Uongozi UDSM wasema hapana kwa Zitto Kuunguruma

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
Habari zilizo nifikia muda huu zinasema Ukumbi pale Chuo ujemaa pomoni na watu wana ngoja kusikia maneno mazito toka kwa Ziito. Uongozi wa Chuo umekaa chonjo unasema hapana Zitto hawezi kuunguruma pale Mlimani maana Serikali haitapenda. Hizi ndiyo habari zinazo jiri na sijui mwisho wake ni upi . Natoka naelekea kunako maeneo nikiwa na nazidi nitawauma sikio. Ila kwa sasa huu ndiyo uhalisia wenyewe.

Wanafunzi ni wengi sana ila Zitto katakiwa kutogusa maeneo hayo ambayo ni makao ya wasomi wetu .
 
sasa itakuwaje tena? inamaana hakufanya taratibu za kiutawala? embu endelea kutuhabarieha
 
Ni kheri wamruhusu tuu otherwise yanaweza zuka mengine.
Namshauri apate kibari rasmi ili wanaomtakia mabaya wasije wakapata sababu.
 
Nilijua tu kwamba hilo lingeweza kutokea. Unadhani akina Mkandala wako upande gani? Hawawezi kumpa nafasi huyo jamaa aende kuunguruma pale na hasa kwa kuwa walishaona moto umewaka vibaya na ukimwagwa kwa wasomi ndiyo kwanza watakuwa wanaongeza petroli kwenye moto. Kazi kwake Mkandala, atajua aidha asuke ama anyoe. Zama zile alikuwa akijifanya yuko neutral na REDET yake, sasa naona amejiweka wazi zaidi. Muhimu kwa Zitto ilikuwa ni kuomba kibari cha kuongea na wanafunzi hapo kwenye Ukumbi wa Nkrumah, je, alifanya hivyo? Au kama alialikwa hao waliomwalika walifanya hiyo mipango? Kama hayo yalifanyika basi uongozi wa chuo umejiweka wazi kwamba wao ni watu walio upande wa serikali ama upande wa CCM!
 
Muacheni Aongee weeeeeee!! hakuna Tatizo!!
Ila Zito Kua Makini-!!sio kwamba unaweza sana...unajitahidi!! Muda..
Hao wanao sema serikali haipendi-waongo!! kwani ZITTO sio sehemu ya serikali?
 
sasa itakuwaje tena? inamaana hakufanya taratibu za kiutawala? embu endelea kutuhabarieha
kaka sasikia taratibu zote zilifuatwa ila ndo hivyo tena zengwe la wafisadi inawezekana ndo lipo kazini. kwakweli nasikia ukumbi ulianza kujaa toka saa mbili asubuhi na mpaka sasa watu nyomi wako nje ya ukumbi wa muhadhara wa nyerere(theater ii).

hisia za wanafunzi wengi ni kuwa walinyimwa kutumia nkhuruma hall kwa makusudi kabisa ili kuzuia idadi kubwa ya watu waliojitokeza. wanaona kama njama za mafisadi zinafanikiwa na wengi wanasema walisha anticipate mizengwe ili zito asingurume.

hisia nyingine ni kuwa vice chancellor ni mtu wa karibu sana na muungwana so by any means hawezi kutoa ukumbi kwa watu wanaomlima madongo swahiba wake. kuna madai kuwa kabla jamaa hajaula u-vc alikuwa mshauri wa raisi mambo ya jamii. nawengine wanasema kuwa hata slogan ya ari mpya nguvu mpya na kasi mp[ya ni yake. so by any means kutikishwa kwa serikali ni kutikiswa kwa vc moja kwa moja na hawezi kuruhusu hilo kutokea.

nimetaarifiwa tena kuwa watu wameanza kuchachamaa kuhusu mizengwe ya kukwamisha public talk. kwa sasa ni hayo tu nikidaka mengine nitawaleteeni.
 
Kazi ipo!Yaani Uongozi wa UDSM wameanza mizengwe ya wanasiasa. Poor prof Mukandara, inaonekana huyu bwana amepata nafasi ya ukuu wa chuo kama takrima.
 
Kazi ipo!Yaani Uongozi wa UDSM wameanza mizengwe ya wanasiasa. Poor prof Mukandara, inaonekana huyu bwana amepata nafasi ya ukuu wa chuo kama takrima.

kaka hilo lilisha semwa sana na walimu pale mlimani walili debate sana wakati wa vuguvugu la kumpata VC wa kumrithi Prof. luhanga! watu wandani pale wanasema kwa kujiamini kabisa kuwa kati ya watu wa karibu na mafundi wa kuu wa wanamtandao jamaa ndie chief artitecture wa mtandao. kuna habari vijana walikuwa wananiambia pia kuwa anabenzi moja matata ambalo wazushi na wazee wa tetesi walikuwa wanasema linatoka state house kama hongera kwa kazi nzuri ya kuwanoa wanamtandao kufikia ushindi wa kishindo.

msisahau kuwa pia huyu ndie aliekuwa mkuu wa kitengo cha REDET kilicho kuwa kinafanya uchunguzi na kusema muungwana atapita kwa kishindo. hivyo wanafunzi wengi walisha hisi kuwa siasa lazima zitaingizwa kwenye hili nadhani na hilo ndilo linalotokea.
 
kuna habari vijana walikuwa wananiambia pia kuwa anabenzi moja matata ambalo wazushi na wazee wa tetesi walikuwa wanasema linatoka state house kama hongera kwa kazi nzuri ya kuwanoa wanamtandao kufikia ushindi wa kishindo.

Humble,
Kuweka sawa mambo, ni kweli Benzi ya jamaa inatisha hadi alisha fuatwa na PCCB kumhoji!, Ila walipo fika waligwaya wenyewe kwani jamaa aliwaonyesha Bank stement iliyo waacha midomo wazi na macho yamewatumbuka, na kwamba ilikuwa ikionyesha jamaa hajawahi kugusa mshahara wake unaoingia bank kwa miongo kadhaa!

Lakini kilicho mpa hela kama Nyasi huyo Jamaa ni hiyo PROJECT ya REDET! siyo siri jamaa ana FWEZA!! ila haija toka Ikulu, japo uswahiba wao ni mkubwa tu na Muungwana, kwahiyo kumlinda hilo halina ubishi, na ndo maana hata wakati ule alipowafukuza wanafunzi na kufunga chuo bila sababu za msingi ilkuwa ni kumlinda swahiba tu!

Ila kwa hili, nadhani bora wangemruhusu tu Zitto aongee, kwani kumzuia naona ndo watazidi kuamsha MORI!!
 
Kuna habari kwambsa mageti yote yamefungwa na wanafunzi hadi zitto aruhusiwe kwenda.stay tuned......

Hakuna gari kuingia wala kutoka muda huu....
 
Zitto ninamuona yuko online ... Mh. naomba tuambie kulikoni huko Mlimani? VC anaogopa sumu utakayomwaga????
 
mimepata news sasa kama nusu saa iliyopita!mimeongea na mmoja wawaandaaji akanieeleza zengwa la kukataliwa zito. jaama anasema waliomba venue ya nkruma kwa kufuata taratibu zote za kiutawala na walikubaliwa na ofisi husika bila kinyongo! ila ilipofika siku ya alhamisi wakataarifiwa kuwa hawataweza kutumia ukumbi wa nkruma na badala yake watumie ukumbi wa nyerere theater hall II ambao ni mdogo mno ukilinganisha na muutikia wa watu.

basi kwa kuwa siku zilikuwa zimesalia chache na resourses za kutoa matangazo mapya hawakuwa nayo ilibidi watangaziane kwa midomo tu kuwa Public talk imehamia theater II. lakini wakati wakifanya hivyo wakapigiwa simu siku ya ijumaa wakiambiwa kuwa hawataweza kufanya mjadala huo wa uma. basi kwakuwa hawakuwa na muda wa kutosha kuwafahamisha wanafunzi hawakuweza kuahirisha mjadala huo.

wakati wao(viongozi wa PUPSA na student networking..... sijasikia vizuri jina la waandaaji) wakifikiria kuu ahirisha wanafunzi walisha fika asubuhi na mapema katika venue husika na kuchukua nafasi tayari kumsikiliza zitto na kujadili juu ya mada iliyo pangwa. kwakuwa wafagizi walikuwa hawajui lolote wao walifungua ukumbi na wanafunzi wakajaa ndani na hapo ndo janja ya wakuu wa chuo ilipo zidiwa na nguvu ya umma wakashindwa kuwatoa wanafunzi waliokuwa wamejazana ndani ya ukumbi.

wakati huu huo ilionekana kama wakuu wa chuo walitoa agizo kwa walinzi wa mageti yote ya chuo kuto kumruhusu zitto kabwe kuingia katika maeneo ya chuo(kwa wale ambao hamkufika huko kitambo!sikuhizi chuo kimezungukwa na mageti pale chuo cha maji,Aridhi na njia ya kwenda msewe na changanyikeni) so muheshimiwa zitto alipo fika pale akapambana na maaskari wa nao itwa AUXILLIARY POLICE wa chuo walio mzuia pale geti la chuo cha ardhi.

mpaka napopwea habari hii inasemekana zitto amewaahidi kuwa nataingia ndani na mkuu wa chuo aende kutoa maelezo kwa nini yeye zitto asiruhusiwe kufika maeneo ya chuo nasikia kama wataendelea kumzuia ataingia kwa nguvu! sasa sijui nini kitatokea

i hope wakuu wa chuo hawatajiingiza kwenye mitego ya siasa maana inaweza ikasababisha tafrani wakati wowote. lets wait and see
 
Hivi hii ni laana ama alama za nyakati...

Waswahili walishasema kuwa kifo cha nyani miti yote huteleza nadahni huu ni ushuhuda mwengine.

Kuhusu Mukandala nina wasiwasi kuwa mnamsulubu bila ushahidi wa kutosha. Nina uhakika hii ni kazi ya Public Relation Oficer wa UDSM Mr Seule ambaye miaka yote ya Zitto mlimani alikuwa ndio mpika majungu mkuu dhidi yake na wengine. Seule ndiyo tatizo kubwa pale na ndio aliyekuwa akimtumia sana mjasiriamali Prof ....kulipukakuwasimamisha kina Zitto chuo kila mara wanafunzi wanapogoma. Kwake yeye haikuwa inawezekana kuwe na mgomo ama harakati zozote za kimapinduzi chuoni hapo bila ya uhusika wa Zitto na wenzake. Na kama isingekuwa imani ya Prof Luhanga kwa Zitto basi ni wazi Seule angelifanikiwa na mkakati wake wa kummaliza Zitto tangia enzi hizo. Kwa taarifa ni kuwa huwezi kuwa PRO mlimani bila ya kuwa na uhusiano maalum na nyumba kuu.

Kuhusu Mukandala naona mnamnyanyua kuliko ukweli wenyewe. Mukandala hajawahi kuwa mwanamtandao na wala swahiba wa JK. Mukandala alipelekwa kule miaka ya mwisho ya kampeni za kuelekea Chimwaga na mwanafunzi wake mmoja ambaye alifanikiwa kujiweka karibu sana na JK mara alipomaliza masomo yake pale mlimani. Mukandala alikuwa kama kwa kutumia tafsida "contractor" wa kufanikisha na kuhalalisha ushindi wa JK na ndipo alipopewa jukumu la kusoma jamii na kutoa utaalamu wake katika njia za kucheza na akili za jamii yaani "political psycholgist" kwa kutumia hiyo cheo cha mshauri wa masuala ya kijamii.

Baadaye ndipo alipopewa baraka za kugombea kuwa VC na nafasi hii ilikuja baada ya UDASA ya Chachage, DARUSO na Muungano wa wafanyakazi wafanyakazi hao mlimani(RAAWU) kufanikiwa kuwamaliza kundi la kina Prof Mshana, Prof Nkunya na Prof Maboko ambao walijiona kuwa wao ndio warithi halali wa nafasi ya Prof Luhanga. Wasijue kuwa Luhanga aliapa kuwa hamna kati yao atakayechukuwa nafasi hiyo.

Kwa hiyo ingawa Mukandala alisaidia kwa kiasi fulani ushindi wa JK lakini kamwe yeye sio mwanamtandao wa karibu kama wengi wanavyomrate.
 
Tanzania njema,
Nakubaliana na wewe kwamba Mkandala si mtandao ila ni kweli ni swahiba wa JK

Aliye kuwa akitaka nafasi ya Luhanga kwa garama yoyote ile alikuwa Mshana, wakati huo alikuwa ndo chief Admin. na hadi akawa anapachika vigezo vya VC ambavyo ni yeye tu aliye navyo hadi akawa ameteua kampuni ya kuendesha mchujo, ndo kina Marehemu Chachage walipo ngamua hiyo na kuisambaratisha kwa nguvu zote!. Na kuingiza mtindo wa 'search committee' badala ya mtu kuomba/kuwania nafasi husika. Nkunya na Maboko hawakuwa katika kundi hilo!
 
tanzania njema nadhani wewe ndio una mu-underrate mukandala katika siasa za wanamtandao na uswahiba wake na muungwana. haya yaliongelewa sana pale UDSM wakati wa mchakato wa kumpata mridhi wa Luhanga. siwezi kusema kwa hakikika kama DARUSO,RAAWU na UDASA walikuwa wanamuunga MKANDALA mkono moja kwa moja. ila ukweli ni kuwa katika hili kila mmoja na hasa wahadhiri walikuwa wana maoni yao huku wengine wakipinga na wengine wakimsupport. na zaidi kuli kuwa na kama race between COET(wahandisi) na MANGUINE(social sciences). hili nalijua kwa hakika! haya yalikuwa ndani ya jumuiya ya wasomi wa mlimani na ninadhani sitatizo watu kupinga au kushabikia mtu flani kuchukua cheo

ila hili la kuwa mtu wa karibu au la! ndilo hasa linaelezee sababu has ya yeyekuwa muhusika wa kuzuiwa kabwe kufika chuo kuhudhuria public talk.
ni kweli kuwa Mukandala hausiki na utoaji wa kibali ukijaribu kuangalia mgawanyiko wa madaraka pale mlimani. anae husika moja kwa moja ni deputy vice chancellor planning finance and administration(DVC-PFA)ambaye barua zote zinaelekezwa kwake na yeye idhinisha kupitia ofice ya PAO(public relation officer). sasa basi kwa jinsi sakata hili lilivyo inaonekana ofisi ya PAO ilifanya kazi yake vizuri na kuidhinisha ukumbi wa nkuruma ila baada ya mkuu kuona imekuwa hivyo ndo wakabadilishiwa na then wakanyimwa kabisa. hivyo sioni kama PAO anakosa lolote katika hili.

na zaidi inasenekana MUKANDALA mwenyewe ndio ameonekana akiwagombeza wafagizi kwa kufungua ukumbi. sasa kwa nini watu wasiconnect rumours za uana mtandao wake na zoezi alilo lifanya leo? ningekuwa na nafasi tungendelea kujadili hili mpaka unge kubali mwenyewe kuwa huyu ni achitecture wa mtandao! it is unfortunate i have only few hrs kuja humu forum per month
 
Zitto kama raia mwingine ana haki ya kukutana na watanzania wenzie. Uongozi wa chuo unachofanya hapa ni kukiuka katiba, hivyo wanawajibika moja kwa moja na uvunjifu wa amani utakaotokea mahali hapo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom