Uongozi katika siasa na siasa katika uongozi

Alaik

Member
Jul 30, 2012
61
119
Habari zenu wakuu
leo nataka kuzungumza juu ya kiongozi na mwanasiasa, Tunapozungumzia kiongozi wa kisiasa tunamaanisha kwanza lazima huyo mtu awe kiongozi, pili anaongoza katika siasa. Nchi yetu inatatizo kubwa sana la kiuongozi wengi wao wamekuwa wanasiasa katika uongozi na sio viongozi kwenye siasa.
Haiwezekani kabisa kiongozi wa nchi kupitisha jambo fulani kwa maslahi yake binafsi au chama chake hilo halipo kabisa kwenye sifa za kiongozi. Umechaguliwa na mamilioni ya watu wakakuamini wewe ubebe ndoto zao za miaka mitano au kumi ijayo alafu wewe unataka kuzizima kwasababu tu unataka umaarufu kwenye chama chako au rafiki zako. Watu wanaitwa viongozi wengi wametufikisha hapa tulipo( Inategemea na mtazamo wako juu ya mahali tulipo) unajilimbikizia mali na pesa za wananchi masikini alafu unasimama jukwaani kumnyooshea mwenzio kidole hii ni hatari sana.
Tunataka watu tuliowapa dhamana ya kutuongoza wajue wamebeba maono yetu kwa kipindi chote cha uongozi wao na ikumbukwe " The character of the Kingdom emanate from the King" Watanzania hawaitaji polisi ili kuendelea wanahitaji hekima, haki, usawa, utulivu na heshima katika shughuli zao za kila siku. msitutishie eti fulani akiwa hivi basi amani itatoweka labda niwaaambie kuwa amani ni mazingira ya kulea kitu " Peace is just the atmosphere that exist to support something" hatuhitaji amani kama Amani tunahitaji amani kama mazingira ya kutuleo kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimaendeleo kama hivyo hakuna sasa amani ya nini?.
Zipo nchi zinapigana usiku na mchana lakini wanatuzidi maendeleo katika kila eneo sisi tunawazidi mazingira ya amani hii ni aibu sana. Ukiangalia rasilimali za nchi hii utachanganyikiwa kwanini sisi ni masikini yaani Kiongozi tuliyemchagua atupe Vision nae anaomba kwa watu watusaidie kila mtu amebaki kuwa ombaomba.
Tubadilike katika maisha yetu kwanza tusitazame kama kuna mtu wa nje atakaye tutoa hapa tulipo ni sisi wenyewe pasipo kuweka itikadi zetu za kidini, kisiasa na kijinsia kukubali kupambana kwa ajili ya nchi yetu, ifike mahali tuchukie rushwa, ufisadi na uhuni kwa vitendo na sio kwa kelele za magazetini mbona nchi zingine wameweza sisi tuna nini mpaka tushindwe.
Mnisamehe kwa maneno mengi ila jua tu inahitaji utayari na busara " MWENYE HAKI NI JASIRI KAMA SIMBA" ukitaka kuelewa uwe unakosa uone kama wewe ni jasiri.
" Cheap is expensive"
 
Back
Top Bottom