Uongozi UDSM wasema hapana kwa Zitto Kuunguruma

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
3,750
Points
0

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
3,750 0
lakini chuo kikuu sio cha chama chochote cha siasa, sio cha ccm/tlp/chadema wala chama gani ? mbona mwenyekiti wa chama cha mapinduzi alienda kuongea nao pale iweje zitto ashindwe ?

hapa haki haitendeki !
 

Lawson

Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
69
Points
0

Lawson

Member
Joined Sep 25, 2007
69 0
Hiki chama cha Mafisadi(ccm) kimefika mbali hadi wasomi wananyimwa haki yao ya msingi? ila wamenifurahisha pale walipo simama nje ya geti na kuanza kuimba Mafisadi! Mafisadi! Mafisadi! kwa kila kiongozi aliyepita pale na VX yake, hiyo hatua inatia moyo maana hao ndio taifa letu la kesho wakisema hapana najua wanaweza kuhamasisha wengine vile vile, naomba wasilegeze kamba mwendo ni huo huo mpaka Kieleweke 2010.
Naomba mwenye list ya Mafisadi anitumie maana nataka kuprint nakuiweka kwenye ubao wa matangazo ya chuo.
 

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2007
Messages
3,071
Points
1,195

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2007
3,071 1,195
Lawson.
Ukitaka list ya Mafisadi nenda kweneye Website ya Ngurumo.
http://www.ngurumo.blogspot.com/

NA majina yao ni haya hapa.

1. Rais Jakaya Kikwete


2. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa


3. Waziri Mkuu Edward Lowassa


4. Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi


5. Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge


6. Waziri wa Viwanda na Biashara Basil Mramba


7. Gavana wa Benki Kuu (BoT) Daudi Balali


8. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Gray Mgonja


9. Katibu Mkuu Wizara ya Maji Patrick Rutabanzibwa


10. Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono
11. Mbunge wa Igunga Rostam Aziz (pichani juu).


Hivi Mzee Punch bado yuko hai hapo Mlimani?
 

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Messages
2,812
Points
1,250

Halisi

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2007
2,812 1,250
Nahisi kama LAANA YA MWALIMU NYERERE inaanza kuwashukia. Hii si kawaida hata kidogo.. Haiwezekani kwa watu wenye akili timamu kufanya wanayoyafanya. Hivi hata kama alishitukiza na hakukua na kibali chochote (japo kilikuwapo hata kama hakihitajiki kikatiba) ilihitaji saa ngapi na gharama kiasi gani kwa uongozi wa chuo kufanya mawasiliano na waandaaji na kuwashauri njia ya kufanya ili shughuli yao iendelee?

LAANA HIYOOOOO NAIONA NA CCM SASA INAELEKEA KUZIMU.
 

Mwawado

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2006
Messages
998
Points
195

Mwawado

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2006
998 195
Naona UDSM ni Tawi la chama Tawala,Prof Mukandala kwa nguvu zote ametetea maamuzi ya kutomruhusu Mh.Zitto kushiriki kwenye Mdahalo wa "Nafasi ya Mwanafunzi wa Elimu ya Juu Katika Maendeleo ya Jamii".Kuna jambo linafichwa hapa,Prof.Mukandala anamzuia Mh.Zitto kwa sababu anaona maswahiba wake wanapakwa Uchafu!!,Je?Prof ana uwezo wa kuzuia wimbi hili kubwa la mabadiliko? Endelea kusoma habari hiyo hapo chini,kuna mengi mapya humo!!

SUNDAY REPORTER
Daily News; Sunday,September 30, 2007 @00:04

The University of Dar es salaam (UDSM) yesterday cancelled a public lecture on the "The Role of Higher Learning Students in the Nation's Development" because the student organisers did not follow proper channels.

Vice Chancellor, Prof Rwekaza Mukandala, said the varsity' Political Science Association (DUPSA) the organiser's of the event, also had not specified the list of key speakers. The administration had nevertheless blessed the lecture under the spirit of academic freedom.

"We were surprised to find out at the eleventh hour that a legislator was apparently scheduled to be the main speaker. Now that was not proper because we are very keen on not using the university as a ground for partisan politics," said Prof Mukandala.

He was referring to Kigoma North legislator Mr. Zito Kabwe (Chadema), who apparently the organisers had lined as the main speaker. Prof Mukandala also said one of the organisations, Tanzania Students' Network Programme, said to be a co organiser of the event, was not even known to him!

Because the organisers had not been forthright in their application, they were allocated a smaller room, contrary to the large number of the students who turned for the lecture, which was in itself endangering the welfare of the students themselves, Pro Mukandala added.

Proper Mukandala said further that it was improper for the MP to sneak into the university as there was protocol involved in receiving dignitaries. The organisers were free to send fresh application, be specific and follow procedures, which includes routing their request through the faculty dean and their academic patron, Mr Mukandala explained.

"But we are very strict on academic independence and freedom. That is why two weeks also, we also advised the ruling CCM to find another venue for their meeting when they wanted to use one of our facilities here for a meeting on party polls," Prof Mukandala explained further.

However, Mr Kabwe denied to have sneaked into the campus, saying "I Live there." The MP was apparently referring to the fact that he was a co-parent of Ms J. Mgumia, an Assistant Lecturer in Sociology at the University.

Mr Kabwe has been banned from sitting in two sessions of parliament for refusing to apologise or retract his statement in the House, which Speaker, Samuel Sitta said he failed to substantiate. He will technically not be in parliament until next January.
 

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Kitu ambacho nina uhakika mara nyingi Watanzania tunapenda njia za mkato.

Zitto sasa ni kinara cha wapinga ufisadi. Serikali na watu ambao wanaunga mkono serikali wasingetaka apewe uwanja. Hivyo ni muhimu mno kwa watu wanaoandaa mikutano ya mheshimiwa kuhakikisha wanafuata sheria zote.

Hapa kuna watu wa UDSM, mimi ningetaka kujua ukitaka kuandaa hizo public lectures inakuwaje? Je hiyo form waliyojaza DUPSA ikoje?

Pamoja na Mukandala kuwa mfuasi mkubwa wa CCM lakini kama anachosema ni kweli basi kina make sense.

Kinachotakiwa ni uchunguzi wa kina kujua tatizo lilikuwa wapi ili huko mbele kuzuia matatizo kama hayo.

Ni rahisi sana kutokufuata sheria zote kama hotuba yenyewe haiwezi kuamsha mori na kuvuta watu wengi. Kwa jinsi nilivyoona wanafunzi kwenye video ilikuwa muhimu mno kuhakikisha ukumbi unatosha na pia kunakuwa na ulinzi wa kutosha, sio lazima polisi lakini hata walinzi wa chuo.

Kukitokea janga kwenye mikutano kama hiyo ni chuo ambacho kitabeba lawama zote.
 

Gigo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2006
Messages
455
Points
225

Gigo

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2006
455 225
Yaani Hata Chuo Kikuu!!!!???...Vyuo vikuu!!Dah! I'm sorry!!
Muachieni Zitto aendelee Ku- intataini-wananchi...

Hofu yenu Nini...Ukiona Mtu Kama Zitto ana wasumbua!! Je Vita dhidi Ya Umasikini MTAIWEZA?
 

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
However, Mr Kabwe denied to have sneaked into the campus, saying "I Live there." The MP was apparently referring to the fact that he was a co-parent of Ms J. Mgumia, an Assistant Lecturer in Sociology at the University.
Mmmhhhhh!!!! kwahiyo chuo inatakiwa kujua waheshimiwa wote wenye nyumba ndogo, wachumba hapo mlimani?

Bado mimi naamini tatizo lilikuwa ni mawasiliano mabaya kati ya waandaaji na uongozi wa chuo.

Katika uzoefu wangu na masuala ya Watanzania, mara nyingi hatufuati sheria zote na nimeona watu wengi wanalalamika kweli hata mahali ambapo ni makosa yako.

Ukiwa mwanaharakati inabidi uwe mwangalifu muda wote maana wanaotaka kukupinga wako wengi na wanasubiri tu ufanye makosa.

Ushauri wangu kwa CHADEMA, kuweni na mtu wa maana kwenye chama ambaye ndiye atakuwa ana organise mikutano yote ya Zitto kwa kushirikiana na wenyeji wa sehemu ambako anaenda kuhutubia. Mtu wa namna hiyo anaweza kushughulikia mambo kama usalama wa Zitto pamoja na raia wanaoenda kumsikiliza, kuhakikisha forms zote zimejazwa vizuri nk.

Huko majuu majanga kama ya watu wengi kuingia kwenye hall dogo na kufa yameshatokea sana na ndio maana kwasasa safety assessment lazima ifanywe. Ni kwa faida ya mheshimiwa Zitto mwenyewe kuhakisha mikutano yake haipati majanga.

Nimesoma kwa Michuzi kwamba jana kidogo kutokee janga la msongamano pale mnazi mmoja.
 

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2007
Messages
980
Points
1,225

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2007
980 1,225
Mtanzania,
bongo kunakitu kimoja ambacho akikowazi wa watanzania wote,kwa sababu kila siku hutasikia utaratibu haukufuatwa lakini ukiuliza ni utaratibu hupi huo hakuna anayekuja na jibu lakusema kuwa utaratibu wenyewe ndio huu.hata hizo form zenyewe huwezi kuziona,basi huu ndio umekuwa mtindo wa kila siku.tafauti na huku majuu ambapo hata ukitaka kusafiri tu unapewa taratibu zote kwa ajili ya kusafiri.pili hata kwenye internet
 

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Points
1,225

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 1,225
Mtanzania,
bongo kunakitu kimoja ambacho akikowazi wa watanzania wote,kwa sababu kila siku hutasikia utaratibu haukufuatwa lakini ukiuliza ni utaratibu hupi huo hakuna anayekuja na jibu lakusema kuwa utaratibu wenyewe ndio huu.hata hizo form zenyewe huwezi kuziona,basi huu ndio umekuwa mtindo wa kila siku.tafauti na huku majuu ambapo hata ukitaka kusafiri tu unapewa taratibu zote kwa ajili ya kusafiri.pili hata kwenye internet
Katibu Tarafa,

Nakubaliana na wewe. Ili ufuate utaratibu inabidi ujue utaratibu ukoje lakini mara nyingi sheria zetu na taratibu zingine ni vague. Mimi mwenyewe mara nyingi nimekumbana na taratibu mbovu ninavyoshughulikia mambo yangu TZ.

Ila kwasababu mimi nilisema sitatoa rushwa kwahiyo ninajitahidi kufuatilia kila kitu kama kilivyo mpaka inafika mahali wanakosa cha kusema na kwasababu wanajua na mimi ninajua haki zangu inabidi mwishoni wanipe huduma ninayotaka. Kuna vijana kule kwetu wananiita mjinga, kwanini kama nina uwezo wa kutumia shortcuts nisifanye hivyo?

Kwa mtu kama Zitto najua kabisa ingelikuwa miezi mitatu liyopita angepata kibali cha kuhutubia lakini kwa chati yake ya sasa basi watatumia kila njia kumkwamisha. Kinachotakiwa ni kwa yeye na watu wake kufuatilia kila kitu ili kutokuwapa nafasi hao watawala ya kuzima mikutano yake.

Hapo ni suala la kuamua kuungana nao au kuwapinga, ukiamua kuwapinga jiandae kwa usumbufu mbalimbali.
 

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2006
Messages
752
Points
195

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2006
752 195
"Ndio utaratibu wetu" haya maneno tumeyazoea na yametuingia sana akilini. Ukiuliza huo utaratibu uko wapi watakwambia "Yaani ni wewe tu peke yako hujui, lakini kila mtu hapa anajua". Hii ni desturi iliyoota mizizi katika jamii yetu.
Hii haitokani na bahati mbaya, ila ni muendelezo wa rushwa, kwani mahali ambapo utaratibu hauko kwenye maandishi, manake awaye yote anaweza kuupindisha kukidhi matakwa yake au ya mabwana zake waliomuweka mahali hapo.
Hoja ya DUPSA kutofuata utaratibu haina maana, kwani ilikuwaje wapewe ukumbi mdogo kama hawakufuata utaratibu? Kama hoja idadi ya wanafunzi ilikuwa wengi, kwanini hawakupewa Uhuru wa kwenda kwenye ukumbi au uwanja unaokidhi idadi ya wahudhuriaji? Kwa kifupi maelezo ya Mukandara yanakosa mantiki, kwani Zito alikuwa anakuja kutoa mhadhara wa kitaaluma na sio hotuba kwa niaba ya CHADEMA.
Anyway, huu ni mwanzo tujiandae kuona mengi mwaka huu. Nasikia NDANDA KOSOVO kashamaliza ziara na yupo Jijini.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Mkuuu Lunyungu alisema:-

Lunyungu
JF Senior Expert Member

Uongozi UDSM wasema hapana kwa Zitto Kuunguruma

Habari zilizo nifikia muda huu zinasema Ukumbi pale Chuo ujemaa pomoni na watu wana ngoja kusikia maneno mazito toka kwa Ziito. Uongozi wa Chuo umekaa chonjo unasema hapana Zitto hawezi kuunguruma pale Mlimani maana Serikali haitapenda. Hizi ndiyo habari zinazo jiri na sijui mwisho wake ni upi . Natoka naelekea kunako maeneo nikiwa na nazidi nitawauma sikio. Ila kwa sasa huu ndiyo uhalisia wenyewe.
Wanafunzi ni wengi sana ila Zitto katakiwa kutogusa maeneo hayo ambayo ni makao ya wasomi wetu .
My first response on the ishu ni hii hapa:-

Wakuu heshima mbele, ninajaribu ku-read between the lines sipati the juice bado on this ishu,

kwa hiyo labda ningeomba more facts, kuanzia kibali cha Mbunge kuruhusiwa kuongea hapo chuoni, na sheria zote zinazohusiana na suala zima la kiongozi yoyote kuruhusiwa na uongozi wa shule kuongea hapo shuleni,

It is a high time sasa kwenye JF tukufu tuache songi songi, na tuweke facts kwanza, ili tuzichambue ipasavyo,

However, shukrani kwa wale mnaojitahidi kutuhabarisha na yanyojiri huko shuleni!

Sasa here comes the facts:-


1. Because the student organisers did not follow proper channels.

2. The organiser's of the event, also had not specified the list of key speakers.

3. We were surprised to find out at the eleventh hour that a legislator was apparently scheduled to be the main speaker. Now that was not proper because we are very keen on not using the university as a ground for partisan politics


4. One of the organisations, Tanzania Students' Network Programme, said to be a co organiser of the event, was not even known to him!

5. Because the organisers had not been forthright in their application, they were allocated a smaller room, contrary to the large number of the students who turned for the lecture, which was in itself endangering the welfare of the students themselves

6. Proper Mukandala said further that it was improper for the MP to sneak into the university as there was protocol involved in receiving dignitaries.


7. The organisers were free to send fresh application, be specific and follow procedures, which includes routing their request through the faculty dean and their academic patron

8. But we are very strict on academic independence and freedom. That is why two weeks also, we also advised the ruling CCM to find another venue for their meeting when they wanted to use one of our facilities here for a meeting on party polls,"Anyways, ahsante sana kwa wale wote mliokuwa mstari wa mbele kutuhabarisha on this ishu, ustaarabu wenu na dilligence ni very appreciated, ila tu in the future kumbukeni kuwa kwenye huu uwanja mtukufu,

1. Kuna ishus ambazo zinahitaji dataz tu, halafu tunachambua wenyewe ukweli ulipo,

2. Kuna ishu kama hii ambayo inahitajika only FACTS!

Peace!
 

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2006
Messages
752
Points
195

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2006
752 195
Sasa here comes the facts:- [B said:
1. Because the student organisers did not follow proper channels.

2. The organiser’s of the event, also had not specified the list of key speakers.

3. We were surprised to find out at the eleventh hour that a legislator was apparently scheduled to be the main speaker. Now that was not proper because we are very keen on not using the university as a ground for partisan politics


4. One of the organisations, Tanzania Students’ Network Programme, said to be a co organiser of the event, was not even known to him!

5. Because the organisers had not been forthright in their application, they were allocated a smaller room, contrary to the large number of the students who turned for the lecture, which was in itself endangering the welfare of the students themselves

6. Proper Mukandala said further that it was improper for the MP to sneak into the university as there was protocol involved in receiving dignitaries.


7. The organisers were free to send fresh application, be specific and follow procedures, which includes routing their request through the faculty dean and their academic patron

8. But we are very strict on academic independence and freedom. That is why two weeks also, we also advised the ruling CCM to find another venue for their meeting when they wanted to use one of our facilities here for a meeting on party polls,”[/B]


Anyways, ahsante sana kwa wale wote mliokuwa mstari wa mbele kutuhabarisha on this ishu, ustaarabu wenu na dilligence ni very appreciated, ila tu in the future kumbukeni kuwa kwenye huu uwanja mtukufu,

1. Kuna ishus ambazo zinahitaji dataz tu, halafu tunachambua wenyewe ukweli ulipo,

2. Kuna ishu kama hii ambayo inahitajika only FACTS!

Peace!
Mzee FM pokea saluti yangu kamanda,
Nashukuru kwa facts ulizotoa, lakini tatizo hapa linaonekana kuwa kuna zaidi ya hizo facts. Kwani Mukandara anashindwa kujibu kuwa kwanini walipewa ukumbi mdogo wakati wanafunzi hawakufuata utaratibu, mmoja wa waandaji hatambuliki, na waandaji hawakuwatoa majina ya wahutubu?

Hapa naona kuna tatizo kama sio shinikizo. Mukandara nadhani anachojaribu kufanyani visingizio vya kuhalalisha udhalimu wake.
 

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,777
Points
1,195

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,777 1,195
Mzee FM pokea saluti yangu kamanda,
Nashukuru kwa facts ulizotoa, lakini tatizo hapa linaonekana kuwa kuna zaidi ya hizo facts. Kwani Mukandara anashindwa kujibu kuwa kwanini walipewa ukumbi mdogo wakati wanafunzi hawakufuata utaratibu, mmoja wa waandaji hatambuliki, na waandaji hawakuwatoa majina ya wahutubu?

Hapa naona kuna tatizo kama sio shinikizo. Mukandara nadhani anachojaribu kufanyani visingizio vya kuhalalisha udhalimu wake.
Tatizo lipo,

Ilikuwaje wakatoa kibali bila kujua mtoa mada? wala Muandaaji mkuu? Bila hata kujua ama kukadiria idadi ya wahusika? kwavyovote vile muombaji ukumbi (muandaaji) lazima ana specify ukumbi gani anao uhitaji kulingana na idadi ya washiriki anao wategemea!.

Naamini muandaaji alijua wazi watakuwa wengi washiriki ndo maana aliomba Nkuruma ambayo mwanzoni walipewa kabla ya zengwe kuanza ingilia!

Maelezo haya ya Mkandala ni sawa na majibu ya Karamagi aliyo yatoa Bungeni wakayatumia kumhukumu Zitto na kumfungia, BADO kuna mambo makubwa yaliyo jifunika katika kumkatalia Zitto zaidi ya kutofata taratibu kama anavo dai VC.
 

Forum statistics

Threads 1,379,949
Members 525,639
Posts 33,761,999
Top