....kweli kabisa uyasemayo...na mimi bado sijawahi kuona mwanasiasa anayegombea nafasi ya uongozi eti ili aje awatumikiye wananchi....sijawahi/sintowahi kuona.....Hawa wote ni Wanasiasa kama vile walivyo watu wengine vile hivyo kuna hali ya freaking fulani hivi so CHADEMa kuwa Imara siku zote
Mi nafikiri wakati umefika wa kujadili john mnyika kwa upana,in depth,maana inaonekana katika kila tatizo la chadema,john mnyika anatajwa kutumika,na sio kama mtu huru mwenye misimamo yake.
kuridhika ama kutoridhika na cheo inategemea sana falsafa yake juu ya maisha ya kisiasa, na uelewa wako juu ya CHADEMA, PIA HUTEGEMEA na matamanio yake kama kijana.
KURIDHIKA AU KUTORIDHIKA KUTATEGEMEA NAMNA GANI WALE ALIODHANI NI MAADUI ZAKE WATASAMEHEANA NAE PALE MAKAO MAKUU,KINONDONI.
NAAMINI ZITO SI MUOGA HIVYO ATAJITOKEZA HADHARANI KUTUELEZA KAMA AMERIDHIKA AMA LAAH.
Nadhani ulimaanisha PM, na si MP. Hiyo avatar imenikumbusha alama ya jembe na nyundo, lakini sijui wale wafanyabiashara wafadhili wanaangukia wapi katika hizo alama!!Labda uMP, ni memba hapa JF
wajitangaze nini wakati tunawajua.achana na propaganda za CCMWameshindwa kulipia hata kwenye redio ili mkutano huu uwe live angalau masikioni tu? Wenzao CCM hii namna moja ya kujinadi na kujitangaza.
Wanabodi, nilihudhuria Mkutano huu, Mabalozi wafuatao walikuwepo in person, Tim Clarke, wa EU, Diane Corner wa Ujerumani, Balozi wa Canada, Balozi wa Uholanzi na Balozi wa Sweden!.Salaam, nilihudhuria mkutano mkuu wa Chadema uliofanyika ukumbi wa Kiramoo ulioko Mbezi Beach Sec School.
Siku ya kwanza ulianza kwa maandamano na kufuatiwa na hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Mwenyekiti Mbowe.
Siku ya pili ulipokea taarifa mbalimbali za chama na kufanya uchaguzi mkuu.
Matokeo ni:-Mwenyekiti ni Freeman Mbowe: kura ndiyo 425 (93%), kura hapana 22 (5%), Zilizoharibika 10.
Makamu mwenyekiti znz: Said Issa Mohamed 243 (53%), Said Mzee Said 212 (46%), Zilizoharibika 4
Makamu mwenyekiti bara: Said Arfi 315 (69%), Shambwee Shitambala 99 (22%), Ben Kapwani 40 (9%), Zilizoharibika 2.
Uchaguzi umekwisha sasa kwa Chadema imebaki kuponya vidonda, kufukia makovu na kujenga chama tayari kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2010.