Uongozi wa CCM rudisheni utaratibu wa awali wa namna ya kumpata Mbunge, wapatikane 3 kisha ndio wapigiwe kura za maoni. Hili la Kawe ni somo tosha

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,778
28,423
Uongozi wa CCM muda bado mnaweza kufanya mabadiliko rudusheni utaratibu wa zamani ili kumpata mbunge bora, ule utaratibu wa mwanzo wa watu kupimwa kwanza na Kamati husika kabla ya kura za maoni ndio unafaa kisha zipatikane 3 bora zikapigiwe kura za maoni na Wajumbe wa Halmashauri ya Jimbo.

Utaratibu wa sasa unaotaka watia nia wote kupigiwa kura mbele ya wajumbe hatuwezi pata kiongozi bora maana huwezi weka watu wote let say 80 kama hao wa Jimbo la kawe katika ukumbi kisha kila mtu apate muda wa kujielezea na upate kilicho bora, ni kitu kisichowezekana.

Kwanza unawachosha wajumbe watia nia wajieleze 1-80 ni wazi wajumbe watakosa concentration, pili kura zinatakiwa zipigwe siku 1 tu huo muda uko wapi?

Duniani kote kunafanyika kwanza screening kupata walio bora kisha ndio wanashindanishwa, mazingira ya watu wengi kujitokeza kuliko ilivyo kadiriwa kunaharibu umaana wa zoezi hili.
 
Hao wengine sio was kuwazingatia sana kwani lengo lao ni kupata sifa tu kwamba walishiriki kwenye kura za maoni ili hatimaye wapate kuteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali na yule Mussolini meusi a.k.a Meko.
 
Yaani tittle ya uzi tu umeweka gazeti.....duh. siku ingine tafuta mtu akusaidie jinsi ya kutengeneza iliyo short but clear..! Huko kawe inaonyesha ni jinsi gani watu walivyomchoka mbunge anayemaliza muda wake.
 
Kawe ccm haitakiwi hata iweje
 
To Every action there is equal and opposite reaction, gharama ya kununua wapinzani, kuzuia demokrasia imepelekea walafi, wachumia tumbo wanafiki na wasio na mapenzi ya dhati kukimbilia ccm
 
Hao watu wengi wamechukua fomu kwa wingi maana wanajua ukishachaguliwa na ccm, automatically unakuwa mbunge, kwani mwenyekiti wao yuko juu ya katiba, hivyo anaweza kuagiza tume ya uchaguzi imtangaze mgombea wa chama chake, bila kujali maamuzi ya wananchi.
 
Huko Kawe wengi wamekichangia chama. Surely CCM haitoruhusu every Tom & Jerry kupewa platform ya “kumwaga sera” kwa wanachama. Watakatwa juu kwa juu baada ya hela yao kukusanywa
 
Hao watu wengi wamechukua fomu kwa wingi maana wanajua ukishachaguliwa na ccm, automatically unakuwa mbunge, kwani mwenyekiti wao yuko juu ya katiba, hivyo anaweza kuagiza tume ya uchaguzi imtangaze mgombea wa chama chake, bila kujali maamuzi ya wananchi.
Mambo yanaenda kuwageuka, sidhani kama watafanikiwa
 
Hao watu wengi wamechukua fomu kwa wingi maana wanajua ukishachaguliwa na ccm, automatically unakuwa mbunge, kwani mwenyekiti wao yuko juu ya katiba, hivyo anaweza kuagiza tume ya uchaguzi imtangaze mgombea wa chama chake, bila kujali maamuzi ya wananchi.
Kama atafanya hivyo mwaka huu, kutakuwa na mauwaji. Maana hawatakubali kuonewa kirahisi hivyo. Hata yeye maisha yake atakuwa ameyaweka rehani
 
Kama atafanya hivyo mwaka huu, kutakuwa na mauwaji. Maana hawatakubali kuonewa kirahisi hivyo. Hata yeye maisha yake atakuwa ameyaweka rehani

Uchaguzi wa serikali za mitaa yalitokea hayo, na hakuna lolote lilitokea. Huenda safari hii matamanio yako yakatimia. Muda utaamua.
 
Back
Top Bottom