Uongozi na Posho/Mshahara: Ukweli na Uwazi

Kwa tiketi ya Chadema kamanda.

Ndugu Diwani nimefurahishwa na plan yako, maana madiwani na wabunge wa ukweli wa CHADEMA, mjitofautishe kabisa kiutendaji na wale wa CCM. Ulicho amua ni sawa, ila ukigawa hizo pesa mashuleni, utakuwa umewapelekea ulaji walimu. Njia nzuri ni kupeleka vitu, kama ni chakula, madawati, vitabu, kalamu nk.

Na wasiwasi na kumkabidhi mtu pesa, labda ufuatilie matumizi yake kwa karibu maana unaweza kumlaumu mtu kumbe wewe ndo ulikosea.
 
Mawazo yako ni ya Kimaskini:-

Kwanza unafikiria kwenye matumizi ya kidogo ulichonacho badala ya kufikiria kidogo ulichonacho utumie kuzalisha zaidi!
Na msimamo wa wengi hapa uko hivyo hivyo yaania kupigiwa makofi kwa ku-embrace umasikini.... ndio maana mtoto wa mkulima alivyosema ana nyumba mbili alipendwa sana kwa mataifa mengine na mimi mwenyewe... that was disqualification ya kutompa u-PM. Kwa kuwa tunataka kiongozi wa kufanya waTanzania wawe na uwezo... sio wawe wa kupewa samaki badala ya ndoana.... so plan yako sio effective lakini kisiasa utasifiwa sana... but haina tija... use those little money to make more money.

Hii hapa chini tu ndio yenye akili, the rest is short plans for publicity:-
2. Posho za vikao vya Kamati ya Elimu naanda utaratibu zishindaniwe na watapewa wanafunzi watatu wa kiume na watatu wa kike watakao fanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya muhula kwa kata.

Mwisho:
Wakati unakampeni aidha ulitangaza vipaumbele vyako au at least mpaka sasa umeona vipaumbele kwenye kata yako baada ya kuwa na muda wa kutosha wa kujua au kuzungukia kata yako... is quite WRONG kututumia sisi ambao sio wapiga kura wako kupanga vipaumbele vya wananchi/wapiga kura wako (aidha unaona wao mazuzu au ....)... please be serious na mamlaka uliyopewa na wananchi.... acha longo longo za kwenye mtandao au sehemu zingine... you remember yaliyomtokea mbunge aliyekuwa anaitwa Seleli akiwa anapendwa na watu nje ya jimbo lake... lakini jimboni kwake eeeh?
 
Kutuambia vikao viko vinne kwa mwaka nachelea kuliamini hilo labda kwa mwezi. Vile vile hukusema hivyo vikao vinne vinakuwa vya siku ngapi? Sasa wakati wa kampeni mnakamiana hivyo kwa ajili ya Shs 120,000 au kwenda kujipa tenda na kujigawia viwanja?

Mkuu,vikao vya kamati za kudumu za Halmashauri hufanyika kwa robo,ambapo mwaka una robo nne,na huwa hufanyika kwa siku moja otherwise kuwe na dharura.Kikao cha kamati ya Fedha hufanyika kila mwezi,kwa hiyo Mh.diwani kama ni mjumbe wa kamati ya huduma za jamii,yuko sahihi,naomba niamini.
 
Back
Top Bottom