Uongozi Mpya wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Salaam, nilihudhuria mkutano mkuu wa Chadema uliofanyika ukumbi wa Kiramoo ulioko Mbezi Beach Sec School.
Siku ya kwanza ulianza kwa maandamano na kufuatiwa na hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Mwenyekiti Mbowe.

Siku ya pili ulipokea taarifa mbalimbali za chama na kufanya uchaguzi mkuu.
Matokeo ni:-Mwenyekiti ni Freeman Mbowe: kura ndiyo 425 (93%), kura hapana 22 (5%), Zilizoharibika 10.

Makamu mwenyekiti znz: Said Issa Mohamed 243 (53%), Said Mzee Said 212 (46%), Zilizoharibika 4

Makamu mwenyekiti bara: Said Arfi 315 (69%), Shambwee Shitambala 99 (22%), Ben Kapwani 40 (9%), Zilizoharibika 2.

Uchaguzi umekwisha sasa kwa Chadema imebaki kuponya vidonda, kufukia makovu na kujenga chama tayari kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2010.
 
Last edited by a moderator:
tunafuatilia mkuu. Ni mkutano muhimu sana huo, a golden chance for Zitto Kabwe and Chadema!
 
Wameshindwa kulipia hata kwenye redio ili mkutano huu uwe live angalau masikioni tu? Wenzao CCM hii namna moja ya kujinadi na kujitangaza.
 
Humo ndani hakuna demokrasia, kura zilezile za enzi za mwalimu, ya kuchagua mwalimu na kivuli. Zidumu fikra za mwenyekiti Mbowe!
 
tunafuatilia mkuu. Ni mkutano muhimu sana huo, a golden chance for Zitto Kabwe and Chadema!
Mh. Zitto yupo meza kuu amekaa next to Bob Makani. Zitto anajitahidi kusmile kwa nguvu sana ili kuwathibitishia wajumbe all is well.
 
Mh. Zitto yupo meza kuu amekaa next to Bob Makani. Zitto anajitahidi kusmile kwa nguvu sana ili kuwathibitishia wajumbe all is well.
Hao ndio wanasiasa wetu TZ. Hakuna chuki, hasira wala ADUI wa kudumu kwenye siasa. Usishangae siku Mh Mwakyembe na EL watakumbatiana na kucheka sana.
 
Mbowe amemalizia kwa kuifagilia Cuf na kusisitiza Chadema itashirikiana na vyama makini tuu. Ccm kumbe ilitoa ushauri kwa Chadema jinsi ya kuendesha demokrasia. Amesema hali ya Chadema ni kama ina mafua ila Ccm ina kansa. Hotuba ya Mbowe imekuwa ikikatishwa na ushangiliaji unaongozwa na Jose Selasin
 
Selasin kajiunga juzi tu tayari ni mjumbe? Kwa kuwa ni MCHAGA?
 
Ukumbi uligeuka uwanja wa dansi kwa muda kushangilia hotuba ya Mbowe. Kumbe Chadema pia wana Tambalizeni wao. Hotuba ilifuatiwa na utambulisho wa wageni na sasa ni salaam za Cuf zimesomwa na Lipumba na za Ccm zimesomwa na Madcida
 
Back
Top Bottom