Nadir Naimuor
Member
- Sep 13, 2020
- 15
- 15
Kumekuwa na mchango wa shilingi elfu 10 kwa kila kaya ambayo imeelezwa na wadai kuwa ni fedha zinazo changishwa kwa ajili ya kujenga shule ya kata nyamplukano shida sio wananchi kuchangia maendeleo yao hapana, tatizo ni force inayotumika kukusanya michango hiyo.
Mwenyekiti ajulikanae kwa jina la Jeni Msoga anazunguka na migambo kukusanya michango hiyo na ni lazima utoe elfu 15 elfu 10 mchango elfu 5 usumbufu na kama mtu hana anakamatwa na mgambo na kupelekwa office ya mtendaji wa kata na kufungiwa ndani na anawekwa chini ya ulinzi wa mtendaji na migambo wake.
Hii sio sawa kabisa nchi yetu ina sheria ambazo hutungwa bungeni na kusainiwa na mhe Rais hivyo wanao husika likemeeni hili kabla amani haijapotea hapa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza hususani kata ya Nyamplukano hakuna anae kataa kushiriki kwenye swala la maendeleo.