Uongo wa Masoud Othman waumbuliwa. Kadanganya taifa kwamba "+259" ndiyo "Code" ya Zanzibar na "+255" ni ya Tanganyika wakati sivyo

Paschal Mayalla anahusika vipi na suaka hili.

Ndugu Paschal Mayala, Unatuzingua wazenji, Utumbu usituletee na kuitwa kiongozi wetu muongo halikubaliki. Sisi wazenji tuna mila na desturi zetu na kuna lugha ya kutumia ambayo haileti hisia za chuki. Mwandishi wa nakala hii na mletaji wake ni watu dhaifu sana. Ni watu wenye chuki na ubaya wa roho juu ya zanzibar. Kwa ufupi wazanzibari wamechoka kuhusu kero za muungano na usanii wa viongozi watanzania. The first opportunity we get, we'll be out of this UNION."
 
Unampaje sifa mleta mada kwa article aliyoikopi gazetini na kutuletea humu.

Tena bahati nzuri ina jina na contact za mtafiti.
Aaah kumbe! Tunaita plagiarism!

Ila siku moja jamaa alichapisha thread yangu ya humu Jamii Forum kwenye gazeti la Mwananchi bwana, na akaweka jina lake bila hata kusema ameichukua toka thread ya Jamii Forum! Anyway, kwa kuwa ilisaidia watu wengi zaidi kupata ujumbe niliotoa sikuona ni tatizo. Thread yenyewe aliyoichukua na kuchapisha Mwananchi kama makala yake hii hapa chini;

Huyu mwandishi wa Mwananchi Juma Bakari kaamua kukopi uzi wangu kwenye JF na kuuchaopisha gazetini bila hata kusema kaitoa hiyo habari JF!
 
TITLE: UKWELI KUHUSU NAMBA YA SIMU YA KIMATAIFA "+259"
ANALYST: JOSEPH MAGATA
Cell: +255 75 4710684
PUBLICATION: RAIA MWEMA, pg. 12

Juni 8, mwaka huu Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman Masoud alitoa hotuba ambayo sehemu ninayoinukuu anasema,

"Kwenye serikali hiihii ambayo tumekuwa nayo ndiyo vikwazo vya kila aina, miye nawapa kimoja tu kwa mfano.Tulipoanza simu, zile zilisosajiliwa Bara, TRITEL, sijui nani, walipewa leseni mara moja. Ilipokuja ZANTEL ikasajiliwa Zanzibar. Kosa lake kusajiliwa Zanzibar. Ukawa ugomvi, ikawa vita vikubwa kwelikweli".

"Mpaka tukafika Geneva kwenye Shirika la Simu duniani, ITU, kwenda kusuluhishwa na baada ya kutishia kwamba tutakwenda kudai namba yetu 259." Maana hii tunayoitumia leo, "255" ni ya Tanganyika, ya Zanzibar ambayo mpaka leo hii ipo hajapewa mtu mwingine ni "259". Na ilibidi kwenda (ITU) kutishia kuidai ile namba kwa sababu wenzetu wamekataa kutupa leseni".

Je ITU walikoenda Masoud na wenzake wa Zanzibar ina majukumu gani?

Teknolojia ya "telegraph" iliyovumbuliwa mwaka 1837 ilitoa huduma za kutuma maandishi (telegram), kutuma pesa (moneygram) na baadaye "telex". Hivyo mwaka 1865 ITU ikaundwa ikiitwa "International Telegraph Union" kusimamia viwango vya teknolojia hii.

Mwaka 1876 teknolojia ya simu nayo ikavumbuliwa, kisha ikafuata ya redio na baadaye ya televisheni. Kufikia mwaka 1934 zikawepo teknolojia hizi nne, redio, "telegraph", simu na televisheni. Japo ITU ilianzishwa kusimamia "telegraph" ikajikuta inasimamia na hizi tatu, hivyo ikaitwa "International Telecommunication Union".

Teknolojia ya simu iliposambaa ilikosa mfumo unaofanana wa simu zinazoenda nje ya nchi, kila nchi iliunda wake. ITU ikaunda mfumo unaoitwa sasa "E.164" wa nchi kuwa na namba ya simu. Hivyo ITU ilipokutana Mei 25 hadi Juni 26, 1964 ilizipa nchi 129 namba za simu, ikiwemo Tanzania iliyopewa namba "255". Mkutano huo ulipogawa namba za "telex" Tanzania ilipewa "989". Taarifa ya mkutano huo imo kwenye ripoti inayoitwa "Blue Book".

Mkutano uliofuata wa Septemba 23 hadi Oktoba 25, 1968 uliipa Zanzibar namba ya simu "259". Ndugu Cromarty wa Tanzania aliushiriki kama inavyoonyesha ripoti inayoitwa "White Book". Hivyo mtu aliyepiga simu Zanzibar alipaswa sasa aache kutumia namba "255" ya Tanzania atumie "259" ya Zanzibar.

Je kwa nini Zanzibar ilipewa namba yake kama vile ni nchi tofauti na Tanzania? Muungano wetu uliipa dola ya Zanzibar mamlaka kwenye masuala yasiyo ya muungano ambapo teknolojia ya simu haikuwa suala la muungano.

Kwa kuwa "telegraph" ndiyo iliyokuwa suala la muungano, Zanzibar haikupewa namba ya "telex" ambayo ni huduma na "telegraph", ikabaki na mamlaka kwa teknolojia tatu zilizobaki yaani televisheni, redio na simu.

Je dola ya Zanzibar ilitumiaje mamlaka yake kwenye televisheni, redio na simu? Tangu siku ya muungano Zanzibar ilibaki na redio yake. Mwaka 1974 ilianzisha televisheni yake. Kitu ambacho haikukifanya ni kuweka teknolojia inayopokea simu zinazoanzwa na "259". Matokeo yake Zanzibar ikaendelea kutumia ya namba ya Tanzania "255".

Simu zetu zote duniani ziko katika ule mfumo "E.164" ambao kwa kirefu unaitwa "ITU-T Recommendation E.164". ITU hutangaza taarifa ya mfumo huu panapotokea mabadiliko ya simu katika nchi yoyote. Taarifa ya Novemba 15, 1995 ilionyesha kwamba "259" ilikuwa bado ni namba ya Zanzibar. Baada ya taarifa hii ITU iliweka viwango vipya kudhibiti matumizi ya namba vilivyoanza kutumika Machi 9, 1998 vikiitwa "E.164.1". Tuone vifungu vitatu ndani ya viwango hivyo yaani kifungu cha 5.13, 5.14 na 6.2.1.

Kifungu cha 5.13 na 5.14 kinasema ITU itanyang'anya namba zote duniani zisizotumika vizuri. Je Zanzibar ilitumia vizuri namba yake "259"? Zanzibar si tu haikuitumia vizuri bali haikuitumia kabisa kwa miaka thelathini. Hivyo Machi 1, 1999 ITU iliinyang'anya Zanzibar hii namba "259" kupitia tangazo "ITU Operational Bulletin No. 687".

Hii maana yake taarifa ile ya Novemba 15, 1995 ilikuwa ya mwisho kuionyesha Zanzibar kama nchi inayotumia namba "259". Hivyo haijulikani kwa nini Masoud anapotosha kwamba "259" bado ni namba ya Zanzibar wakati Zanzibar ilishanyang'anywa namba hiyo tangu mwaka 1999.

Waliohamasishwa na hotuba ya Masoud walitamka palepale wanavyotaka Zanzibar irudishiwe hii namba yake. Je, kurudishiwa huko kunawezekana? Kifungu cha 6.2.1 cha viwango vile kinasema nchi isiyotambulika Umoja wa Mataifa (UN) au ITU haipewi namba. Zanzibar haitambuliki UN wala ITU hivyo haiwezi kupewa namba yoyote.

Uzoefu ulioonekana kabla ya mwaka 1998 unaonyesha kuwa Hong Kong ilibaki na namba yake "+852" ilipoungana na China kama Taiwan ilivyobaki na "+886" ilipoondolewa UN. Kote huko kitendo cha kutotambulika UN kimekuta taifa lilishazoea namba yake, hivyo ITU haikuwanyang'anya.

Kuanzia mwaka 1998 ITU ilizingatia miungano kwa kifungu cha 6.3.2 cha vigezo vile kinachosema nchi zikiungana zitabaki na namba moja tu. Hivyo Hong Kong nayo ingechelewa kama Zanzibar, ingelazimika kutumia namba ya China "+86".

Ukiwa katika sekta ya mawasiliano unalazimika kusoma sana na kutafiti sana kila siku. Wazoefu wa sekta hii wanajua inapotokea fursa unalazimika kuisoma palepale, kuielewa palepale na kuitumia palepale.

Tumeona Zanzibar ilivyopata fursa ya mamlaka kwenye redio, televisheni na simu. Fursa hiyo iliyowaletea televisheni haikutumika kuwaletea teknolojia inayoelekeza simu za namba yao zifike Zanzibar. Kama wangeitumia, basi mwaka 1999 ungekuta namba "259" inatumika hivyo ITU isingewanyang'anya kama Taiwan na Hong Kong.

Hivyo namba "255" siyo ya Tanganyika kama anavyohamasisha Masoud bali ni ya Tanzania. Vilevile "259" siyo namba ya Zanzibar bali ilipewa kihalali mwaka 1968 na ikanyang'anywa kihalali mwaka 1999.
Angalia hii: na hata kabla ya hii kulikuwa na code tafauti kupiga Zanzibar. sisi watu wazamani tunajuwa.
Kama upo Zanzibar unataka kupiga bara au mikoani kulikuwa na code. nakama upo bara ukitaka kupiga Zanzibar una piga.
Hiyo Code ipo na unassigned mpaka leo.
Pia kuna Radio frequensy za FM za zanzibar zinatumiwa na CCM na AM wanazo na shortwave wanazo.

Two Channel za TV zimechukuliwa na TBC

Changes in the 1968 CCITT White Book... the list was then titled Recommendation E.161 / Q.11. Changes listed in order of country code:

+1 - Antigua (territory added)
- Barbados (territory added)
- British Virgin Islands (territory added)
- Cayman Islands (territory added)
- Dominica (territory added)
- Grenada (territory added)
- Montserrat (territory added)
- St Kitts (territory added)
- St Lucia (territory added)
- St Pierre & Miquelon (territory added)
- St Vincent (territory added)
x Guatemala (CHANGED to country code +500)
x Mexico (CHANGED to country code +52)
x Netherlands Antilles (CHANGED to country code +599)
+240 - Equatorial Guinea (NEW)
+243 - Congo (Dem. Rep. of the) (Name change)
+259 - Zanzibar (NEW)
+260 - Zambia (Name Change)
+263 - Rhodesia (Name Change)
+266 - Lesotho (Name Change)
+267 - Botswana (Name Change)
+269 - Comoro Islands (Name Change)
+355 - Albania (NEW - changed from +405)
+358 - Finland (NEW - changed from +401)
+359 - Bulgaria (NEW - changed from +403)
+36 x Turkey (CHANGED to +90)
+36 - Hungary (NEW - changed from +402)
+37 - East Germany (added - announced in ITU Notification #980 of
10 March 1966)
+40 - Romania (NEW - changed from +404)
+500 - Guatemala (NEW - changed from +1)
+52 - Mexico (NEW - changed from +1)
+599 - Netherlands Antilles (NEW - changed from +1)
+65 - Singapore (NEW - became independent of Malaysia +60 code)
+681 - Wallis and Futuna (NEW)
+686 - Gilbert & Ellice Islands (NEW)
+90 - Turkey (NEW - changed from +36)
+968 - Sultanate of Muscat & Oman (NEW)
+969 - Southern Yemen (Name Change)
+971 - Trucial States (NEW)
+973 - Bahrain (NEW)
+974 - Qatar (NEW)
 
Wakati wa analogia, televisheni na simu vilikuwa vitu tofauti. Zanzibar kuwa na televisheni yake hakuhusiani kabisa na kuwa na code yake ya simu. Masharti yaliyokuwepo mwaka 1968 yaliruhusu Zanzibar kupata code yake kwa sababu suala la simu halikuwa katika masuala ya Muungano, uanachama wa UN haukupewa uzito. Mwaka 1998, ITU ilianza kutumia viwango vipya ambavyo vilitaka nchi ambazo hazitumii code yake ipasavyo kunyang'anywa na kutaka code zitolewe kwa nchi ambazo ni wanachama wa UN isipokuwa zile ambazo tayari zilikuwa zinatumia code zake kama Hongkong na Taiwan. Kwa vile Zanzibar ilinyang'anywa kwa kutoitumia basi hii exception haihusu.

Amandla...
Lakini mpaka sasa hiyo code unassigned
 
Lakini mpaka sasa hiyo code unassigned
Ndio. Zanzibar wakiitaka wanaweza kuiomba pale watakapotimiza masharti. Njia rahisi kwa wao kuipata ni kuvunja Muungano halafu wakaiomba kama nchi iliyo mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Haiwezi kupatikana ndani ya Muungano.

Amandla...
 
Sio namba tuu, Tanzania ni Tanganyika kuanzia bendera na kila kitu. In practice Tanganyika imeivamia Zanzibar na kujiongezea mipaka (nukuu ya katiba ya Tanganyika ndio inavyosema Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika).

Najua watanganyika watanuna, lakini practical translation ya muungano wetu hauna tofauti na ukoloni period.
 
TITLE: UKWELI KUHUSU NAMBA YA SIMU YA KIMATAIFA "+259"
ANALYST: JOSEPH MAGATA
Cell: +255 75 4710684
PUBLICATION: RAIA MWEMA, pg. 12

Juni 8, mwaka huu Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman Masoud alitoa hotuba ambayo sehemu ninayoinukuu anasema,

"Kwenye serikali hiihii ambayo tumekuwa nayo ndiyo vikwazo vya kila aina, miye nawapa kimoja tu kwa mfano.Tulipoanza simu, zile zilisosajiliwa Bara, TRITEL, sijui nani, walipewa leseni mara moja. Ilipokuja ZANTEL ikasajiliwa Zanzibar. Kosa lake kusajiliwa Zanzibar. Ukawa ugomvi, ikawa vita vikubwa kwelikweli".

"Mpaka tukafika Geneva kwenye Shirika la Simu duniani, ITU, kwenda kusuluhishwa na baada ya kutishia kwamba tutakwenda kudai namba yetu 259." Maana hii tunayoitumia leo, "255" ni ya Tanganyika, ya Zanzibar ambayo mpaka leo hii ipo hajapewa mtu mwingine ni "259". Na ilibidi kwenda (ITU) kutishia kuidai ile namba kwa sababu wenzetu wamekataa kutupa leseni".

Je ITU walikoenda Masoud na wenzake wa Zanzibar ina majukumu gani?

Teknolojia ya "telegraph" iliyovumbuliwa mwaka 1837 ilitoa huduma za kutuma maandishi (telegram), kutuma pesa (moneygram) na baadaye "telex". Hivyo mwaka 1865 ITU ikaundwa ikiitwa "International Telegraph Union" kusimamia viwango vya teknolojia hii.

Mwaka 1876 teknolojia ya simu nayo ikavumbuliwa, kisha ikafuata ya redio na baadaye ya televisheni. Kufikia mwaka 1934 zikawepo teknolojia hizi nne, redio, "telegraph", simu na televisheni. Japo ITU ilianzishwa kusimamia "telegraph" ikajikuta inasimamia na hizi tatu, hivyo ikaitwa "International Telecommunication Union".

Teknolojia ya simu iliposambaa ilikosa mfumo unaofanana wa simu zinazoenda nje ya nchi, kila nchi iliunda wake. ITU ikaunda mfumo unaoitwa sasa "E.164" wa nchi kuwa na namba ya simu. Hivyo ITU ilipokutana Mei 25 hadi Juni 26, 1964 ilizipa nchi 129 namba za simu, ikiwemo Tanzania iliyopewa namba "255". Mkutano huo ulipogawa namba za "telex" Tanzania ilipewa "989". Taarifa ya mkutano huo imo kwenye ripoti inayoitwa "Blue Book".

Mkutano uliofuata wa Septemba 23 hadi Oktoba 25, 1968 uliipa Zanzibar namba ya simu "259". Ndugu Cromarty wa Tanzania aliushiriki kama inavyoonyesha ripoti inayoitwa "White Book". Hivyo mtu aliyepiga simu Zanzibar alipaswa sasa aache kutumia namba "255" ya Tanzania atumie "259" ya Zanzibar.

Je kwa nini Zanzibar ilipewa namba yake kama vile ni nchi tofauti na Tanzania? Muungano wetu uliipa dola ya Zanzibar mamlaka kwenye masuala yasiyo ya muungano ambapo teknolojia ya simu haikuwa suala la muungano.

Kwa kuwa "telegraph" ndiyo iliyokuwa suala la muungano, Zanzibar haikupewa namba ya "telex" ambayo ni huduma na "telegraph", ikabaki na mamlaka kwa teknolojia tatu zilizobaki yaani televisheni, redio na simu.

Je dola ya Zanzibar ilitumiaje mamlaka yake kwenye televisheni, redio na simu? Tangu siku ya muungano Zanzibar ilibaki na redio yake. Mwaka 1974 ilianzisha televisheni yake. Kitu ambacho haikukifanya ni kuweka teknolojia inayopokea simu zinazoanzwa na "259". Matokeo yake Zanzibar ikaendelea kutumia ya namba ya Tanzania "255".

Simu zetu zote duniani ziko katika ule mfumo "E.164" ambao kwa kirefu unaitwa "ITU-T Recommendation E.164". ITU hutangaza taarifa ya mfumo huu panapotokea mabadiliko ya simu katika nchi yoyote. Taarifa ya Novemba 15, 1995 ilionyesha kwamba "259" ilikuwa bado ni namba ya Zanzibar. Baada ya taarifa hii ITU iliweka viwango vipya kudhibiti matumizi ya namba vilivyoanza kutumika Machi 9, 1998 vikiitwa "E.164.1". Tuone vifungu vitatu ndani ya viwango hivyo yaani kifungu cha 5.13, 5.14 na 6.2.1.

Kifungu cha 5.13 na 5.14 kinasema ITU itanyang'anya namba zote duniani zisizotumika vizuri. Je Zanzibar ilitumia vizuri namba yake "259"? Zanzibar si tu haikuitumia vizuri bali haikuitumia kabisa kwa miaka thelathini. Hivyo Machi 1, 1999 ITU iliinyang'anya Zanzibar hii namba "259" kupitia tangazo "ITU Operational Bulletin No. 687".

Hii maana yake taarifa ile ya Novemba 15, 1995 ilikuwa ya mwisho kuionyesha Zanzibar kama nchi inayotumia namba "259". Hivyo haijulikani kwa nini Masoud anapotosha kwamba "259" bado ni namba ya Zanzibar wakati Zanzibar ilishanyang'anywa namba hiyo tangu mwaka 1999.

Waliohamasishwa na hotuba ya Masoud walitamka palepale wanavyotaka Zanzibar irudishiwe hii namba yake. Je, kurudishiwa huko kunawezekana? Kifungu cha 6.2.1 cha viwango vile kinasema nchi isiyotambulika Umoja wa Mataifa (UN) au ITU haipewi namba. Zanzibar haitambuliki UN wala ITU hivyo haiwezi kupewa namba yoyote.

Uzoefu ulioonekana kabla ya mwaka 1998 unaonyesha kuwa Hong Kong ilibaki na namba yake "+852" ilipoungana na China kama Taiwan ilivyobaki na "+886" ilipoondolewa UN. Kote huko kitendo cha kutotambulika UN kimekuta taifa lilishazoea namba yake, hivyo ITU haikuwanyang'anya.

Kuanzia mwaka 1998 ITU ilizingatia miungano kwa kifungu cha 6.3.2 cha vigezo vile kinachosema nchi zikiungana zitabaki na namba moja tu. Hivyo Hong Kong nayo ingechelewa kama Zanzibar, ingelazimika kutumia namba ya China "+86".

Ukiwa katika sekta ya mawasiliano unalazimika kusoma sana na kutafiti sana kila siku. Wazoefu wa sekta hii wanajua inapotokea fursa unalazimika kuisoma palepale, kuielewa palepale na kuitumia palepale.

Tumeona Zanzibar ilivyopata fursa ya mamlaka kwenye redio, televisheni na simu. Fursa hiyo iliyowaletea televisheni haikutumika kuwaletea teknolojia inayoelekeza simu za namba yao zifike Zanzibar. Kama wangeitumia, basi mwaka 1999 ungekuta namba "259" inatumika hivyo ITU isingewanyang'anya kama Taiwan na Hong Kong.

Hivyo namba "255" siyo ya Tanganyika kama anavyohamasisha Masoud bali ni ya Tanzania. Vilevile "259" siyo namba ya Zanzibar bali ilipewa kihalali mwaka 1968 na ikanyang'anywa kihalali mwaka 1999.
Huyo masoud siyo mtu rafiki na muungano. Kama 255 ni namba ya tanganyika na 259 ni ya zanzibar atuambie ya tanzania ni ngapi. Maana wenye kuweka hizo namba wanaonyesha 255 ni ya tanzania.
 
Back
Top Bottom