Uongozi unaoacha alama.

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Kuna kitu kinaitwa mizani, mizani ni kifaa cha kupimia kitu kwa vipimo vya kilo, mizani inazaa neno mizania. Mizani haitakiwi izidi upande wowote wa kile kinachopimwa. Ikizidi upande wowote kuna mmoja atafaidika na mwingine atapunjika, ikiwa kwenye urari sawia kila mtu atafaidika. Haki pia hupimwa kwenye mizania ya haki, ndio maana kwenye mahakama zetu na vyombo vya sheria hutumia picha ya kikaragosi cha mizani.

Simulizi za akina Yohana Mbatizaji na Yohana mtembezi zinatupa elimu ya mizania ya urari wa haki lakini kwa mitazamo yakinifu na tengeufu. Yohana Mbatizaji akijulikana kama mtume pia ni mtu mwenye simulizi nyingi mpaka kubadilika na kuwa nabii na Mbatizaji. Ametengeneza LEGACY mpaka leo hii kama kiwakilishi cha upendo, utu wema, unyofu wa moyo na kama njia ya wokovu kiimani, kwa wale wana imani na waamini. Yohana huyu ni kiwakilishi cha ulimwengu huru wa nuru.

Tuna huyu Yohani mwingine, Yohana mtembezi ama Yohana chapombe. Ni kutokana na mtu huyu mpaka leo tuna kilevi cha bei ghali, kitamu chenye arikohori ya kutosha tu, ametengeneza LEGACY yake pia.

Simulizi zinasema hapo zamani za kale huko Uskotishi kulikuwa na upungufu wa vileo na Yohana akiwa chapombe maarufu aliweza kutembea kwa miguu muda mrefu tu akisakanya kilevi.. Inasemekana (pengine ni utani tu) hakupenda kupanda gari ili aokoe pesa ya ulabu. Yohana huyu alitembea mji hadi mji akisaka kilevi pendwa. Ni kwa umaarufu wake huu kilizaliwa kileo kikali kiitwacho John Walker kikiwa na kikaragosi cha picha kwa muktadha wa jina. Yohana huyu ni kiwakilishi cha ulimwengu wa nira za starehe, vifungo na tamaa za mwili.

Yohana wa kwanza alizunguka miji mingi akihubiri na kubatiza watu, Yohana wa pili alizunguka miji mingi akitafuta ulabu....

Uongozi unaoacha alama. Unaacha alama gani? Zenye madoa meusi ya damu iliyokauka ama alama zenye rangi nzuri za kuvutia? Mizania ya uongozi unaoacha alama tutaupimaje? Utaegemea wapi? Kwenye haki ama kwenye dhuluma?

Ni sawa na kilio cha samaki machozi yameenda na maji, usifananishe na kilio cha mamba. Siku hizi watu wanatambulika kwa vimo vyao si majina wala vyeo vyao. Vimo! Asante Ally Hapi.

Uongozi unaoacha alama.Yohana Mbatizaji na Yohana mtembezi wote waliacha alama. Kuacha alama si tatizo... Je umeacha alama gani? Kukichwa kutambazuka lakini kabla jua halijachomoza kiza huwa totoro.
 
Nimekuelewa sana mkuu.Yohana mbatizaji yeye anabatiza, Yohana mtembezi yeye anazurura kusaka ulabu na Yohana stone yeye anapasua tu hata damu ikimwagika he dont care.lol
 
Nimekuelewa sana mkuu.Yohana mbatizaji yeye anabatiza, Yohana mtembezi yeye anazurura kusaka ulabu na Yohana stone yeye anapasua tu hata damu ikimwagika he dont care.lol
Yohana,, baba Jesca, wastaafu na wanakaribia kustaafu wamejikatia Tamaa kazini wapo wapo tu,,, Chezea 25% .....
 
Yohana mtembezi siyo wa mchezo hakika amewarisisha kina yehana wenzio yaani yohana wa leo walio katili na roho mbaya isiyo na huruma
 
Unapoharibu ili utengeneze sio jambo baya... Ni jambo zuri pia la la kheri... Lakini unaharibu nini ili utengeneze nini.... Walevi ni watu wema sana.... Hawanyimani, hawapunjani... Lakini anapotokea cha POMBE mmoja akasema huyu mupe, yure muruke... Tambua huyu si mmoja kati ya wale wema ni mbaguzi asiyefaa... Ana hulka za kutenganisha badala ya kuunganisha, kubomoa badala ya kujenga.. Huyu ni kenge kwenye msafara wa mamba... Mlevi wa kilevi cha madaraka ya kulevya... Pombe yenye kirevi cha arikohori nyingi sana
Hatununui ambulance badala yake tunanunua maroli ya kubebea maiti zilizokufa.... Ukisikia uchuro ndio huu... Uongozi unaoacha alama
 
Kwenye ukusanyaji wa kodi Zakayo alikuwa haruki nyumba wala mtaa ila kwa kwenye kuleta huduma utamsikia Zakayo ajisifia na kubagua kana kwamba pesa katoa mfukoni mwake
 
Kwenye ukusanyaji wa kodi Zakayo alikuwa haruki nyumba wala mtaa ila kwa kwenye kuleta huduma utamsikia Zakayo ajisifia na kubagua kana kwamba pesa katoa mfukoni mwake
.
IMG-20181223-WA0016.jpeg
 
uongozi unaoacha alama ni ule ambao mtu akiukumbuka tu hutokwa na machozi ya furaha ama ya huzuni. Yesu mwenyewe aliacha alama kama kiongozi nzuri kwa wale aliowatendea mazuri na mbaya kwa wale walioamini wanaonewa kama wale waliokuwa wanafanya biashara hekaluni lazima wachukie. hekalu ni nyumba takatifu ya Mungu inatakiwa iwe safi kwa uchafu wa aina yote.

kiongozi asiyetaka kusafisha nyumba yake inapochafuka huyo si mzuri. sharti ya nyumba iwe safi na hiyo ndio alama pekee ambayo kiongozi anatakiwa kuiacha, kusafisha nyumba iwe safi. je unadhani wale waliochafua hiyo nyumba , uchafu wao unapotelewa kiongozi ataacha alama nzuri kwao?
 
Rip Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aka Mchonga meno
 
Back
Top Bottom