chadema.
 
A

Akili 7

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2019
Messages
242
Points
500
A

Akili 7

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2019
242 500
Taarifa nilizodokezwa kutoka ndani ya CHADEMA ni kwamba uongozi wa chama hicho Taifa unaisha muda wake siku ya ijmaa tarehe 14.09. 2019 na kama hawajafanya uchaguzi msajili wa vyama siasa Nchini atalazimika kukifuta chama hicho au kukitaka kisitishe shughuli za kisiasa Nchini.

Hata hivyo viongozi wake akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe na Dr Mashinji wapo kimya na hakuna dalili zozote za kuitisha uchaguzi hivi karibuni jambo litakalohalalisha kufutiwa usajili.
My Take: Yale Yale ya kupuuza katiba ya Nchi.
Kama mwenyekiti wa ccm anavyopuuza katiba ya nchi
 
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Messages
12,790
Points
2,000
W

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2016
12,790 2,000
Ndugu Chadema inaongozwa kwakufuata katiba ya chama hicho na miongozo yake, sio matamanio ya mtu au kikundi cha watu,

Soma katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.3 (a).....

Ukimaliza hapo, pia Kasome Katiba ibara ya 7.3.3

Mamlaka ya kupanga tarehe ya uchaguzi Ndani ya chama inapangwa na nani. ....

Then urudi hapa ukiwa na hoja sio matamanio yako
Kamanda makada Mbowe na Lissu watahakikisha wanaichinja Chadema ndio mtaamka
 
T

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Messages
1,780
Points
2,000
T

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2019
1,780 2,000
Makamanda hivi kwa nn msifanye uchaguzi wa mwenyekiti? Tatizo nn?
Naunga mkono hoja! Chadema kama chama kikuu cha upinzani na chama kinachoamini kwenye Demokrasia na Maendeleo, hawana budi kuwa mfano wa kuigwa!

Muda wa Mwenyekiti wa sasa kimsingi ulitakiwa kufikia kikomo mwaka 2014, kwa kuongoza mihula miwili! lakini katika hali ya kushangaza aliongezewa muhula mwingine.

Kwa sasa hakuna namna, unatakiwa ufanyike uchaguzi wa ndani na mwenyekiti wa sasa awaachie vijana wa kumhenyesha Magufuli na pia kwa ajili ya kurudisha mvuto kwa hili kundi la vijana ambalo ni muhimu sana kwenye ujenzi wa chama.

Iwapo mh.Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti, mtawapa ccm kiburi cha kuanzisha mchakato wa Rais wa sasa kutawala maisha! Maana chama kitakosa nguvu ya kukemea hali hiyo kama kilivyoshindwa kwenye hoja ya ufisadi baada tu ya kumpokea mh. Lowassa kuwa mgombea urais mwaka 2015 na wakati hapo awali walimtuhumu kama mmoja wa mafisadi nchini.

Katibu Mkuu amepwaya sana, na ni ukweli uliowazi ameshindwa kuvaa viatu vya Dr. Slaa! Mwenyekiti mpya aje na timu yake. Mbinu za mapambano zinatakiwa zibadilishwe! Mbinu ya kuvaa magwanda kupambana na ufisadi, kwa awamu hii siyo rafiki. Jk alikuwa ni mwanasiasa aliyekomaa kuliko huyu tuliye naye hivyo ni lazima uongozi mpya ubadilishe.

Ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya chama na pia ofisi za mikoani na wilayani, ili kupunguza kejeli kutoka kwa wapinzani wenu ccm!

Chama kianzishe vyombo vyake vya habari mfano magazeti na kituo cha luninga ili kutangaza taarifa zenu muhimu maana awamu hii karibia vyombo vyote vya habari vimegeuzwa kuwa mali ya mtu mmoja na chama chake. Ni mwendo wa kusifia tu huku chadema wakionekana kwenye matukio hasi tu kama yale ya kusikilizwa kwa kesi zao za uchochezi, nk.

Ikibidi Mwenyekiti awamu hii atoke ukanda mwingine kabisa ili tu kuwaziba midomo wapinzani wenu wanaomini kwamba, chama kimeshikiliwa na watu wa kaskazini tu! na hivyo ni chama cha kikanda.

Chadema ni chama kikuu chenye ushawishi mwingi kwenye jamii hivyo hakina budi kupambana mwanzo mwisho. Kikifanya utani, kitarudi nyuma kwa hatua nyingi na hivyo kuwakatisha tamaa wapenda mabadiliko. Tafadhali, makamanda msije mkanishambulia kwa matusi, tujenge tu hoja.
 
P

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
10,571
Points
2,000
P

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
10,571 2,000
Watashinda lakini hawatashinda.

Unaweza kuvuta vyama vya siasa, lakini kamwe huwezi futa fikra za kutaka mabadiliko.
Tatizo jingine ni hili lililo katika hoja yako, ubishi na ukaidi halafu maamuzi yakitolewa dhidi yenu mnatafuta huruma ya watu.

Yale yale ya Lissu kiburi kimemjaa mpaka anashindwa hata kutuma ujumbe wa sms kwa spika.
 
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
21,485
Points
2,000
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
21,485 2,000
Tatizo jingine ni hili lililo katika hoja yako, ubishi na ukaidi halafu maamuzi yakitolewa dhidi yenu mnatafuta huruma ya watu.

Yale yale ya Lissu kiburi kimemjaa mpaka anashindwa hata kutuma ujumbe wa sms kwa spika.
Chadema ni fungu la kukosa,wafuasi ni bendera fuata upepo
 
P

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
10,571
Points
2,000
P

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
10,571 2,000
Chadema ni fungu la kukosa,wafuasi ni bendera fuata upepo
Lengo la Mzee Mtei mwaka wakati anaanzisha chama halifanani na uhalisia wa sasa hivi, Marehemu Mwalimu Nyerere alizisoma sera za CHADEMA na akazikubali, tatizo limekuja baadae baada ya kaka wa Hai kukigeuza chama kuwa kama ni taasisi yake binafsi.
 
A

amigod

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2018
Messages
317
Points
250
A

amigod

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2018
317 250
Itakuwa nzuri kikifutwa tunahitaji kuunda chama kimoja tuondoe huu utitili wa vyama ccm itatushinda tena na tena kwanini hatufikirii kuunda chama cha kuitoa ccm madarakani kila mtu ana kachama kake kupambana na ccm ni ngumu tuvunje tuvyama tote tuunde chama kimoja kiing"oe ccm
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
453
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
453 500
Mbowe aendelee kua mwenyekiti wachama ila aitishe uchaguzi fasta.
 
suramlamu

suramlamu

Member
Joined
Sep 9, 2019
Messages
10
Points
45
suramlamu

suramlamu

Member
Joined Sep 9, 2019
10 45
Kwa hapa Tanzania hakuna chama chenye demokrasia kamwe...
hakika mkuu Siku zote tumaini langu ilikua chadema ila baada ya kubadili gia angani nikaona wote matapeli bora niwe nacheki movie za Korea kuliko upinzani feki huu
 
Forum statistics

Threads 1,334,886
Members 512,157
Posts 32,489,924
Top