Uongo wa miaka juu ya miaka 2000 ya kifo cha Kristo

Yesu alizaliwa mwaka 2 mi Kwa taarifa tuu. Kama umewahi kusoma historia zamani watu walikuwa wanahesabu kutoka juu kwenda chini kwahiyo Yesu alizaliwa mwaka 2 kutoka juu. Kwahiyo Kwa mtiririko huo ni kwamba 2, 1, 0, 1 ,2, 3 kwahiyo ndivyo ilivyo. Fuatilia miaka ya AD after death au huitwa ano domino na BC maanake Before christ. Hata kwenye historia ndio ilivyo
Napenda kukusahihisha hapo kwenye kuhesabu kwa kurudi Nyuma ...umechanganya mkuu
 
Japo kuwa si mimi uliyeninukuu....ningependa tuendeleze mjadala
Awali ya yote zamani hawakuwa wakihesabu kurudi nyuma bali walikuwa wakihesabu miaka baada ya tukio fulani mfano wakati wa mfalme fulani nk
Rejea biblia takatifu.
Danieli 1:1
Danieli 1:1 BHN
Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Yehoyakimu wa Yuda, mfalme Nebukadneza wa Babuloni alikwenda Yerusalemu, akauzingira mji.
BHN: Biblia Habari Njema
huu ndio msimamo wangu,nilitaka yeye sasa kwa mujibu wa msimamo wake aeleze kama Yesu hajawahi kuwepo,hii miaka ilianzishwa na nini????
 
Hawa wanazuoni wametudanganya juu ya hii miaka ilioko. Leo hii hata huu mwaka tulionao sio mwaka 2019 itabidi wataalamu hata wa humu akina Jr mshana Rakism Kiranga na wengine wathibitishe hili.

Kama Yesu alizaliwa mwaka 0 na kufa mwaka 34 iweje tuseme alikufa miaka 2019 iliopita
Yesu alikufa miaka 1985 iliopita (2019-34=1984) hivyo huu ni mwaka 1985

Tunahesabu miaka kuanzia pale Yesu alipozaliwa, siyo kuanzia pale alipokufa na kufufuka hatimaye kupaa mbinguni! Angekuwepo duniani hadi leo, mwaka huu ilikuwa asherehekee Birthday yake ya kufikisha miaka 2019
 
Umewa nukuu vibaya, mkuu, baada kifo chake ndipo A.D inaanzia After Death :in the year of our lord Jesus Christ (Annno Domini nostri Jesu christi) yaani wakati wa bwana wetu Yesu Kristo (kumuenzi). Na B.C (Before Crucifixion). Kinyume na hapo ukifika Vatican holy City, utapata majibu mazuri zaidi juu ya swali lako.
 
Mimi huwa nasikia miaka 2000 iliyopita baada ya Yesu kuzaliwa. Hapa huwa haitajwi namba dhahiri ya miaka kama vile 2019, bali huwa wanatumia tu miaka 2000.
 
Yesu alizaliwa mwaka 2 mi Kwa taarifa tuu. Kama umewahi kusoma historia zamani watu walikuwa wanahesabu kutoka juu kwenda chini kwahiyo Yesu alizaliwa mwaka 2 kutoka juu. Kwahiyo Kwa mtiririko huo ni kwamba 2, 1, 0, 1 ,2, 3 kwahiyo ndivyo ilivyo. Fuatilia miaka ya AD after death au huitwa ano domino na BC maanake Before christ. Hata kwenye historia ndio ilivyo
AD ni anno domino sio After Death.
 
Ngoja waje ..jiandae kupokea mapovu mkuu
Yesu ajawahi kuexist popote pale duniani..

Waafrika sababu ni wavivu/tegemezi ndio maana mnapenda sana kuokolewa na mtu/vitu visivyo exist.

History huandikwa na aliena mamlaka kipindi cha tawala tofauti za dunia, sasa jiongeze kujua yale waliyoyaficha kwenye history zao
 
Funua yaliyofichika
 
Back
Top Bottom