Uongozi na timu mpya ccm ni tumaini jipya au janga jipya


M

Mghaka

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
320
Points
195
Age
57
M

Mghaka

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
320 195
Ujanja katika uongozi ni kukataa kushughulikia mambo ambayo unajua utashindwa na ushujaa katika uongozi ni kufanya ambayo umma unazani huenda hayawezekani. Busara katika siasa ni kutumia akili na mikono ya watu wengine kufanya yale ambayo watu wanaona hayawezekani na kushikiria fimbo ya kuongoza kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unaendana na matakwa ya umma bila athari kubwa katika kufikia malengo yake.

Baada ya kuwa na timu ambaye haikumuelewa kwa kipindi kirefu J.K. ameamua kutumia wale kwa kipindi kirefu walihisiwa kuwa hawakuivana ili afanikishe kufikia malengo yake. Kwa kweli kwa hili wale watu ambao kwa kipindi kirefu walikuwa na busara za JK ni vizuri wakatambua kuwa kiongozi huyu yuko sayari nyingine kisiasa na wanamsaidia kwa nyakati fulani wamekawia kumuelewa na wanapojaribu kumuelewa huwa wamechelewa kiasi kuwa au mabo yanakuwa yameharibika au hayumkiniki tena

Watanzania lazima waelewe kuwa kazi ya JK sasa ni kuhakikisha kuwa anaendelea kuwa mhimili katika siasa za Tanzania katika kipindi kingine cha miaka kumi na ili kufanikiwa ni lazima ahakikishe kuwa anafanyakazi na maadui zake wa zamani ambao wanahasira isiyo kifani na timu yake. Kwa mtazamo rahisi ni kuwa maadui hawa wanaona hawawezi kufika mwisho wao bila JK nae anaona hawezi kufikia malengo yake akiwa na timu ya 95. Kazi kwenu!


Mchanyato huu wa kisiasa ni kweli waweza kuleta radha bora kwa watanzania? hakuna ajuaye ngoja tusubiri. Lakini JK ameanza ngoja tuone wale ambao wanamashaka ni juhudi hizi za JK na ambao kwa makusudi wanafanya hima kwenda kinyume na matakwa ili wafanikishe yale yao bila ridhaa ya wenye CCM yao kama kweli wapo kama tulivoona wanajinadi Kizota na wengine wakadirika kuwapatia wapinzani wao hawa majina ya fedha na kuwafananisha na wahaini. Sisi yetu macho, si Mangula wala Kinana ambao wanalo lao dogo la kufanya hapa wajiandae kimbunga chaja juu yao kuzika yale matarajio yao. Sioni tahadhari kama inatosheleza kuiokoa meli ya Mangula isizame na nahisi wakati ukifika rubani wa meli hiyo atawaruka walioanzisha kazi ya kupingana na kimbunga hicho kama alivonyamizia madudu wakati wa uchaguzi wa chama. Kazi kweli kweli na tutashuhudia mengi
 
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
5,562
Points
1,195
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
5,562 1,195
Meghji : EPA
Kinana : Alshabaab
 
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
3,520
Points
2,000
Age
38
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
3,520 2,000
Ni janga jipya! Kinana-magendo, megji+mangula+nchemba-epa,migiro+khatibu+nepi-dhaifu
 

Forum statistics

Threads 1,284,356
Members 494,038
Posts 30,822,629
Top