Uongozi ni hekima na busara, Rais Samia ana sifa zote mbili

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Uongozi sio misuli au kubobea sana kwenye fani fulani. Uongozi hauhusiani na kunyanyua vitu vizito au kufanya vitu mwenyewe mwenyewe, bali uwezo wa kuunganisha watu na kuwasaidia kufikia malengo ya pamoja.

Dunia haina tatizo la wataalam wa vitu mbalimbali, bali ina tatizo kubwa la uhaba wa watu wenye hekma na busara ambao kimsingi ndio viongozi wa kweli. Watu hawa ni adimu sana na akipatikana mmoja kwenye jamii fulani, Mungu anakuwa ameipa jamii hiyo zawadi kubwa.

Rais Samia ana hekma na busara kwa kiwango kinachotia moyo. Kwa vitu hivyo viwili pekee, Mungu kampa hazina kubwa ambayo sasa ni faida kwa watanzania wote.

Kwa hekma na busara hiyo na kwa baraka za Mungu, haki na uadilifu vitatamalaki nchini. Hali ya kusimamia haki na uadilifu miongoni mwa makundi yote itapelekea upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania katika kuijenga nchi yetu.

Mazingira hayo kwa ujumla wake, yatatupelekea kuwa na mshikamano na upendo baina ya makundi yote na hivyo kuweza kuwa na nguvu moja kupambana na matatizo yanayotukabili kama taifa na kunufaika na mafanikio tuyapatayo kwa pamoja.

Kwa ujumla kwa kuwa na kiongozi mwenye hekima na busara ni zawadi kubwa toka kwa Mungu na matokeo yake katika hatua ya juu kabisa ni kuwa na jamii inayoishi katika misingi ya haki na jamii inayoishi katika misingi ya haki huwa na furaha daima, na ukiweza kuishi maisha yenye furaha, hayo ndio mafanikio makubwa kwenye dunia. Mungu akupe nini tena?

La msingi tu ni kila mtu kujitahidi kumpa ushirikiano kulingana na uwezo na mazingira yake kwani hata kiongozi awe mzuri vipi, hawezi kufanikisha mambo bila ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa watu wema.

Ikimbukwe mafanikio ya kiongozi wa watu yamejificha kwenye namna anavyosimamia haki na kuzima au angalau kupunguza dhulma zisitokee kwa watu anaowaongoza na nyenzo kuu za kufanikisha hayo ni hekma na busara, nyenzo ambazo niwachache sana miongoni mwetu wamejaaliwa kuwa nazo.

Kuhusu ishu nyingine kama uchumi hako hakuna wasiwasi maana nchi hii ina wataalamu wa fani nyingi wakutosha kwa hiyo tutaenda vizuri tu.
 
Samia suluhu Hassan ndiye Rais wa jmt na Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. Hivyo kama kuna yeyote alikuwa hajui na ajue hivyo kuanzia sasa!
 
Hata afanye vipi, hawez kuwa Magufuli, Magufuli aliwapiga chini wachumi na theory zao, akaenda kivyake na mambo yakaenda faster. Kiongoz ukienda kwa misuli hata wasaidiz wako wanaenda kwa misuli.
 
Hata afanye vipi, hawez kuwa Magufuli, Magufuli aliwapiga chini wachumi na theory zao, akaenda kivyake na mambo yakaenda faster.Kiongoz ukienda kwa misuli hata wasaidiz wako wanaenda kwa misuli.
Kwani Lazima afanye Kama Magufuli?
Atafanya mbinu zake anazojua,nae anajua atafanyaje.
Na sio lazima yaende fasta,maendeleo Kama yapo yapo tu.
 
Hata afanye vipi, hawez kuwa Magufuli, Magufuli aliwapiga chini wachumi na theory zao, akaenda kivyake na mambo yakaenda faster.Kiongoz ukienda kwa misuli hata wasaidiz wako wanaenda kwa misuli.
Hakuna namna ambayo mtu A anaweza kuwa mtu B. Hata ingewezekana haipaswi kuwa hivyo kwa kuwa mtu akiamua kuwa mtu mwingine anakuwa ameamua kujibadili kuwa kama robot. Kila mtu ameumbwa yeye kama yeye na anapaswa kuwa yeye kama yeye. Hata wewe unapaswa kuwa kama wewe na sio kama mtu mwingine.

Kuhusu uchumi, unatakiwa kufahamu kuwa uchumi ni sehemu ndogo tu (japo muhimu) ya mafanikio ya mwanadamu. Yapo maeneo mengine muhimu ambayo usipofanikiwa kwayo, bado unakuwa kwenye hali ambayo si nzuri.

Mafanikio katika upana wake ni kuweza kujenga jamii yenye furaha na mtangamano. Kwa hiyo inabidi kubalance vitu vingi ili kufanikisha hilo.
 
Kwani Lazima afanye Kama Magufuli?
Atafanya mbinu zake anazojua,nae anajua atafanyaje.
Na sio lazima yaende fasta,maendeleo Kama yapo yapo tu.
Halafu sijui kwa nini watu wengi huangalia maendeleo kwa kigezo kimoja tu cha 'uchumi' bila kuelewa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuangalia gari kama 'gear box' tu bila kuelewa gari ni mfumo mzima

Halafu mwenye mtizamo huo hoja yake anayoitoa tu ni kuwa' hivi gari bila gear box kuna gari hapo'? Ni changamoto kidogo ya uelewa nadhani.
 
Back
Top Bottom