Uongozi UDSM wasema hapana kwa Zitto Kuunguruma

Nimepewa taarifa kuwa vijana wa DUPSA wametoa tamko kali kwa uongozi wa chuo na kulaani jinsi walivyosingiziwa kuwa hawakufuata sheria wameonyesha jinsi mkandala alivyo muongo.

Nalitafuta nikilipata nitaliweka hapa hilo tamko lao.

Good, M/kieleweke

Hapo ndo patakuwa patamu tutakapo pata majibu ya upande wa pili kwamba kweli hawakufata utaratibu? ama ndo kama nilivo sema hapo nyuma kwamba Majibu ya Mkandala ni sawa na majibu ya Karamagi kwa issue ya Zitto!!!
 
Tamko lenyewe hili hapa,

DAR ES SALAAM UNIVERSITY POLITICAL SCIENCE
STUDENTS' ASSOCIATION (DUPSA)

TAMKO DHIDI YA KITENDO CHA UONGOZI WA CHUO
KUSITISHA MDAHALO HALALI CHUONI

I. UTANGULIZI
Jumamosi, Septemba 29, 2007, Uongozi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ulisitisha kufanyika kwa mdahalo wa wazi uliolenga kujadili mada ya "Hali ya elimu ya juu nchini na nafasi ya wanafunzi wa elimu ya juu katika maendeleo ya nchi", uliokuwa ufanyike kwenye ukumbi wa "Theatre 1". DUPSA tuliitisha mdahalo huu tukishirikiana na taasisi ya mtandao wa wanafunzi Tanzania "TSNP" kwa lengo la kutoa fursa kwa wanachuo kubadilishana uzoefu na kuibua fikra mbadala za kutatua kero na matatizo ya kielimu na kutimiza wajibu wao kwa maendeleo ya taifa.

Tulifanya hivi kwa nia njema, tulifanya hivi kutimiza wajibu wetu wa kitaasisi ambao unatutaka kuwa jukwaa la kuchochea utashi wa kitaaluma kwa wanachuo, kwa kuwawezesha kujifunza mambo mengi zaidi ya yale wafunzwayo darasani. Tulifanya hivi tukizingatia maslahi ya wanachuo na mustakabali wa taifa ambao jamii ya wanachuo kama sehemu ya taifa inawajibu wa kuulinda. Tulifanya hivi tukizingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazopaswa kufuatwa na taasisi za kitaaluma kwa mujibu wa sheria na itifaki za chuo hiki.

Pamoja na mazuri yote haya ambayo yalikusudiwa na mdahalo huo, uongozi wa chuo ghafla ulitutaka tusitishe na baadaye kupitia kwa Ndugu Maro (Deputy Dean of Students) ukatangaza kuahirishwa kwa mdahalo huo pasipo kutoa sababu licha ya kuulizwa na wanachuo. Baadaye kupitia mahojiano na waandishi wa habari viongozi wa chuo hasa Afisa Uhusiano wa chuo Bwana Julius Saule na Makamu Mkuu wa chuo Profesa Rwekaza Mukandala, walitoa hoja mbalimbali kuhalalisha uamuzi wa chuo. Nyingi ya hoja hizo zimeidhalilisha DUPSA na TSNP kama taasisi pamoja na viongozi wake kwa kudaiwa kutozingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuandaa mdahalo huo. Kutokana na uzito wa madai hayo dhidi ya taasisi hizi zinazoheshimika - DUPSA na TSNP, tunachukua fursa hii kuueleza umma wa wanachuo na watanzania kwa ujumla jinsi ukweli wa mambo ulivyokuwa.

II. HOJA ZA CHUO NA UKIUKWAJI WA HAKI.
DUPSA inatamka kuwa uamuzi uliochukuliwa na uongozi wa chuo kusitisha, kukwamisha ama kuahirisha mdahalo huo, haukuzingatia haki na uliambatana na hoja dhaifu zilizokinzana na misingi ya haki na utawala bora, kama ifuatavyo;

1. Kwanza, licha ya DUPSA kuwa wa kwanza kuomba na kuruhusiwa kufanya mdahalo huo kwenye ukumbi wa Nkrumah, baadaye mdahalo huo ulihamishiwa kwenye ukumbi wa Nyerere Theatre 1 kwa kile kilichodaiwa kuwa kulitokea tukio lingine lililohitaji ukumbi wa Nkrumah. Uamuzi huu ulionesha ni jinsi gani uongozi wa chuo ulivyothamini zaidi tukio hilo lingine na kupuuza mdahalo wa wanachuo uliostahili ukumbi wa Nkrumah kwani tulikuwa wa kwanza kuuomba.

2. Uongozi wa chuo haukutenda haki kusitisha mdahalo ghafla yaani takribani masaa 12 kabla ya tukio tena kwa taarifa ya simu iliyopigwa saa 1:59 usiku – muda ambao kimsingi si muda wa kazi. Inastaajabisha kuona uongozi wa chuo ulichukua uamuzi huu dakika za mwisho ilhali ulijua fika kuwa washiriki wa mdahalo huo walikwishatangaziwa uwepo wa mdahalo huo kwa takribani wiki moja na zaidi kabla ya tukio. Uongozi wa chuo ulikuwa wapi siku zote hizo?Ama uamuzi huu wa ghafla ulitoka wapi?.

3. Uongozi wa chuo ulisitisha mdahalo kwa hoja kuwa mdahalo huo ungekuwa ni makelele na usumbufu kwa mkutano wa mabalozi uliokuwa ufanyike ukumbi wa jirani. Hii nayo ni hoja nyepesi na dhaifu mno;

 Kwanza, walipotuhamishia ukumbi wa "Theatre 1" kutoka Nkrumah bila shaka walishakuwa na taarifa za kuwepo mkutano wa mabalozi jirani na ukumbi huo kwa hiyo, kusitishwa kwa mdahalo huo hakukuwa halali.

 Pili, uongozi wa chuo ulijuaje kuwa mdahalo wetu ungekuwa ni kelele na usumbufu kwa mkutano wa mabalozi?

 Tatu, Kwanini haukufikiria kwamba mabalozi nao wangeweza kuwa ni kelele na usumbufu kwa mdahalo wa wanachuo?

 Nne, kwa kuwa kelele zingeweza kutolewa na yeyote kati ya mabalozi au wanachuo, Je kulikuwa na uhalali gani kusitisha mdahalo wa wanachuo na si kusitisha mkutano wa mabalozi?Au mabalozi wana haki zaidi ya kutumia kumbi za chuo kuliko wanachuo ambao ndio wadau wakuu wa chuo hiki?

4. Hoja kwamba DUPSA tulikiuka utaratibu wa kuomba ruhusa ya mkutano (mdahalo) haina ukweli wowote. Ukweli ni kuwa, DUPSA tulifuata taratibu zote za kuomba ruhusa za kufanya mdahalo na shahidi wa hili ni uongozi wa chuo wenyewe maana huo ndio ulioturuhusu tufanye mdahalo katika ukumbi wa Nkrumah na baadaye ukatuhamishia Theatre 1. Kama DUPSA isingefuata taratibu isingeweza kupangiwa kumbi yoyote kati ya hizo.

5. Kwamba mdahalo ulisitishwa kwa kuzingatia sheria ya vyuo vikuu hasa ya mwaka 2005 inayokataza masuala ya kisiasa kufanyika katika vyuo, hili nalo linashangaza na kushitua.
Mdahalo ulioitishwa haukuwa wa kisiasa - mada, aina ya washiriki na watoa mada vyote vilitangazwa. Hoja kuwa mdahalo ungekuwa wa kisiasa eti kwa sababu mmoja wa watoa mada alikuwa ni Mhe. Zitto Kabwe, haikuwa na msingi kwani hakualikwa kufanya siasa na hakuitwa kwa kuzingatia nafasi yake ya kisiasa. Alialikwa kufanya kazi ya kitaaluma (kutoa mada) kama mwanataaluma, na alialikwa kwa kuzingatia uzoefu wake katika masuala yanayogusa wanachuo kama mmoja wa viongozi wa zamani wa serikali ya wanafunzi ya chuo hiki. Pia, alialikwa kwa kuzingatia kuwa naye ana haki ya kikatiba kama mtanzania yeyote yule, ya kushiriki mijadala na kutoa mawazo yake.

Kwa mantiki hii, DUPSA tunasisitiza kuwa mdahalo tuliokuwa tumeitisha haukuwa na maslahi ya kisiasa kwa mtu yeyote yule. Hata hivyo, tunashawishika kuamini kuwa uamuzi uliochukuliwa na uongozi wa chuo kusitisha mdahalo huo, ndio uliokuwa wa kisiasa".

6. Hoja ya kusitishwa kwa mdahalo huo eti kwa sababu tulialika wanafunzi wa vyuo vingine jambo ambalo lingesababisha kuwepo kwa umati mkubwa, nayo inaonyesha kujikanganya kwa uongozi wa chuo. Kama walijua mdahalo wa wanachuo ungekuwa na umati mkubwa, kwanini walituhamisha kutoka kwenye ukumbi mkubwa wa Nkrumah na kutupeleka kwenye ukumbi mdogo wa Theatre 1?. Katika hali hii, mtu akifikiri kuwa uongozi wa chuo ulipanga kwa makusudi kukwamisha mdahalo huo atakuwa anakosea?, maana hata huko Theatre 1 tulikohamishiwa hatimaye tulikatazwa kutumia. Na hata huo ukumbi wa jirani uliodaiwa kuwa na mkutano wa mabalozi, mkutano huo haukufanyika.

7. Katika hali ya kuzidi kuhalalisha uamuzi wake, uongozi wa chuo ulidai kuwa haukujulishwa nani angekuwa msemaji mkuu wa mdahalo huo. Kwa hili, ni dhahiri kuwa uongozi wa chuo unakiuka dhana ya "uhuru wa kuzungumza" maana hoja yao inamaanisha kuwa ni lazima tuwataarifu nani wa kuzungumza naye ili wampime kisha waamue tuzungumze naye au tusizungumze naye. Kwani wanachuo ni wafungwa au wako kizuizini.

III. MSIMAMO WA DUPSA.
DUPSA inalaani vikali kitendo kisicho halali cha uongozi wa chuo kusitisha isivyohalali mdahalo huu halali ulioalika washiriki halali na waliolengwa kihalali na taasisi hii halali kwa kushirikiana kihalali na "TSNP".

DUPSA, inautaka uongozi wa chuo uwaombe radhi wanachuo hususani washiriki wote waliojitokeza kuhudhuria mdahalo ule uliositishwa katika dakika za mwisho kwa sababu zisizo za msingi. Uongozi wa chuo ufanye hivyo, kwa kuzingatia kuwa washiriki hao walitumia gharama kama, fedha, muda, nguvu, na akili kuhudhuria mdahalo uliositishwa pasipo kutaarifiwa kwa wakati muafaka na pasipo kufidiwa gharama hizo walizoingia.

DUPSA, inatoa mwito kwa uongozi wa chuo kuzingatia vyema sheria na taratibu za chuo pamoja na katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama.

Aidha, DUPSA tunatoa pole kwa wanachuo na washiriki wote ambao waliathirika kwa namna moja ama nyingine kutokana na kusitishwa kwa mdahalo huo.

DUPSA inawahakikishia kuwa itaendelea kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kufuata sheria na taratibu za chuo na katiba ya nchi kama ilivyofanya katika maandalizi ya mdahalo huo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki DUPSA.

Imetolewa na;

Mambo, James.
Naibu Katibu Mkuu – DUPSA
Tarehe 1 Oktoba, 2007
 
Tamko hili limebandiokwa kwenye mbao zote za matangazo chuo kikuu pale mlimani.

Sasa kuna haja ya kujadili baada ya kuusikia upande wa pili wanasemaje juu ya kadhia hii iliyojitokeza siku ya jumamosi.

Mimi nimjifunza kuwa nchi hii wapinzani wakiendelea kuibana serikali kuna siku itakuwa ni ya kidikteta , na uhuru wa kutoa maoni unaweza ukawa ni kwa ajili ya wateule wachache.
 
Jamani wenye utaalamu, saidia kuweka picha ya gazeti la uwazi ipo kwa mjengwa na hata kule kwa Abdala mrisho, yaani ni aibu!

Askari na slaa za nguvu wamebebelea eti wote hao wanaenda kumzuia an 'empty handed guy- Zitto' asiingie chuo kikuu??

Bado tuna safari ndefu sana aisee!
 
DAR ES SALAAM UNIVERSITY POLITICAL SCIENCE
STUDENTS’ ASSOCIATION (DUPSA)

TAMKO DHIDI YA KITENDO CHA UONGOZI WA CHUO
KUSITISHA MDAHALO HALALI CHUONI

I.UTANGULIZI
Jumamosi, Septemba 29, 2007, Uongozi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ulisitisha kufanyika kwa mdahalo wa wazi uliolenga kujadili mada ya “Hali ya elimu ya juu nchini na nafasi ya wanafunzi wa elimu ya juu katika maendeleo ya nchi”, uliokuwa ufanyike kwenye ukumbi wa “Theatre 1”. DUPSA tuliitisha mdahalo huu tukishirikiana na taasisi ya mtandao wa wanafunzi Tanzania “TSNP” kwa lengo la kutoa fursa kwa wanachuo kubadilishana uzoefu na kuibua fikra mbadala za kutatua kero na matatizo ya kielimu na kutimiza wajibu wao kwa maendeleo ya taifa.

Tulifanya hivi kwa nia njema, tulifanya hivi kutimiza wajibu wetu wa kitaasisi ambao unatutaka kuwa jukwaa la kuchochea utashi wa kitaaluma kwa wanachuo, kwa kuwawezesha kujifunza mambo mengi zaidi ya yale wafunzwayo darasani. Tulifanya hivi tukizingatia maslahi ya wanachuo na mustakabali wa taifa ambao jamii ya wanachuo kama sehemu ya taifa inawajibu wa kuulinda. Tulifanya hivi tukizingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazopaswa kufuatwa na taasisi za kitaaluma kwa mujibu wa sheria na itifaki za chuo hiki.

Pamoja na mazuri yote haya ambayo yalikusudiwa na mdahalo huo, uongozi wa chuo ghafla ulitutaka tusitishe na baadaye kupitia kwa Ndugu Maro (Deputy Dean of Students) ukatangaza kuahirishwa kwa mdahalo huo pasipo kutoa sababu licha ya kuulizwa na wanachuo. Baadaye kupitia mahojiano na waandishi wa habari viongozi wa chuo hasa Afisa Uhusiano wa chuo Bwana Julius Saule na Makamu Mkuu wa chuo Profesa Rwekaza Mukandala, walitoa hoja mbalimbali kuhalalisha uamuzi wa chuo. Nyingi ya hoja hizo zimeidhalilisha DUPSA na TSNP kama taasisi pamoja na viongozi wake kwa kudaiwa kutozingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuandaa mdahalo huo. Kutokana na uzito wa madai hayo dhidi ya taasisi hizi zinazoheshimika - DUPSA na TSNP, tunachukua fursa hii kuueleza umma wa wanachuo na watanzania kwa ujumla jinsi ukweli wa mambo ulivyokuwa.

II.HOJA ZA CHUO NA UKIUKWAJI WA HAKI.
DUPSA inatamka kuwa uamuzi uliochukuliwa na uongozi wa chuo kusitisha, kukwamisha ama kuahirisha mdahalo huo, haukuzingatia haki na uliambatana na hoja dhaifu zilizokinzana na misingi ya haki na utawala bora, kama ifuatavyo;

1.Kwanza, licha ya DUPSA kuwa wa kwanza kuomba na kuruhusiwa kufanya mdahalo huo kwenye ukumbi wa Nkrumah, baadaye mdahalo huo ulihamishiwa kwenye ukumbi wa Nyerere Theatre 1 kwa kile kilichodaiwa kuwa kulitokea tukio lingine lililohitaji ukumbi wa Nkrumah. Uamuzi huu ulionesha ni jinsi gani uongozi wa chuo ulivyothamini zaidi tukio hilo lingine na kupuuza mdahalo wa wanachuo uliostahili ukumbi wa Nkrumah kwani tulikuwa wa kwanza kuuomba.

2.Uongozi wa chuo haukutenda haki kusitisha mdahalo ghafla yaani takribani masaa 12 kabla ya tukio tena kwa taarifa ya simu iliyopigwa saa 1:59 usiku – muda ambao kimsingi si muda wa kazi. Inastaajabisha kuona uongozi wa chuo ulichukua uamuzi huu dakika za mwisho ilhali ulijua fika kuwa washiriki wa mdahalo huo walikwishatangaziwa uwepo wa mdahalo huo kwa takribani wiki moja na zaidi kabla ya tukio. Uongozi wa chuo ulikuwa wapi siku zote hizo?Ama uamuzi huu wa ghafla ulitoka wapi?.

3.Uongozi wa chuo ulisitisha mdahalo kwa hoja kuwa mdahalo huo ungekuwa ni makelele na usumbufu kwa mkutano wa mabalozi uliokuwa ufanyike ukumbi wa jirani. Hii nayo ni hoja nyepesi na dhaifu mno;

Kwanza, walipotuhamishia ukumbi wa “Theatre 1” kutoka Nkrumah bila shaka walishakuwa na taarifa za kuwepo mkutano wa mabalozi jirani na ukumbi huo kwa hiyo, kusitishwa kwa mdahalo huo hakukuwa halali.

Pili, uongozi wa chuo ulijuaje kuwa mdahalo wetu ungekuwa ni kelele na usumbufu kwa mkutano wa mabalozi?

Tatu, Kwanini haukufikiria kwamba mabalozi nao wangeweza kuwa ni kelele na usumbufu kwa mdahalo wa wanachuo?

Nne, kwa kuwa kelele zingeweza kutolewa na yeyote kati ya mabalozi au wanachuo, Je kulikuwa na uhalali gani kusitisha mdahalo wa wanachuo na si kusitisha mkutano wa mabalozi?Au mabalozi wana haki zaidi ya kutumia kumbi za chuo kuliko wanachuo ambao ndio wadau wakuu wa chuo hiki?

4.Hoja kwamba DUPSA tulikiuka utaratibu wa kuomba ruhusa ya mkutano (mdahalo) haina ukweli wowote. Ukweli ni kuwa, DUPSA tulifuata taratibu zote za kuomba ruhusa za kufanya mdahalo na shahidi wa hili ni uongozi wa chuo wenyewe maana huo ndio ulioturuhusu tufanye mdahalo katika ukumbi wa Nkrumah na baadaye ukatuhamishia Theatre 1. Kama DUPSA isingefuata taratibu isingeweza kupangiwa kumbi yoyote kati ya hizo.

5.Kwamba mdahalo ulisitishwa kwa kuzingatia sheria ya vyuo vikuu hasa ya mwaka 2005 inayokataza masuala ya kisiasa kufanyika katika vyuo, hili nalo linashangaza na kushitua.
Mdahalo ulioitishwa haukuwa wa kisiasa - mada, aina ya washiriki na watoa mada vyote vilitangazwa. Hoja kuwa mdahalo ungekuwa wa kisiasa eti kwa sababu mmoja wa watoa mada alikuwa ni Mhe. Zitto Kabwe, haikuwa na msingi kwani hakualikwa kufanya siasa na hakuitwa kwa kuzingatia nafasi yake ya kisiasa. Alialikwa kufanya kazi ya kitaaluma (kutoa mada) kama mwanataaluma, na alialikwa kwa kuzingatia uzoefu wake katika masuala yanayogusa wanachuo kama mmoja wa viongozi wa zamani wa serikali ya wanafunzi ya chuo hiki. Pia, alialikwa kwa kuzingatia kuwa naye ana haki ya kikatiba kama mtanzania yeyote yule, ya kushiriki mijadala na kutoa mawazo yake.

Kwa mantiki hii, DUPSA tunasisitiza kuwa mdahalo tuliokuwa tumeitisha haukuwa na maslahi ya kisiasa kwa mtu yeyote yule. Hata hivyo, tunashawishika kuamini kuwa uamuzi uliochukuliwa na uongozi wa chuo kusitisha mdahalo huo, ndio uliokuwa wa kisiasa”.

6.Hoja ya kusitishwa kwa mdahalo huo eti kwa sababu tulialika wanafunzi wa vyuo vingine jambo ambalo lingesababisha kuwepo kwa umati mkubwa, nayo inaonyesha kujikanganya kwa uongozi wa chuo. Kama walijua mdahalo wa wanachuo ungekuwa na umati mkubwa, kwanini walituhamisha kutoka kwenye ukumbi mkubwa wa Nkrumah na kutupeleka kwenye ukumbi mdogo wa Theatre 1?. Katika hali hii, mtu akifikiri kuwa uongozi wa chuo ulipanga kwa makusudi kukwamisha mdahalo huo atakuwa anakosea?, maana hata huko Theatre 1 tulikohamishiwa hatimaye tulikatazwa kutumia. Na hata huo ukumbi wa jirani uliodaiwa kuwa na mkutano wa mabalozi, mkutano huo haukufanyika.

7.Katika hali ya kuzidi kuhalalisha uamuzi wake, uongozi wa chuo ulidai kuwa haukujulishwa nani angekuwa msemaji mkuu wa mdahalo huo. Kwa hili, ni dhahiri kuwa uongozi wa chuo unakiuka dhana ya “uhuru wa kuzungumza” maana hoja yao inamaanisha kuwa ni lazima tuwataarifu nani wa kuzungumza naye ili wampime kisha waamue tuzungumze naye au tusizungumze naye. Kwani wanachuo ni wafungwa au wako kizuizini.

III.MSIMAMO WA DUPSA.
DUPSA inalaani vikali kitendo kisicho halali cha uongozi wa chuo kusitisha isivyohalali mdahalo huu halali ulioalika washiriki halali na waliolengwa kihalali na taasisi hii halali kwa kushirikiana kihalali na “TSNP”.

DUPSA, inautaka uongozi wa chuo uwaombe radhi wanachuo hususani washiriki wote waliojitokeza kuhudhuria mdahalo ule uliositishwa katika dakika za mwisho kwa sababu zisizo za msingi. Uongozi wa chuo ufanye hivyo, kwa kuzingatia kuwa washiriki hao walitumia gharama kama, fedha, muda, nguvu, na akili kuhudhuria mdahalo uliositishwa pasipo kutaarifiwa kwa wakati muafaka na pasipo kufidiwa gharama hizo walizoingia.

DUPSA, inatoa mwito kwa uongozi wa chuo kuzingatia vyema sheria na taratibu za chuo pamoja na katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama.

Aidha, DUPSA tunatoa pole kwa wanachuo na washiriki wote ambao waliathirika kwa namna moja ama nyingine kutokana na kusitishwa kwa mdahalo huo.

DUPSA inawahakikishia kuwa itaendelea kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kufuata sheria na taratibu za chuo na katiba ya nchi kama ilivyofanya katika maandalizi ya mdahalo huo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki DUPSA.

Imetolewa na;

Mambo, James.
Naibu Katibu Mkuu – DUPSA
Tarehe 1 Oktoba, 2007
 
Wanafunzi bado wanamhitaji Mh. Zitto:

Mtandao wa wanafunzi wamlilia Zitto

2007-10-05 17:35:58
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania, TNSP, Tawi la Dar es Salaam umezungumzia kitendo cha `kupigwa stop` kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe kuhudhuria mkutano mmoja wa majadiliano ya kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa hakikuwa sahihi.

Aidha, mtandao huo umetoa taarifa inayotaka Chuo Kikuu Dar es Salaam kuache kuzuia mijadala inayolenga kupanua fikra za wanafunzi.

Mratibu wa mahusiano wa mtandao huo, Bw. Dady Igogo, amesema wameamua kutoa tamko hilo kufuatia hatua ya Mhe. Zitto kuzuiwa kuhudhuria mjadala ulioandaliwa na mtandao huo chuoni hapo.

Akasema Mhe. Zitto alialikwa pamoja na mwanarakati aitwaye Said Mussa kwenda kutoa mada kwenye mjadala huo uliokuwa na ajenda isemayo `nafasi ya wanafuzi wa elimu ya juu katika jamii`, ukiwa na lengo la kuibua fikra pevu katika utatuzi wa matatizo ya jamii.

Amesema mtandao huo uliamua kumualika Mhe. Zitto kama msomi mwenzao aliyewahi kusoma chuoni hapo, mbunge na kiongozi kama walivyo viongozi wengine.

Akasema kwa sababu hyo, kitendo cha kumzuia hakikuwa sahihi.

``Kumzuia Zitto ilikuwa sawa na unyanyasaji� hatuamini kama kulikuwa na sababu yenye nguvu kiasi cha kumzuia asihudhurie mkutano wetu,`` akasema Bw. Igogo.

Aidha, akasema uamuzi huo wa kumzuia Zitto ulitolewa katika muda ambao wao tayari walishafanya maandalizi ya kuwa naye na matokeo yake wanafunzi wengi wakakerwa na hatua hiyo.

``Uamuzi wa kumzuia Zitto ulitufikia Septemba 28, saa 2:15 usiku, wakati mjadala ulitakiwa ufanyika Septemba 29 kuanzia saa 2:00 asubuhi� kitendo hicho kiliwaudhi wengi ambao walijiandaa kusikiliza mjadala huo, `` akasema.

Hata hivyo, wakati TSNP wakitoa maelezo hayo, uongozi wa Chuo Kikuu Dar ulishatoa taarifa kuwa Mhe. Zitto alizuiwa kwakuwa waandaaji wa mkutano huo hawakuwa wamefuata taratibu za chuo.

SOURCE: Alasiri

Source link: Ipp Media.

SteveD.
 
Mwisho wa ngoma ni lelee ,na huu bilaq shaka ni mwisho wa hawa mafisadi hawataki wanavyuo waujue ukweli kwani utawaweka huru nao wataweza kuhoji.

ushauri wanu kwa wanavyuo hawa ni wao kujipanga na kukodi ukumbi mkubwa then wamwalike zitto ,slaa ,lissu na wengineo ili kujadili juu na mstakabali wa taifa lao hili linaliwa na mafisadi kila kukicha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom