Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Mara nyingi sana nimewasikia Wakenya pindi wakumbwapo na baa la njaa wakijitetea kwamba nchi yao ni Jangwa hivyo haina ardhi ya kutosha kulima na ndiyo maana wanashida ya chakula, huu ni uongo na upotoshaji mkubwa!
Nchi ya Kenya ina km za mraba zaidi ya 580 000 (km²) na watu zaidi ya milioni 40 tu, hivyo kukosa sehemu kulima chakula cha kutosha watu milioni 40 tu ndani ya nchi yenye zaidi ya km² laki tano na themanini ni UONGO na ni maajabu ya Dunia!
Ikumbukwe kwamba nchi ya Kenya imepitiwa na Bonde la Ufa na hii ni moja kati ya sehemu zenye rutuba kuliko zote hapa Afrika sasa iweje wakose chakula?
Ukweli ni kwamba nchi ya Kenya inakuwa na uhaba wa chakula siyo kwa kukosa ardhi ya kulima kwa sababu ya Jangwa la hasha, bali sehemu kubwa ya ardhi yao inayofaa kwa kilimo inahodhiwa na Wanasiasa na Wazungu ambao wameiweka tu na hawalimi chochote hiyo ndiyo sababu na watu wa chini na masikini wameachiwa Turkana, ndiyo maana chakula siku zote hakitoshi!