Uongozi wa CHADEMA na hatima ya sisi CHADEMA, wao ni wasaliti

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Licha ya misukosuko kadhaa iliyowahi kukitikisa CHADEMA bado umuhimu wa umoja ndani ya chama umeendelea kuwa muhimu na kudumishwa hadi hivi karibuni.

Ingawa CHADEMA kipo kwenye mchakato wa mapitio kutoka chama uanaharakati kwenda chama taasisi ili kukidhi matakwa ya kukabidhiwa nchi, sehemu kubwa inayogonga vichwa vya wanachama na wanachi kwa sasa ni mtifuano wa uongozi unaoendelea ndani ya chama.

Wapo wanataka kundi moja litoswe na wengine wakitaka kuwepo na maridhiano huku wengine wakiona kuwa chama kimekosa viongozi waadilifu wanaosimamia katiba, kanuni, itifaki na kutokana na tatizo hilo, viongozi wamekuwa ni chanzo cha matatizo kwenye chama na kufanya uchaguzi ili kuwapata viongozi wapya ndiyo utakiponya katika matatizo haya.

Tukiwa tunatafakari yanayoendelea ndani ya CHADEMA, hatuna budi kuijongea falsafa ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyoitoa Machi 13, 1995 alipokutana na Waandishi wa Habari wa Tanzania katika Hoteli ya Kilimanjaro nyakati hizo.

Katika hotuba hiyo Mwalimu alizungumzia nyufa tano alizoziona Tanzania wakati huo na ufa wa kwanza ilikuwa ni Muungano wa Tanzania.

Mwalimu alisema kuwa nchi changa ni sawasawa na nyumba mpya na kwa mantiki hiyo, hata mimi ninasema, chama cha siasa kichanga kama CHADEMA ni sawasawa na nyumba mpya.

CHADEMA ni kama nyumba mpya. WanaCHADEMA waanzilishi wameijenga vizuri baada ya kutayalisha katiba, msingi, kanuni na pia itifaki. Waanzilishi walikuwa na furaha kwa jinsi ilivyokuwa inapendeza huku wakipeana mgawanyo kazi na kikomo chake kuusimamia bila kinyongo.

Kwa bahati nzuri au mbaya haikuwahi kupata mtikisiko wa kisiasa mpaka hivi karibuni. Kwa sasa CHADEMA inatikiswa. Na mtikisiko umeonyesha jinsi nyumba ilivyo mbovu baada ya nyufa kubwa za kiuongozi kuonekana hata kwa wapita njia.

Kama mtikisiko huu utaendelea kuna hatari ya nyumba ya CHADEMA kubomoka hasa iwapo hizi nyufa kubwa na ndogo hazitazibwa kisiasa (katiba, kanuni, itifaki, hekima na busara) au kisheria (Mahakamani) kwa ustadi wa hali ya juu. Kama msisitizo wa uzibaji wa nyufa hautaanzia kwenye kutengeneza msingi imara wa kitaasisi, kuna uwezekano mkubwa wa nyumba kupata nyufa zaidi na hasa kama mtikisiko utatokea hapo baadaye na kuanguka.

Baadhi ya wanachama wa CHADEMA kwa sasa wanazungumza kuwa sisi ni CHADEMA na wao wasaliti, baadhi ni viongozi wa CHADEMA , wanajivunia ubaguzi. Nadhani wengine wanafikiria hata kuanzisha vikundi vyao ndani ya chama na kuwafukuza wengine "Wapo, si wengi; lakini wapo. Kuwafukuza wengine maana yake ni kuvunja chama kilichoko. Chama kivunjike kisiwe kile cha mwanzo kilichoachwa na waanzilishi. Kuwe na vyama viwili ndani ya kimoja. Hili ni jambo linalozungumzwa kwa sasa na baadhi ya wanachama.

CHADEMA inahitaji viongozi watakaoelewa kuwa kuzungumza sisi CHADEMA na wao wasaliti si fahari. Hatima yake ni kukivunja chama. " ndani ya CHADEMA, mtu mwenye akili timamu hawezi kufikiri sisi CHADEMA na wao wasaliti ni fahari:

Hawezi akautukuza ubaguzi kwa kujiita ‘sisi ni CHADEMA' na ‘wao ni wasaliti'.

Asiye na akili, atadhani ile ina usalama ndani yake. Kwamba, wenye chama wale, wasaliti wale una usalama ndani yake.

Ngoma ikipigwa sana, hatima yake CHADEMA itameguka. wenye CHADEMA wakijitenga kutokana na ulevi tu wa sisi CHADEMA na wao wasaliti', wakumbuke kwamba CHADEMA ndiyo inawafanya waseme ‘sisi CHADEMA wao wasaliti'. Nje ya CHADEMA ya sasa, hawawezi kusema hivyo: kuna ‘wao mkoa fulani, wilaya fulani na kabila fulani' na ‘sisi mkoa fulani, wilaya fulani na kabila fulani'. "Napenda wajue hivyo. Nje ya CHADEMA hakuna ‘sisi CHADEMA wao wasaliti'. Hakuna.

Kinachowafanya wajiite ‘sisi; ni ubaguzi. Wakiisha kuwabagua wengine, ile dhambi ya ubaguzi, haifi itaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukisha kuitenda inaendelea: Ni kama kula nyama ya mtu, utaendelea kuila. "Watamaliza watatengana na wengine halafu, mara watakuta kumbe ‘sisi si wa sehemu fulani katika wilaya fulani'. Ndani yake kuna ‘Wasukuma wa Bariadi, Maswa, kahama. Kuna Wabena, Wakidigo, Wagogo, Wahaya, Wahehe, Wameru, Wakimoshi (Wachaga), Wamakonde, Wamakua, Wanyakyusa, Wanyilamba, Wamasai, Wanyamwezi, Wanyakyusa (wa Ngonde), Washambala, Waswahili, waiyao, n.k.

Wengine wakitengwa na kufukuzwa, watapata msukosuko kidogo na kujikunyata pembeni wakisema, kweli tumetengwa!. Ni kweli tumefukuzwa! Waliofukuzwa na kutengwa hawatasarambatika, watakuwa wamoja. Watashikamana.

Wanaosema sisi CHADEMA watakuta kumbe kuna wengine zaidi ya walivyokuwa wanafikiria. Watataka tena kuwatenga. Hawatakaa salama. Hawawezi kukaa salama baada ya kutenda dhambi ya kuwabagua wanachama ndani ya CHADEMA na kuwaita ‘wale wao na hao siyo sisi'.

Dhambi ile haishii hapo. Ndivyo historia ilivyo; ni sheria ya historia siyo sheria ya Mwanadamu. Huwezi kufanya ubaguzi wa namna hiyo halafu dhambi ile ikuache hapo hapo. Hapana, itakuandama mpaka kaburini kama ilivyoiandama NCCR-Mageuzi mpaka leo ambapo kutoka wabunge 24 mwaka 1995 mpaka wabunge 4 mwaka 2010.
 
Nataka nitamke mapema sana kwamba sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika.
Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka"-Zitto Kabwe.


"Hakuna namna ambavyo chama chochote kinaweza kushawishi umma kwamba kitapigania demokrasia katika nchi wakati kinayahainisha mapambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenyewe"-Dkt. Kitila Mkumbo.
 
Nataka nitamke mapema sana kwamba sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika.
Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka"-Zitto Kabwe.


"Hakuna namna ambavyo chama chochote kinaweza kushawishi umma kwamba kitapigania demokrasia katika nchi wakati kinayahainisha mapambano ya kidemokrasia ndani ya chama chenyewe"-Dkt. Kitila Mkumbo.

Mie hizi thread zenu mpya mnazozileta naona zinanichosha tu. Nyie endeleeni mie mtanikuta kule kwenye POLL..... Naendelea kushuhudia jinsi Mlume anavyoendelea kushikishwa kiwambaza!
 
Mie hizi thread zenu mpya mnazozileta naona zinanichosha tu. Nyie endeleeni mie mtanikuta kule kwenye POLL..... Naendelea kushuhudia jinsi Mlume anavyoendelea kushikishwa kiwambaza!
Kama zinakuchosha kwa nini unazisoma?. Kitu gani kimekufanya usome wakati wewe umeishakata ushauri kulingana na fikra na mtazamo wako katika mwenendo wote wa hoja katika hili bandiko.

Sitakosea nikisema unasumbuliwa na unafiki. Unafiki ni siraha ya ulaghai katika chama.
 
Chanzo cha yte hayo ni ubaguz tna wakipumbavu xxna, kiukweli nlikuwa mfuac mzur xna wa CHADEMA, ila kwasasa imetambua kuwa CHADEMA co cha cha kukabidhiwa nchi hata kidogo, tangu nlipo ona haya wanayo yafanya CHADEMA ni wamekuwa mataperi wakubwa, na kwa mwendo huu! Naimani hata cku moja CHADEMA haita kuja kushika Nchi na itakuwa ndto kama hawata acha Uzandiki, Jeuri ya kufanya chama ni cha Kabila na Kanda fulani na CHADEMA kitaporomoka kama embe linavyo enguliwa mtini, viongoz wa CHADEMA waktaka yote haya yawapite waachan na hup upumbavu wanao ufanya, na unafiki wa kujifanya wao wasafii wakat ni madudu matupu. mkiendedea hamta pata Nchii Ng'ooooooooooooooooooooooo! mtaishia kubwabwaja unafiki, Mmenkera ha ctak tna Siasa Uchwara. Mkumbuke mnavyofanya humu hapa hapa Duniani, mcshike Nchi mtatupeleka kubaya tukajuta kama Libya wanaavyo juta. Na Mungu watazame ta kuzid kuwaumbuwa mukiache chama, Salamu ziwafikie.:A S-confused1::A S-confused1:
A%20S-confused1.gif






 
Back
Top Bottom