Uongozi Unahitaji Hekima


Sifa kubwa ya Kiongozi ni hekima, na kuwasikiliza unaowaongoza hata kama wako kinyume na wewe.
Huku kwetu huyo bwana anayempinga Obama angepotezwa!!! Kama alivyopatezwa yule diwani kule Kigoma kabla hata jiwe halijafika alichukuliwa akahifadhiwa ili asije kumpinga! Hajarudishwa hadi leo, na haijulikani aliuliwa ama la! Na waliomchukua wanajulikana wazi!!

Taifa lina laana hili!!
 
Sijui tunakwama wapi?
Lakini lazima tujue hatuwezi kuwa na mawazo sawa.
Na pia tujue hamna mtanzania mwenye haki sana kuliko mwingine.
Katika kulijenga taifa letu tuna mawazo tofauti na yote yana mchango sawa kuimarisha na kulijenga taifa
Asante
 
Na hekima itafaa nini ikiwa rasilimali zinaibiwa, hekima ina tija gani hasa wakati watendaji wa serikali ni wabadhilifu na wasio aminika. Sisi huku Tz hekima itafaa nini wakati pale Ngende kijijini zahanati ya kijiji hakuna kibatari katika chumba cha mapumziko.

Hapa kwetu sisi hekima si mahala pake. Huyu wa kwetu ana mengi ya kuyaonyesha na kutenda zaidi ya hekima katika uongozi wake kwenda kwa raia.

Kumfananisha Obama na huyu wa kwetu ni kumkosea adabu huyu wa kwetu kipenzi.

Waache marekani wawe na hekima kwa sababu wao washamaliza safu yao ya mahitaji na wanatafuta ziada. Kwetu bado.
 
Back
Top Bottom