Uongozi siyo haki ya kiongozi bali ni haki ya wale anaowaongoza

BenElohimy

Senior Member
Sep 21, 2021
181
222
Natumai wote wana JF mko salama kabisa.

Ninapenda kuwasilisha kwako kwamba katika hii sayari ya dunia ni ngumu sana kumkuta kiongozi ambaye yuko tayari kwa ajili ya wengine.

Viongozi wengi hutumia nafasi walizonazo ili kujinufaisha wao, kujilinda wao au kujiwekea kinga kwa yote wanayoyafanya.

Nia za viongozi wengi imekuwa siyo tena mtu kuwa kiongozi ili kuwaongoza wengine lakini imegeuka na kuwa panga lake la kuwachinjia watu, kuwanyinya watu, kuwaonea watu.

Mwaka fulani nikiwa naenda kufanya usahili kwa ajili ya kujiunga na chuo kikuu mojawapo hapa Tanzania, kati ya wale waliokuwa wanafanyisha watu usahili, akanifokea baada ya mimi kuonekana kuna kitu hakipo, hakuweza kunielekeza lakini alinifokea," Ndipo nikamwambia uongozi siyo yako, bali ni haki ya yule unayemwongoza"

Maneno yale niliyasema wala mimi sikujua kama pembeni yangu kulikuwa na mkuu wa idara ya takwimu, akaniita ofsini kwake, yaliyotokea baadaye ni kwamba akafanyika rafiki yangu mpaka leo.

Jana nikiwa natoka kazini, kuna gari ikawa imepaki katikati ya barabara na mwenye gari akawa anachati kwenye simu, lakini kuangalia vizuri kwenye kiti cha dereva kaweka uniform ya JWTZ, huyu naye anautumia uongozi wake vibaya, serikali imemwamini kuwa mmoja wa JWTZ lakini yeye anafanya kinyume na kuvunja sheria, tusitumia uongozi wetu vibaya.

Mwisho kabisa maisha yana pande mbili.
 
Back
Top Bottom