Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
WanaJF,
Kwa sababu mimi sio Mbunge nitawasilisha kwenu kile ninachopata kama Diwani.
Ili nichangie kwa uhuru na niweze kutoa mawazo yangu bila kung'ata maneno ni vyema nikaweka wazi kile ninachopata kama Diwani.
Hii itasaidia pia kwa WanaJF kujua na kuchambua tuko wapi, tunaenda wapi na tutafika lini.
Mimi kama Diwani nalipwa posho (sio mshahara) kwa mwezi shilingi laki moja na ishirini (Tzs 120,000).
Posho ya Kikao cha Halmashauri ni shilingi elfu hamsini (Tzs 50,000) kwa kikao. Vikao vinatakiwa angalau vinne kwa mwaka.
Posho ya Vikao vya Kamati (Kamati ya Elimu, Afya na Maji) ni shilingi elfu hamsini (Tzs 50,000). Vikao angalau vinne kwa mwaka.
Posho ya vikao vya Kamati ya ALAT Mkoa ni shilingi elfu sitini na tano (Tzs 65,000) kwa kikao.
Hicho ndicho ninachopata kama Diwani.
Nilichoamua kwa roho nyeupe kabisa ni kama ifuatavyo;
1. Posho ya kila mwezi yote igawanywe kwa shule za msingi kuchangia chakula cha mchana cha watoto. Shule ziko 11. Nimemuelekeza Afisa Mtendaji kila mwezi azichukue na kuzigawanya. Nitazisimamia zifike hata kama ni kidogo.
2. Posho za vikao vya Kamati ya Elimu naanda utaratibu zishindaniwe na watapewa wanafunzi watatu wa kiume na watatu wa kike watakao fanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya muhula kwa kata.
3. Posho za vikao vya Halmashauri nitatumia kuwanunulia soda na biscuits wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ambayo Diwani ndie Mwenyekiti wake. Kamati hii haina fungu lolote na ndio chombo ambacho kinaandaa miradi na mipango yote ya maendeleo ya kata.
4. Posho ya ALAT itachangia mafuta yangu ya gari kuzunguka kwenye kata kuangalia shughuli za maendeleo nk.
Changamoto kwa WanaJF, je haya ambayo nimeamua kuyafanya na kuyasimamia yana faida gani kwa jamii? Je ni njia sahihi?
Si madiwani wote wanaweza kupishana na posho zao. Wengi wanazihitaji kujikimu. Wao ndio 'watendaji' wakuu katika kuhamasisha na kusimamia shughuli za maendeleo.
Nielekezeni, nirekebisheni pale ambapo sipo sahihi. Pale ambapo ni pakuboreshwa nisaidiwe. Sioni aibu au fedheha kama kiongozi kuomba msaada na ushauri.
Naamini ni muda wa viongozi kubadilika na kuanza kutenda si kwa maneno bali vitendo. Sote tushiriki kuleta maendeleo yetu hata kwa kushauri na kuelekeza.