Uongo wa Masoud Othman waumbuliwa. Kadanganya taifa kwamba "+259" ndiyo "Code" ya Zanzibar na "+255" ni ya Tanganyika wakati sivyo

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Sep 15, 2008
235
302
TITLE: UKWELI KUHUSU NAMBA YA SIMU YA KIMATAIFA "+259"
ANALYST: JOSEPH MAGATA
Cell: +255 75 4710684
PUBLICATION: RAIA MWEMA, pg. 12

Juni 8, mwaka huu Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman Masoud alitoa hotuba ambayo sehemu ninayoinukuu anasema,

"Kwenye serikali hiihii ambayo tumekuwa nayo ndiyo vikwazo vya kila aina, miye nawapa kimoja tu kwa mfano.Tulipoanza simu, zile zilisosajiliwa Bara, TRITEL, sijui nani, walipewa leseni mara moja. Ilipokuja ZANTEL ikasajiliwa Zanzibar. Kosa lake kusajiliwa Zanzibar. Ukawa ugomvi, ikawa vita vikubwa kwelikweli".

"Mpaka tukafika Geneva kwenye Shirika la Simu duniani, ITU, kwenda kusuluhishwa na baada ya kutishia kwamba tutakwenda kudai namba yetu 259." Maana hii tunayoitumia leo, "255" ni ya Tanganyika, ya Zanzibar ambayo mpaka leo hii ipo hajapewa mtu mwingine ni "259". Na ilibidi kwenda (ITU) kutishia kuidai ile namba kwa sababu wenzetu wamekataa kutupa leseni".

Je ITU walikoenda Masoud na wenzake wa Zanzibar ina majukumu gani?

Teknolojia ya "telegraph" iliyovumbuliwa mwaka 1837 ilitoa huduma za kutuma maandishi (telegram), kutuma pesa (moneygram) na baadaye "telex". Hivyo mwaka 1865 ITU ikaundwa ikiitwa "International Telegraph Union" kusimamia viwango vya teknolojia hii.

Mwaka 1876 teknolojia ya simu nayo ikavumbuliwa, kisha ikafuata ya redio na baadaye ya televisheni. Kufikia mwaka 1934 zikawepo teknolojia hizi nne, redio, "telegraph", simu na televisheni. Japo ITU ilianzishwa kusimamia "telegraph" ikajikuta inasimamia na hizi tatu, hivyo ikaitwa "International Telecommunication Union".

Teknolojia ya simu iliposambaa ilikosa mfumo unaofanana wa simu zinazoenda nje ya nchi, kila nchi iliunda wake. ITU ikaunda mfumo unaoitwa sasa "E.164" wa nchi kuwa na namba ya simu. Hivyo ITU ilipokutana Mei 25 hadi Juni 26, 1964 ilizipa nchi 129 namba za simu, ikiwemo Tanzania iliyopewa namba "255". Mkutano huo ulipogawa namba za "telex" Tanzania ilipewa "989". Taarifa ya mkutano huo imo kwenye ripoti inayoitwa "Blue Book".

Mkutano uliofuata wa Septemba 23 hadi Oktoba 25, 1968 uliipa Zanzibar namba ya simu "259". Ndugu Cromarty wa Tanzania aliushiriki kama inavyoonyesha ripoti inayoitwa "White Book". Hivyo mtu aliyepiga simu Zanzibar alipaswa sasa aache kutumia namba "255" ya Tanzania atumie "259" ya Zanzibar.

Je kwa nini Zanzibar ilipewa namba yake kama vile ni nchi tofauti na Tanzania? Muungano wetu uliipa dola ya Zanzibar mamlaka kwenye masuala yasiyo ya muungano ambapo teknolojia ya simu haikuwa suala la muungano.

Kwa kuwa "telegraph" ndiyo iliyokuwa suala la muungano, Zanzibar haikupewa namba ya "telex" ambayo ni huduma na "telegraph", ikabaki na mamlaka kwa teknolojia tatu zilizobaki yaani televisheni, redio na simu.

Je dola ya Zanzibar ilitumiaje mamlaka yake kwenye televisheni, redio na simu? Tangu siku ya muungano Zanzibar ilibaki na redio yake. Mwaka 1974 ilianzisha televisheni yake. Kitu ambacho haikukifanya ni kuweka teknolojia inayopokea simu zinazoanzwa na "259". Matokeo yake Zanzibar ikaendelea kutumia ya namba ya Tanzania "255".

Simu zetu zote duniani ziko katika ule mfumo "E.164" ambao kwa kirefu unaitwa "ITU-T Recommendation E.164". ITU hutangaza taarifa ya mfumo huu panapotokea mabadiliko ya simu katika nchi yoyote. Taarifa ya Novemba 15, 1995 ilionyesha kwamba "259" ilikuwa bado ni namba ya Zanzibar. Baada ya taarifa hii ITU iliweka viwango vipya kudhibiti matumizi ya namba vilivyoanza kutumika Machi 9, 1998 vikiitwa "E.164.1". Tuone vifungu vitatu ndani ya viwango hivyo yaani kifungu cha 5.13, 5.14 na 6.2.1.

Kifungu cha 5.13 na 5.14 kinasema ITU itanyang'anya namba zote duniani zisizotumika vizuri. Je Zanzibar ilitumia vizuri namba yake "259"? Zanzibar si tu haikuitumia vizuri bali haikuitumia kabisa kwa miaka thelathini. Hivyo Machi 1, 1999 ITU iliinyang'anya Zanzibar hii namba "259" kupitia tangazo "ITU Operational Bulletin No. 687".

Hii maana yake taarifa ile ya Novemba 15, 1995 ilikuwa ya mwisho kuionyesha Zanzibar kama nchi inayotumia namba "259". Hivyo haijulikani kwa nini Masoud anapotosha kwamba "259" bado ni namba ya Zanzibar wakati Zanzibar ilishanyang'anywa namba hiyo tangu mwaka 1999.

Waliohamasishwa na hotuba ya Masoud walitamka palepale wanavyotaka Zanzibar irudishiwe hii namba yake. Je, kurudishiwa huko kunawezekana? Kifungu cha 6.2.1 cha viwango vile kinasema nchi isiyotambulika Umoja wa Mataifa (UN) au ITU haipewi namba. Zanzibar haitambuliki UN wala ITU hivyo haiwezi kupewa namba yoyote.

Uzoefu ulioonekana kabla ya mwaka 1998 unaonyesha kuwa Hong Kong ilibaki na namba yake "+852" ilipoungana na China kama Taiwan ilivyobaki na "+886" ilipoondolewa UN. Kote huko kitendo cha kutotambulika UN kimekuta taifa lilishazoea namba yake, hivyo ITU haikuwanyang'anya.

Kuanzia mwaka 1998 ITU ilizingatia miungano kwa kifungu cha 6.3.2 cha vigezo vile kinachosema nchi zikiungana zitabaki na namba moja tu. Hivyo Hong Kong nayo ingechelewa kama Zanzibar, ingelazimika kutumia namba ya China "+86".

Ukiwa katika sekta ya mawasiliano unalazimika kusoma sana na kutafiti sana kila siku. Wazoefu wa sekta hii wanajua inapotokea fursa unalazimika kuisoma palepale, kuielewa palepale na kuitumia palepale.

Tumeona Zanzibar ilivyopata fursa ya mamlaka kwenye redio, televisheni na simu. Fursa hiyo iliyowaletea televisheni haikutumika kuwaletea teknolojia inayoelekeza simu za namba yao zifike Zanzibar. Kama wangeitumia, basi mwaka 1999 ungekuta namba "259" inatumika hivyo ITU isingewanyang'anya kama Taiwan na Hong Kong.

Hivyo namba "255" siyo ya Tanganyika kama anavyohamasisha Masoud bali ni ya Tanzania. Vilevile "259" siyo namba ya Zanzibar bali ilipewa kihalali mwaka 1968 na ikanyang'anywa kihalali mwaka 1999.
 
So educational ngoja wajuvi waje watupe madini zaidi
 
Unadai Zanzibar ilianzisha televisheni yake 1974! Pia ilipewa code no. yake mwaka 1968 lakini ikanyang'anywa mwaka 1999 kwa vile walishindwa kuitumia hapo hapo unadai Zanzibar haiwezi kurudishiwa hiyo code kwa sababu si mwanachama wa UN,je wakati huo wakipewa walikuwa wanachama wa UN?

Naomba ufafanuzi zaidi.
 
Paragraph ya mwisho ndio ulipoonyesha udhaifu wako!

Ni kitu gani usichoelewa? Kama code 255 ilitolewa tarehe 26 Juni 1964 ni dhahiri kuwa isingeweza kutolewa kwa Tanganyika ambayo ilipotea tarehe 26 Aprili 1964. Zanzibar walipewa namba 259 mwaka 1968 kwa vile masuala ya simu hayakuwemo kwenye masuala ya Muungano. Uamuzi wa kutoitumia hiyo namba kwa zaidi ya miaka 30 ulikuwa wa Zanzibar, sio wa Tanzania. Ilinyang'anywa kwa sababu ya uzembe wao na sio kwa sababu Tanzania haikutaka wawe nayo. Haiwezi kurudishwa kwa vile masharti ya utoaji wa namba hizo umebadilika na sasa hawana sifa ya kupewa hiyo namba. Udhaifu wake uko wapi hapo?

Amandla...
 
Ni kitu gani usichoelewa? Kama code 255 ilitolewa tarehe 26 Juni 1964 ni dhahiri kuwa isingeweza kutolewa kwa Tanganyika ambayo ilipotea tarehe 26 Aprili 1964. Zanzibar walipewa namba 259 mwaka 1968 kwa vile masuala ya simu hayakuwemo kwenye masuala ya Muungano. Uamuzi wa kutoitumia hiyo namba kwa zaidi ya miaka 30 ulikuwa wa Zanzibar, sio wa Tanzania. Ilinyang'anywa kwa sababu ya uzembe wao na sio kwa sababu Tanzania haikutaka wawe nayo. Haiwezi kurudishwa kwa vile masharti ya utoaji wa namba hizo umebadilika na sasa hawana sifa ya kupewa hiyo namba. Udhaifu wake uko wapi hapo?

Amandla...
Mbona Tanganyika Law Society iko hadi leo?!

Tanganyika bado ipo bwashee usihadaike na wanasiasa.

Othman yuko sahihi.
 
Unadai Zanzibar ilianzisha televisheni yake 1974! Pia ilipewa code no. yake mwaka 1968 lakini ikanyang'anywa mwaka 1999 kwa vile walishindwa kuitumia hapo hapo unadai Zanzibar haiwezi kurudishiwa hiyo code kwa sababu si mwanachama wa UN,je wakati huo wakipewa walikuwa wanachama wa UN?
Naomba ufafanuzi zaidi.

Wakati wa analogia, televisheni na simu vilikuwa vitu tofauti. Zanzibar kuwa na televisheni yake hakuhusiani kabisa na kuwa na code yake ya simu. Masharti yaliyokuwepo mwaka 1968 yaliruhusu Zanzibar kupata code yake kwa sababu suala la simu halikuwa katika masuala ya Muungano, uanachama wa UN haukupewa uzito. Mwaka 1998, ITU ilianza kutumia viwango vipya ambavyo vilitaka nchi ambazo hazitumii code yake ipasavyo kunyang'anywa na kutaka code zitolewe kwa nchi ambazo ni wanachama wa UN isipokuwa zile ambazo tayari zilikuwa zinatumia code zake kama Hongkong na Taiwan. Kwa vile Zanzibar ilinyang'anywa kwa kutoitumia basi hii exception haihusu.

Amandla...
 
Ipo lakina haijawa implemented

1630923865294.png
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom