Uongozi Mpya wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

Mawazo ya Philemon Mikael kuwa wachaga wawapo sehemu yoyote hufanya kila wafanyacho kwa juhudi tofauti na makabila mengine ni ya kibaguzi na ni sumu kwa huo uchaga!
 
Mawazo ya Philemon Mikael kuwa wachaga wawapo sehemu yoyote hufanya kila wafanyacho kwa juhudi tofauti na makabila mengine ni ya kibaguzi na ni sumu kwa huo uchaga!

Elezea zaidi kwa kirefu mkuu. Tafadhali... akhsante.
 
Waberoya said:
Waberoya said:
baba, hayo mawazo yako wala usifikiri kila mtu anawaza kama wewe!
Waberoya said:
Kwangu mimi Zito mpiganaji na kiongozi mzuri, andika weeeeeeeee jaza hata thread zote kwangu mimi ni hivyo hiyo haitabadilika; sijamjua leo wala jana!

Pili, weka dhamana au insuarance kuwa wengine woote wapiganaji hawawezi kuhudhiwa na kubadilika; ama sivyo kutakuwa hakuna mpiganaji !

swala la kuwa huyu jamaa atakufa kisiasa pia ni theory is not practical, na wote wanaosema hivyo ni kujaribu kutabiri kama akina Yahaya!

Tukiwa wakali kuwalinda wale wapiganaji wetu tutawaokoa wengi, tukiwa waandika nakala kama wewe tutaua wengi mwishowe utabaki wewe peke yako maana wooote watachukuliwa na upepo.

Uwazi wa Zito ni mzuri ndugu , ni picha tunapata kuwa ni jinsi gani vyama vinavyojiita mbadala vinaishi, Zito angekuwa wa kujikomba angekaa kimya!

KWA NAKALA YAKO UNAPROVE PIA KUWA ZITO YUKO JUU SANA ZAIDI YA CHADEMA, CCM huwa hawafanyi ujinga huu, angekuwa mdogo; why all this unconvicing articles!

Mwambie Mtei na Chadema wote kuwa habari zenu tumezipata na mnavyoishi humo, hamna tofauti na CUF, NCCR, TLP.

Shida ilikuwa nini si angeachwa ashindwe kwenye kibox cha kura, wewe hili hufikirii??

swali la kumalizia, tunawalindaje hawa wapiganaji?? maana juzi tu ulikuwa unampenda Zito , leo humtaki, kesho utamkacha Slaa, maana tuhuma zipo tu, na tusivyopenda vithibitisho!

why are we not believing in them, when then we will belive them as true dream leaders??

Mtu gani mkweli atakayeingia kwenye siasa na kuishi namna hii??

ETI KULINDA CHAMA THIS IS POPPYCOCK !!!, AKILINDE KISHA WAJE KUCHUKUA NCHI, SI KAMA YA KENYA YA KUMUONDOA MOI, THEN WAO HAWATAKI KUTOKA, THUBUTU !!! better this what is CHADEMA ANYWAY , mjinga sana wewe!!

Upumbavu huu anaouvumbua Zitto badala ya kufurahia ndio mnasema kulinda chama, TOFAUTI YA HII NA CCM ni nini then

Kwa wataka mabadiliko tusio na makundi this was good movies, kuona kumbe hakuna cha CHADEMA wala CCM, wala CUF , TLP, NCCR, we are long way to true revolution, lets think another way!

ETI KULINDA CHAMA!!! huu ujinga hausameheki, NDIO MNAISHI NA WANAWAKE WAZINZI ETI KULINDA NDOA!

mchaga nini wewe!!!!!!!!!!

Mkandara,

..wengine tunakerwa na chuki za waziwazi zinazoonyeshwa ktk posting kama hiyo ya Waberoya hapo juu.

..na wachangiaji wa aina hiyo ni wengi tu hapa jamii forums.

..unakuta mtu ana tatizo na mchaga mmoja lakini anajaribu kuelekeza chuki zake kwa jamii nzima ya wachaga.

..mimi nawaomba moderators wawafungie wachangiaji wanaoeneza chuki zao zao za kikabila dhidi ya Wachaga.

..mara nyingine jamii forums inakuwa sawa na ile redio ya Kangura ya kule Rwanda.

Mkandara,

Nakubalina na wewe ila nadhani ni vizuri kuweka vitu katika proper context. Kwanza kabisa ni lazima watu wajue tunapozungumzia hao Wachagga, tunawazungumzia Wachagga wa wapi? Kwani katika wachagga mila, desturi na lugha zinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine. Unajua ya kuwa kuna lugha zaidi ya thelathini katika hao Wachagga mnaowazungumzia. Mfano Mchaga wa Machame na Marangu hawaelewani kabisa lugha, ni kama kichina na kijapani. Kwa hiyo hawa watu wawili wakitaka kuwasiliana they don't have a choice but to speak Swahili! Apart from that, there is so much hatred amongst Wachagga which can be traced three to four generations ago.
Nakubaliana na wewe sana na sababu hasa ya mimi kuulizia ni kutokana na maandishi nayoyasoma humu JF.. Watu hawapendi kusikia jina la Mchagga likitajwa lakini wakakti huo huo ktk Utetezi wa mtu huyo utasikia Wachagga ni wachapa kazi kuliko makabila fulani na fulani.. yaani ile lugha ya Makaburu ikitumika kuwapamba Wachagga badala ya kujibu tuhuma zinazotokea..
Mathlan inasemekana ndani ya Chadema kuna Ukabila.. sasa ikiwa hakuna na viongozi wetu wanadai hakuna kuna shida gani watueleze kwa nini asilimia 70 au juu ya viongozi wake wa juu ni Wachagga!

Ni maswali ambayo mwaka 2000 tuliwauliza CUF wakaja na majibu hayo hayo kuwa wao sii wadini lakini still waliendelea kuwa na hesabu kubwa ya viongozi waislaam pasipo kujibu hoja za msingi kwa wananchi. Hata kama ikiwa sababu ni kwamba CUF ina aslimia kubwa ya wasomi waislaam au Chadema in asilimia kubwa ya wasomi Wachagga ndio sababu...
 
Mawazo ya Philemon Mikael kuwa wachaga wawapo sehemu yoyote hufanya kila wafanyacho kwa juhudi tofauti na makabila mengine ni ya kibaguzi na ni sumu kwa huo uchaga!

Wanajamvi; hii inamanisha hamjui hata neno LIVE linamaanisha nini; mnajipinda kuandika story za alinacha na kufanya lengo la mada hii kuharibiwa; do you mean bila pasco hatuwezi kupata live update from Chadema.
Wengine naona hamna hoja mnapiga story zisizo miguu wala kichwa; leteni live hapa sio kupiga story; tumesoma story nyingi ukabila/udini/upagani/ has ktk propaganda za ki-ugoro tangu enzi hizo; sishangai sana; mana hata CUF mvuto wake ulikosekana kwa kusingiziwa kuwa wadini; kweli ikawa; sasa UT uko chadema kutafuta pahala pengine pa kutokea; i dont know kama wakifaulu then fine else umma ipo siku utawahukumu pamoja na malaya wao wa propaganda ambao lengo ni kuzima ndoto za Watanzania zilizoshindwa kutimia miaka karibu 50 sasa; j amani we are very poor; real poor; what are we doing aibu kwako mwan JF ambaye unapewa hela ili kusaliti watanzania na kuleta propaganda zako hapa; ipo siku tumbo lako litapasuka hata umekufa utatoa machozi kwa kusababisha matatizo ya mamilioni ya watanzania; talk aboout kilimo kwnza; talk about maisha bora kwa kila MTZ; talk about ufisadi; talk about uwezeshwaji wanawake; talk about the millenium challenges; talk about shule za kata na barabara za njia tatu; talk about maji/umeme je kweli tuko sawa; hivi WATZ tumelogwa na nani?? tuanenda wapi? jichunguze na jiangalie na jua roho yako inakusuta kama kweli unasaliti jamii yako
 
Mkandara,

..wengine tunakerwa na chuki za waziwazi zinazoonyeshwa ktk posting kama hiyo ya Waberoya hapo juu.

..na wachangiaji wa aina hiyo ni wengi tu hapa jamii forums.

..unakuta mtu ana tatizo na mchaga mmoja lakini anajaribu kuelekeza chuki zake kwa jamii nzima ya wachaga.

..mimi nawaomba moderators wawafungie wachangiaji wanaoeneza chuki zao zao za kikabila dhidi ya Wachaga.

..mara nyingine jamii forums inakuwa sawa na ile redio ya Kangura ya kule Rwanda.

Hapana, kumfungia mtu hujamsaidia. Ndo maana hapa JF tunatoa mawazo kwa uwazi, kama ukiona mtu anatoa shutuma zisizokubalika basi jibu hapo hapo ukikanusha na toa mifano halisi ili umuelimishe huyo mwenye mawazo potofu.

Tanzania hatuna ukabila wa kulalamikia japo kuwa tusipo kuwa makini tutauleta. Nakumbuka UDP waliwahi kusemwa kuwa ni chama cha wasukuma, sijui iliishia wapi hiyo. Tatizo la CHADEMA mimi nilisema majuzi kwamba wanaoleta shida ni hawa wanofikiri lazima wawe viongozi kwa gharama yoyote ile, na wanapokosa tu, basi, wanaanza oh...uchaga..oh....ukurya......n.k.

Chama chochote kinacho anzishwa na malengo ya ukabila au udini kwa nchi kama Tanzania hakidumu.
 
Mkandara,

..hebu tuonyeshe ni wapi kuna mchangiaji amesema Wachaga ni wachapa kazi kuliko kabila "X."

..tafadhali wacha kuhalalisha chuki za waziwazi ambazo zimekuwa zikiendelea hapa jamii forums kwa kipindi chote cha uhai wake.

..unadai 70% ya viongozi wa juu wa Chadema ni Wachaga, sasa nakuomba utuletee orodha ya viongozi wa Chadema tuone kama ni kweli.
 
Recta,

Mkuu nakukubali na hakika ndivyo navyofikiria kwani kama binadamu ni lazima nikubali pia kupokea reality ya mambo. Kwa mfanoi nimesoma mambo mengi hujmu yanayochukuliwa kama Ukabila lakini sii katika Tafsiri uloandika hapo juu. Kwa mfano mimi kumpigia kura Mkerewe mwenzangu na pengine Wakerewe kumshabikia huitwa Ukabila, lakini wakati huo huo sidhani kama ni Busara kwa Wakerewe kufikiria kwamba maendeleo ya wakerewe yanaweza letwa na mtu wa kuja!.. Hisia za kimtazamo wa aina hii hauwezi kuishia ktk kabila tu kwani hata tukitazam Kitaifa ni Ujuha mkubwa kwa Watanzania kufukiria kwamba maendeleo yetu yanaweza letwa na wageni, na tunapowachagua viongozi wetu na kuweka masharti kuwa ni lazima wawe Watanzania basi sisi ni wabaguzi.
Mimi sielewi hili neno Upendeleo wa makusudi kwa malengo ya kujinufaisha ina kipimo gani kwani mathlan Hivi Mchagga akisema anataka kuolewa na Mchagga (upendeleo) na kwa makusudi kabisa ya kupendelea kuhakikisha kizazi chake kinajiboresha ktk misingi ya Uchagga huyu mtu ana kosa gani?..Mkuu hata koo zetu kama WATU zinatafsirika kwa makabila, na Ubin wetu unatokana na kizazi cha mababu zetu iweje kuenzi na kupenda kwa makusudi kabisa kuendelea hizo mila iwe ni kosa?..
Nachosema mimi Ukabila upo na siwezi kuona madhara yake ikiwa tu una lengo ya kumwendeleza mtu pasipo kuyapanda makabila mengine mgongoni..
Mkuu hizi tafsiri ndizo zinanishinda mie kuelewa hata ktk UZAWA kwa sababu sioni Ubaguzi wowote ikiwa leo tutaweka kipaumbele maendeleo ya Wazawa ati kwa sababu tu asilimia 80 ni weusi basi iwe tunafanya Ubaguzi. Neno WAZAWA limegeuzwa maana yake kabisa kisiasa lakini ktk maiha yetu ya kila siku tunawatambua kama wakazi asilia kabla ya Uhuru..
Mkuu maelezo yako yote hapo juu ni sahihi kabisa. Ila yanaangalia upande mmoja tu. Na vile vile hayakanushi maana halisi ya ukabila (kama nilivyojaribu kuiweka hapo juu).

Kumbuka ndugu yangu kuwa kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Ulichoainisha hapo juu ni uhalali, uzuri na manufaa ya ukabila/utaifa, maamuzi binafsi n.k. Ni halali ukiiona hivyo kwa mtazamo wa hali hiyo.

Mkuu, katika jamii iliyochanganyika, yenye watu wa imani na asili tofauti huwezi kuwabagua (kwa kuzingatia makabila yao) katika mambo yanayowahusu kwa usawa bila kuonekana mkabila. Nadhani unanielewa. Maana yake ni kwamba, ndoa yako si ya kila mtu. Wewe unao uhuru wote wa kumchagua utakaetaka awe mkeo kwa kuzingatia vigezo vyako mwenywe bila kuhitaji kujali tabaka lolote linatamani nini. Hiyo ni issue ya kibinafsi kabisa. Taifa pia, linayo haki ya kibinafsi kabisa kulinda maslahi yake ya ndani kwa kuzingatia vigezo vyake vya ndani na isionekane kuwa ni ubaguzi. Ubaguzi unaanza pale mtu/kundi la watu linapoanza kuainisha ubaguzi katika mambo yanayohusu umoja wao. Mambo ambayo yanataka haki sawa, mamlaka sawa na mazingira sawa kwa wote. Katika hali kama hiyo, ukiweka ukabila, unaharibu kabisa na unaweza kusababisha matatizo makubwa. Hapo ndipo tofauti inapojitokeza kati ya maelezo yako na hali inayozungumziwa hapa kuhusu CHADEMA.
 
Wachaga hawana ukabila...tena kizazi hiki kipya (chini ya miaka 25) baadhi yao ndio kabisa hata Kilimanjaro yenyewe wanaisikia kwenye vitabu tuu.

Wengi humu wanaochangia hawawajua Wachaga, wanafuata mkumbo tu..!!
 
Anzisheni thread mpya ya kujadili huo ukabila wenu! Si wengine tunasubili Update za nini kinaendelea kwenye mkutano! aarrrrgh mnakera!
 
Jokakuu,
mkuu wangu hivi wanisoma kweli au ndio hizo zakuogopa unyasi?..
Mkuu linapotumika neno mathlan ina maana sawa na neno - Kwa mfano... sikusema kuna wachagga viongozi asilimia 70 ndani ya Chadenma isipokuwa katika kuwambieni jibuni hoja ama tuhuma zinazodaiwa...

Halafu mkuu unaniuliza kama kuna mtu alowahi kusema kuwa Wachagga ni wachapa kazi! Nikikuonyehsa je Utakuhbali kuwa Wachagga ni Wabaguzi au! maanake sii maana yangu kusema hivyo ila inaonyesha wazi sasa hivi wewe hutaki kuelewa. Nachosema mimi tusiwe pewesi kulalamikia Ubaguzi, kama mtu kasema na kalaumu kuna Ubaguzi Chadema au CUF ni jukumu letu sisi wahusika tujitazame na kuja mana majibu yatakayo waridhisha wale waliouliza..
 
Semilong, Ikiwa Wachagga wamezungumzwa sana miaka hii ya karibuni kwa nini msitake kuchunguza kwanza madai haya?.. iweje sisi Waafrika tuliweka madai yetu kuhusu makaburu na hata Ubaguzi wa Marekani na kila siku kupamba moto tukawashangaa wazungu kushindwa kuliona hilo!
Sina maana Wachagga ni wabaguzi ila sioni sababu ya Wachagga kuhofia kitu kisichokuwepo. Waache waseme wanaotaka kusema kisha watalala kwani kama wewe hutembei na mke wa mtu unachoogopa kitu gani?..Mkuu wangu pengine mimi nina imani tofauti lakini nimefundishwa hivi: Mara zote mtu anayependa kuruka hata akisikia unyasi ukiyumba basi fahamu ana lake jambo!..

Wachagga wamezungumziwa sana. Kuna wakati baadhi ya watu (hata ndani ya serikali) waliuliza uwepo wa wachagga ndani ya TRA kwa wingi. Na pia wengine waliongezea kusema uwepo wao kwenye taasisi nyingi za umma. Kuna waliokwenda mbalia zaidi kutamani kuchukua haua dhidi yao (wakashauriwa kuacha).

Ninachoweza kusema ni kuwa, kauli hizo hazikuwa na maana zaidi ya uchochezi wa chuki na wivu. Kwakuwa waliokuwa wakisema hivyo hawakuendelea kusema walitaka iweje kwa wachagga wanaohtimu shule zetu na kufaulu vizuri, kwenye utaratibu wa kusaili watu kwa ajira mpya (recruiting), na ni kazi gani hasa ambazo zingewafaa watu hao.

Mkuu wangu hakuna sumu mbaya kama kukaa kimya katika mambo ya hatari. Ukiwaka moto ndani ya nyumba yako na ukaamua kuendelea kupiga usingizi ukidhani kuwa "si utaisha tu". Kweli utaisha, ila utaishaje ndio swali unalotakiwa kujiuliza kabla hujaendelea kuvuta shuka.

Siwezi kabisa kusema kauli hizo za wazi ni sawa na unyasi unaoyumba. Ni kauli ambazo zinaweza kufanyiwa kazi na kuathiri ustaarabu wa watu wetu kama si kusababisha maafa makubwa. Ubaguzi ni sumu mkuu, na unaanza kwa kauli halafu vitendo hufuatiwa kwa nguvu nyingi. Rwanda na Burundi ni mifano ya kutosha sana.

Nimefundishwa hivi: It is with hatred as with sun-beams, the more it is practised, the deeper it burns.
 
Mkuu maelezo yako yote hapo juu ni sahihi kabisa. Ila yanaangalia upande mmoja tu. Na vile vile hayakanushi maana halisi ya ukabila (kama nilivyojaribu kuiweka hapo juu).

Kumbuka ndugu yangu kuwa kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Ulichoainisha hapo juu ni uhalali, uzuri na manufaa ya ukabila/utaifa, maamuzi binafsi n.k. Ni halali ukiiona hivyo kwa mtazamo wa hali hiyo.

Mkuu, katika jamii iliyochanganyika, yenye watu wa imani na asili tofauti huwezi kuwabagua (kwa kuzingatia makabila yao) katika mambo yanayowahusu kwa usawa bila kuonekana mkabila. Nadhani unanielewa. Maana yake ni kwamba, ndoa yako si ya kila mtu. Wewe unao uhuru wote wa kumchagua utakaetaka awe mkeo kwa kuzingatia vigezo vyako mwenywe bila kuhitaji kujali tabaka lolote linatamani nini. Hiyo ni issue ya kibinafsi kabisa. Taifa pia, linayo haki ya kibinafsi kabisa kulinda maslahi yake ya ndani kwa kuzingatia vigezo vyake vya ndani na isionekane kuwa ni ubaguzi. Ubaguzi unaanza pale mtu/kundi la watu linapoanza kuainisha ubaguzi katika mambo yanayohusu umoja wao. Mambo ambayo yanataka haki sawa, mamlaka sawa na mazingira sawa kwa wote. Katika hali kama hiyo, ukiweka ukabila, unaharibu kabisa na unaweza kusababisha matatizo makubwa. Hapo ndipo tofauti inapojitokeza kati ya maelezo yako na hali inayozungumziwa hapa kuhusu CHADEMA.
Mkuu nakusoma sana lakini nachotakamkuuliza kuna Ubaya gani kama tuliyachukulia haya yanayoandikwa hapa kuhusu Chadema na Ukabila na kuyatazama kama upo kweli au hao viongozi wa Chadema wana maelezo gani kupinga tuhuma hizi. Mkuu haiwezekani wangwe, Zitto na baadhi ya watu toka kina kabourou kila mmoja wao issue iwe Ukabila Chadema na matumizi mabaya ya fedha makao makuu.. Kwa nini tunashindwa kuangalia undani wa issue hizi ka tunavyoutazama Ufisadi wa Lowassa, Rostma na wengine ambao tumetumia hata makabila yao, uzawa wao kuzungumza mengi machafu yanayowahusu.. Still hatukukubali kuondoa focus yetu ktk ukjweli kwamba kulikuwa na tatizo kubwa la kuhujumu Uchumi wetu.
 
Mkuu, kwa mara nyingine nakubaliana na wewe kuwa ni vyema hali yoyote inayoashiria ubaguzi ndani ya CHADEMA ichunguzwe na wanaohusika. Naamini hata jamvi hili halitaona haya kuyazungumzia na kutoa mapendekezo yanayoweza kusaidia. Hili lisifanyike kwa CHADEMA tu, ila kwa taasisi au chama chochote kinachoonekana kukumbwa na tatizo hilo.

Mkuu, Hayati C. Wangwe aliongelea ukabila ndani ya CHADEMA miezi michache kabla ya kifo chake (Mungu amuweke mahali pema peponi). Kumbukumbu zangu zinanikumbusha kuwa

1. alikuwa mwanachama kwa muda mrefu kabla hajasema maneno hayo

2. Alitarajia au alitabiriwa kushindana katika uchaguzi fulani

3. Alikuwa karibu na wanaoitwa mafisadi nje ya chama hicho n.k.

Hali hiyo inaelekea kufanana sana na hali iliyomkuta Ndugu yetu Zitto hivi karibuni. Na ndio maana nadhani inafananishwa sana. Sijasikia mwingine ndani ya chama hicho aliedai hivyo.

Ila ukweli unabaki kuwa wote wawili walikuwa wananchama wa chama hicho (tena si kwa muda mfupi). Sasa inakuwaje wakavumilia ukabila huo kipindi chote hicho hadi walipofarakana katika masuala ya kiuongozi? Mkuu labda tuanzie kujiuliza kutokea hapo. Tunaweza kupata njia inayofaa zaidi.
 
- Hapa Bob, tupo pamoja sana na saafi sana.

Respect.

FMEs!
 
- Mkuu Recta, viongozi wengi wa Chadema, wamekua wakilalamikia ukabila na matumizi mabaya ya pesa huko makao makuu, binafsi nimeuliza sana kuhusu matumizi ya helikopta, huku wagombea ubunge wengi wakiwa hawana kabisa hela za kugombea, sasa kitendo cha wazee wa Chadema kuingilia kati uchaguzi kinaleta hisia isiyo nzuri kwamba huenda kuna something wanajaribu kukilinda, je nini hasa?

- Na kwa nini Chadema isiongozwe na mtu huru kutoka kwenye mikono ya Mzee Mtei?

Respect.

FMEs!
 
..nadhani mwalimu angekuwa hai ungemuuliza hilo...maana yeye alikuwa akisema dhambi ya ubaguzi ikija nchi hii itaanza [au imeanza] na WAHINDI....tukiwamaliza ....tunaangaliana wenyewe ..na kwa maneno yake alikuwa akipenda ku joke "wataanza na wachagga ..hawa wachagga wana maduka ..wamesoma..tukimaliza ..tunaendelea mbele zaidi..wahaya ,wanyakyusa hadi tunamalizana...""

Sifa kuu ya hawa wachaga ni kufanya juhudi kwa kila atakachofanya...akisoma atasoma kwa bidii ,akifanya biashara vile vile ....na hata wale wezi pia [tukumbuke kila mahali wezi wapo....ila mwizi wa wachagga haibi maisha yake yote kwani akipata mtaji tu anabadili..tofauti na wengine ambao ataba hadi anazeeka...kiddin..]kimsingi wachagga hawapo wengi kama wasukuma au wanyakyusa..ila wametapakaa kila sehemu unayoijuwa wewe ndani ya Tanzania....kila mtu akitoka kijijini kwake iwe sumbawanga ...hadi mtwara anakuwa na memory ya wachagga wanaofika kwenye vijiji vyao kutafuta nafasi za biashara....na kimsingi wachagga wasiosoma wanajuwa kutafuta pesa ..na wala hawaoni aibu kushona viatu ,kupika uji au supu stendi...labda kazi ya kibarua shambani ndio hawafanyi!!...kazi yeyote isiyokuwa ya kuajiriwa wanaipenda....

sipendi kuamini kuwa wachagga wanachukiwa au kuogopwa ....na sipendi kuamini kuwa kuliko mchagga apate kitu bora kumpa mgeni...mchaga ni kabila tu lakini zaidi ni MTANZANIA!!!
Mwalimu HUYO HUYO ALIWAHI KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA UKABILA SHIRIKA LA BIMA.MWALIMU HUYU HUYU ALIWAPENDELEA WATU WA MUSOMA KUWAPA NAFASI WASIZOSTAHIKI MFANO WARIOBA ALIPEWA UWAZIRI MKUU,MKONO AKAPEWA KAZI ZA KISHERIA ZA SERIKALI ACHUKUE YEYE,CHARLES NYIRABU AKAMPA UGAVANA.GENERAL MUSUGURI AKAWA MKUU WA JESHI.

KWA HIYO WACHAGGA KUJAZWA CHADEMA KWA VILE NI WACHAPA KAZI?
 
- mkuu recta, viongozi wengi wa chadema, wamekua wakilalamikia ukabila na matumizi mabaya ya pesa huko makao makuu, binafsi nimeuliza sana kuhusu matumizi ya helikopta, huku wagombea ubunge wengi wakiwa hawana kabisa hela za kugombea, sasa kitendo cha wazee wa chadema kuingilia kati uchaguzi kinaleta hisia isiyo nzuri kwamba huenda kuna something wanajaribu kukilinda, je nini hasa?

- na kwa nini chadema isiongozwe na mtu huru kutoka kwenye mikono ya mzee mtei?

respect.

fmes!
ni chama cha wachagga lazima kiwe mikononi kwa wachagga kwa gharama yeyote.pili ni bugwagi yao yaani sehemu yao ya kujipatia pesa.
 
Mawazo ya Philemon Mikael kuwa wachaga wawapo sehemu yoyote hufanya kila wafanyacho kwa juhudi tofauti na makabila mengine ni ya kibaguzi na ni sumu kwa huo uchaga!

...hakuna mtu yeyote anayeweza kufanikiwa bila kujituma.....na hutakiwi kuchagua kazi..mradi iwe halali...bila kujali kabila au taifa hiyo ndiyo siri ya mafanikio...

hata hapa forum ukiona mtu kama mwanakijiji....au FMES ameandika makala nyingi basi ujuwe ana juhudi kuliko wenzake....

sidhani kama ulitaka niseme kuwa hao wachagga mnaoona wamefanikiwa ....wanakaa tu mafanikio yaje kama mkate wa mana....huo ndio ukweli !!!

Kaama taifa kwa pamoja lazima tufanye kazi sana na tuache chuki ...tusifike kwa kazi!!.... unafikiri ninapowataja wachina au wajapani..si mnawahusisha na juhudi na maarifa??? je kwa sisi watanzania tunapokuwa nnje au ndani...tunahusishwa na juhudi au maneno matupu??...ili swali nataka kila mmoja ajiulize ...na ikibidi kila mmoja abadilike.......dunnia inakoelekea mataifa yenye wachapa kazi ndio yataenda mbele.......na si vinginevyo....tusikatishe wenzetu tamaa..au kuwafanya watu wawe wavivu na wakae wakiwasema wale wanofanikiwa.......
 
mkandara,

..hebu tuonyeshe ni wapi kuna mchangiaji amesema wachaga ni wachapa kazi kuliko kabila "x."

..tafadhali wacha kuhalalisha chuki za waziwazi ambazo zimekuwa zikiendelea hapa jamii forums kwa kipindi chote cha uhai wake.

..unadai 70% ya viongozi wa juu wa chadema ni wachaga, sasa nakuomba utuletee orodha ya viongozi wa chadema tuone kama ni kweli.

mheshimiwa zitto kawataja kama kina john mrema. Wabunge wa viti maalum watano wanatoka kilimanjaro.

Hajawahi kutokea mwenyekiti wa chadema asiye na connection ya uchagga, mtei-mchagga,makani ameona mke wa kichagga na watoto wake ni wachagga, mbowe- mchagga.
 
Back
Top Bottom