Zanzibar 2020 Uongozi wa ACT wapokelewa Pemba, Maalim Seif amshangaa Rais Magufuli kusema uchaguzi utakuwa huru ilhali hakuna dalili

ACT Wazalendo

Verified Member
May 5, 2014
429
1,000
Leo kuna mapokezi ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Bernard Membe na Mgombea Urais wa Zanzibar, Ndugu, Maalim Seif Sharif Hamad. Wameambatana pia na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Omar Fakih Hamad.

Tayari washawasili Pemba. Picha za matukio ya huko tutakuwa tunawawekea hapa kadiri zinavyotufikia.

#KaziNaBata
#TheFutureIsPurple
================

Zoezi linaloendelea sasa ni kuwatambulisha viongozi wa chama kwa wananchi waliofika kuwalaki.

Mazrui: Nawashukuru wote mlivyojitokeza kwa wingi kuja kuwalaki wagombea na shughuli imefana sana. Umoja wetu ndio nguvu yetu. Wamesema wanataka kuja kuchukua majimbo Pemba, wanao uwezo huo? (Wananchi wanajibu 'Hapanaa'). Hatukubali hii ni ngome ya ACT Tanzania, tusiruhusu ikaguswa.

Wanaota ndoto ya mchana, Pemba hapatoki jimbo. Sina zaidi na salamu zetu ni hizo kutoka Unguja, wameona kwenye mtandao namna gani mmewalipa ya jana.

Mgombea Mwenza: Vyama vyote Tanzania vinatambua Zanzibar inahitaji kuwa na mamlaka yake. Vyote vinaamini Muungano unahitaji kuwa imara wakati pande zote mbili vikipata haki zake.

Tofauti na vyama vingine, ACT kinaamini haya mambo mawili yanawezekana. Pia inaamini iko haja ya kufanywa hivyo. Tunasimama hapa kwa kuahidi mambo hayo yanawezekana na ni moja ya ajenda muhimu ya ACT.

Tofauti na vyama vingine, ACT tunaamini vijana wakitaka jambo halirudi kwa maana hiyo inategemea nguvu na tunavyojua wanafata nyayo ya wazee, tuungane pamoja kuhakikisha Octoba tunapata tulichokuwa tunakipagania kwa miaka mingi ila tunaporwa.

Membe: Leo ujumbe wote tumuona upendo wa wapemba, umeona kura za ushindi za wapemba, umeona ushindi wa kweli wa wapemba, tumemuona Rais mpya wa wazanzibari wote, Rais mpya wa Jamhuri ya muungano kupitia kwenu. Napenda nitoe shukrani za dhati kwa mfano huu mliouonyesha Tanzania nzima.

Leo mitandao yote na wenzangu wa chama kingine wanahangaika kutokuonyesha hadhara hii kwa sababu ya hofu. Watatuweza hawatuwezi?

Leo masheikh wa uamsho walitakiwa wapelekwe mahakamani, hawakupelekwa. Wamenyimwa haki yao, na nasema tena nilichokisema Zanzibar, nikishakuwa Rais Novemba Masheikh watarudishwa hapa Zanzibar.

Vyombo vya mahakama na sheria viko hapa na kama wana makosa washtakiwe hapa, kama hawana makosa nitawaondoa siku ya pili wawe huru. Watatuweza hawatuwezi? Nimesema tena na haki za wazanzibari tutahakikisha mnazipata kwa sababu Zanzibar ni nchi lazima iheshimiwe.

Maalim Seif: Leo ni siku ya kutoa shukraan, niwashukuru nyote ambao tangu asubuhi mko barabarani. Mara nyingi tukija Pemba tunazuiwa kutumia VIP lakini mara hii tumeruhusiwa, tunashukuru polisi pia kwa kulinda msafara wetu kuanzia Airport mpaka hapa.

Lakini ninasikitika sana polisi wanakubali kutumiwa kisiasa, tunaambiwa polisi na vyombo vya ulinzi hawastahiki kuingia kwenye siasa lakini leo wanatumika kisiasa.

Juzi baada ya kuona tsunami Unguja, wakasema Pemba lazima tu-sabbotage. Polisi mnatumwa Alfajiri mkae njiapanda na roadblocks kuwazuia watu wasije. Nawaambia polisi hapa hakuna mfanyakazi wa serikali ambae aliitwa kwa jina aje ampokee mtu.

Hakuna hata mmoja aliepewa gari ama pesa aje kwenye mapokezi lakini wao walipofanya bodaboda zote walipewa mafuta waende airport, leo tunakuja bodaboda wamezuiwa. Polisi ndio kazi yenu hio?

Siwalaumu polisi wadogowadogo, nawalaumu wakuu wa polisi. CCM inabebeka? Mtakwenda na mzoga wenu? Hawa(wananchi) washaamua. Jeshi la polisi mnafanya kazi si zenu, kama nchi hii ikiingia kwenye mavurugu nyie ndio wa kulaumiwa kwa sababu hamfanyi haki, na nyinyi mtakwenda The Hague.

Hawa wanaogopa watu, wakiona watu wengi wanaingiwa kiwewe. Hii ni rasharasha. Namshangaa Rais Magufuli, amesema uchaguzi huu utakuwa huru na haki, mbona hatuoni hizo dalili? Anakuja mgombea wa CCM barabara zote zinafungwa, leo mgombea ana uhakika wa kuchaguliwa mnazuia watu wasije. Waswahili wanasema hiari inashindwa utumwa.

Kubwa nalotaka ni uhuru wa nchi yetu, tumekuwa na wabunge na wawakilishi tangu 95, wameleta mabadiliko hapa? Kama hamna serikali, wasitokee watu wenye tamaa zao wakajaribu kuwachanganyeni wanancho.ACT.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom