Uongo wa Serikali juu ya Miradi ya kitaifa Nani ashugulikiwe

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Machi 26 mtendaji mkuu tanload alisema Daraja la Wami litakamilika Sept 2021. Kwa mujibu wa Mwananchi, Leo Serikali inakuja na Lugha nyingine. Kwanini tunafanywa watoto

Miaka miwili nyuma tuliambiwa kipande Cha reli dar to Moro kuzinduliwa Novemba 2019. Leo 2022. Miaka 3 baadae hakuna kitu Kama hicho.

Mwaka 2p16 Raisi Magufuli anasaini mkataba na Benki ya Exim ya watu wa China ili kupata fedha za kujenga reli Dar to kigoma tsh tillion 16. Leo mama anasema atakopa kutoka sijui Uturuki. Mbona sielewi.

Kama taifa Serikali au watendaji wake kutoa kauli zisizoishi ni kuufanya ionekane ni ya kihuni. Nani NI mkweli.

Je awamu iliyopita walipiga propaganda tu au Awamu hii hazituambii ukweli?

Tusikubali hizi longolongo Tena. Tena kwa vitu vinavyoepukika kwa muda mfupi . Inafanya Serikali isiaminike kabisa kile inachokisema hasa kwa maswala nyeti Kama Deni la Taifa, Akiba ya Taifa, Takwimu mbalimbali na tayari vyombo vya Magharibi hutilia Shaka taarifa zote kutoka nchi Zilizo karibu na Uchina.

Screenshot_20220103-170929.png
 
Attachments

  • Benki ya Exim ya China yakubali kutoa shilingi trilioni 16 kugharamia ujenzi wa reli ya kati. ...mp4
    5.4 MB
Machi 26 mtendaji mkuu tanload alisema Daraja la Wami litakamilika Sept 2021. Kwa mujibu wa Mwananchi, Leo Serikali inakuja na Lugha nyingine. Kwanini tunafanywa watoto

Miaka miwili nyuma tuliambiwa kipande Cha reli dar to Moro kuzinduliwa Novemba 2019. Leo 2022. Miaka 3 baadae hakuna kitu Kama hicho.

Mwaka 2p16 Raisi Magufuli anasaini mkataba na Benki ya Exim ya watu wa China ili kupata fedha za kujenga reli Dar to kigoma tsh tillion 16. Leo mama anasema atakopa kutoka sijui Uturuki. Mbona sielewi.

Kama taifa Serikali au watendaji wake kutoa kauli zisizoishi ni kuufanya ionekane ni ya kihuni. Nani NI mkweli.

Je awamu iliyopita walipiga propaganda tu au Awamu hii hazituambii ukweli?

Tusikubali hizi longolongo Tena. Tena kwa vitu vinavyoepukika kwa muda mfupi . Inafanya Serikali isiaminike kabisa kile inachokisema hasa kwa maswala nyeti Kama Deni la Taifa, Akiba ya Taifa, Takwimu mbalimbali na tayari vyombo vya Magharibi hutilia Shaka taarifa zote kutoka nchi Zilizo karibu na Uchina.

View attachment 2067221
Matarajio sio sawa na uhalisia, kwani wewe ukisema unatarajia kujenga mwaka huu na ukaisha hujajenga utakuwa ni muongo?

Ishu ni kwamba mambo hayajaenda kama ilivyotarajiwa, kwani kuna mtu hataki kumaliza mradi kwa wakati?
 
Huu uongo wa miradi ya taifa uliasisiwa na Magufuli, na tokea wakati akiwa hai tulikuwa tunasema ni kiongozi muongo. Sasa uongo wake unazidi kuendelezwa. Kuna hatari kuwa kuna ukweli mwingi sana wa hatari unafichwa.
Kama magufuli alidanganya basi uongo wake ulikuwa wa kizalendo tofauti na uongo wa kifisadi tunao danganywa sasa
 
Hii Ni nchi ya mazuzu, mazuzu yatafanya nini.

Jiwe aliasisi Uongo, uzandiki propaganda na imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kawaida.
 
Hamna uongo wa kizalendo ww. Yule alikuwa ni roho ya uharibifu.
Nani kakudanganya kuwa hakuna uongo wa kizarendo
1)Uongo wa kizalendo ni ule uliopo kwa maslai ya taifa
2)Na uwongo wa kifisadi ni ule ambao upo dhidi ya maslai ya taifa bali kwa maslai ya wahuni ,tokomeza wahuni popote uwaonapo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nani kakudanganya kuwa hakuna uongo wa kizarendo
1)Uongo wa kizarendo ni ule uliopo kwa maslai ya taifa
2)Na uwongo kifisadi ni ule ambao upo dhidi ya maslai ya taifa bali kwa maslai ya wahuni ,tokomeza wahuni popote uwaonapo.

Kipindi chake alitumia neno uzalendo kuwachota wajinga wa aina yako, kipindi hicho ilikuwa ngumu kutofautisha mzalendo na mjinga.
 
Nani kakudanganya kuwa hakuna uongo wa kizarendo
1)Uongo wa kizarendo ni ule uliopo kwa maslai ya taifa
2)Na uwongo kifisadi ni ule ambao upo dhidi ya maslai ya taifa bali kwa maslai ya wahuni ,tokomeza wahuni popote uwaonapo.
Kwamba tunajenga kwa pesa zetu kumbe unakopa,huo ni uhuni tu
 
acha ujinga, kwani mikopo wakati inasainiwa hukujulishwa?? alikopa sababu alijua tunalipa na ndio maana miradi mingi ilijengwa kwa fedha za ndani
Hajawahi kunijulisha,we alikupigia simu kukujulisha
 
Huu uongo wa miradi ya taifa uliasisiwa na Magufuli, na tokea wakati akiwa hai tulikuwa tunasema ni kiongozi muongo. Sasa uongo wake unazidi kuendelezwa. Kuna hatari kuwa kuna ukweli mwingi sana wa hatari unafichwa.

Magufuli alikuwa na NIA na DHAMIRA ya dhati ktk kuleta mabadiliko ya kweli kwenye nchi yetu, ndio maana amekuwa ni mtu wa vitendo zaidi ktk kutekeleza miradi mbalimbali aliyoahidi

Ishu ya kukamilika kwa miradi hio huwezi kumlaumu kiongozi wa Serikali kwakuwa na yeye anapewa ahadi ya makisio ya ukamilishaji wa miradi kutoka kwa wataalamu wanaohusika na ujenzi na usimamizi wa miradi

By the way kuna dawa hapa Burundi inaitwa Uburukutu inasaidia kuondoa sumu mwilini,,, Nakushauri ndugu Tindo, Sexless na wenzako muitumie kupunguza kiwango cha chuki kwa Magufuli,, je niwaletee!??? 😀
 
Back
Top Bottom