Uongo wa dini za kihuni za Mashariki ya Kati(Middle East)

Mbona umeeongelea zaidi Afrika. Hujui hizi dini zimesambaa dunia nzima mpaka China na huko Japan? Je,huko napo kuna waafrika?!!!!
Huko waumini wa dini hizi ni wachache sana wana dini zao huko kama Hinduism, Jainism, Buddhism, Tao, Shinto n.k Islamic and Christian ni asilimia 3%na 4 %kwa India na China.
 
Mkuu tujuze Wewe unaamini kama Mungu yupo au unaamini katika Mwingu?
Je Dini ipi ya Kiafrika unayo ikubali?

Je sababu zipi zilikufanya kutoamini Dini zilizo anzia huko middle East?
Hajasema Mungu hayupo, ila hakubaliani na ujinga wa mavitabu yenu yaliyoletwa kwenye majahazi, hizo ni riwaya tu
 
Waafrika tuliacha majina yetu ya asili tukachukua majina ya wageni. Tembea dunia nzima huwezi kuta mzungu anaitwa masawe au mkude.

Nirudi kwenye mada, hata mimi huwa najiuliza sana afrika hatukua na dini zetu?
Mtemi Mwanamalundi alikuwa ni Nabii huko usukumani, kama historia yake ingeshikiliwa vema, ile ilikuwa ni dini kabisa ya watu wa pande hizo kwani alitenda miujiza kibao, ingekuwa mashariki ya kati tayari angekuwa ameandikwa kwenye mavitabu yao kama nabii, ila tukatiwa ujinga na hao wazungu na waarabu tukadharau vyetu vikaitwa vya kishenzi nasi tukaiga upuuzi wao tumepotea sasa tunachinjana hivyo mara Alshabaab, mara Antibalaka na mengineyo ni ujinga wa kudharau imani za mababu zetu na sasa we are paying the price
 
Uchawi haupo ndio sasa unapobisha na kusema upo bila kututhibitishia inaonesha kuwa ata hiyo Dini yako ya kiafrica ina mambo kibao ya uongo
Nyie mmekuwa brainwashed na watu weupe, we ulishasikia mwarabu au muisrael au mzungu akaitwa Kimaro, Masanja, Mwakaleli au Byarubaga? kwa nn tuendelee kuwa watumwa wa hawa watu waovu kwa kivuli cha dini?
 
Wewe ndie umeleta neno shetani
Niambie maana yake nini/shetani ni nani na ameandikwa wapi
Ubishi usio na lazima hauna maana,sio kwamba mie ndio nimeleta bali nimetumia neno la kiswahili lenye kutumika katika maongezi yetu ya kila siku na si kwamba ni neno jipya au gumu kueleweka ndiyo maana nikasema hulijui basi.
 
Ubishi usio na lazima hauna maana,sio kwamba mie ndio nimeleta bali nimetumia neno la kiswahili lenye kutumika katika maongezi yetu ya kila siku na si kwamba ni neno jipya au gumu kueleweka ndiyo maana nikasema hulijui basi.
Nimekuelewa kuwa umeandika neno usilolijua
 
Walikuwa wanaomba Mungu kupitia msaada na maombi ya waliotangulia ili kuweka uzito wa maombi. Dini ipi haiombi kwa kuhusisha walikufa? Wanaposema kwa jina la Yesu wanamaana gani?. Neno mzimu wametoa ila ukweli ni kupitia mzimu wa Yesu.
Ahsante sana kwa kunifungua macho
Nalog off
 
Back
Top Bottom