Uonevu unaofanywa na Wenyeviti wa Mtaa na Mtendaji wa Kata ya Nyamlukano wilaya ya Sengerema

Nadir Naimuor

Member
Sep 13, 2020
15
15
Kumekuwa na mchango wa shilingi elfu 10 kwa kila kaya ambayo imeelezwa na wadai kuwa ni fedha zinazo changishwa kwa ajili ya kujenga shule ya kata nyamplukano shida sio wananchi kuchangia maendeleo yao hapana, tatizo ni force inayotumika kukusanya michango hiyo.

Mwenyekiti ajulikanae kwa jina la Jeni Msoga anazunguka na migambo kukusanya michango hiyo na ni lazima utoe elfu 15 elfu 10 mchango elfu 5 usumbufu na kama mtu hana anakamatwa na mgambo na kupelekwa office ya mtendaji wa kata na kufungiwa ndani na anawekwa chini ya ulinzi wa mtendaji na migambo wake.

Hii sio sawa kabisa nchi yetu ina sheria ambazo hutungwa bungeni na kusainiwa na mhe Rais hivyo wanao husika likemeeni hili kabla amani haijapotea hapa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza hususani kata ya Nyamplukano hakuna anae kataa kushiriki kwenye swala la maendeleo.
 
Hao wenyeviti ni makada wa CCM waliokwaa madaraka kwa njia haramu kwahiyo haramu kwao
ni nyumbani
 
Mkuu sija soma kichwa cha habari bali nimeangalia kichwa cha habari, napenda watanzania wote na kuwaheshim, napenda nchi yangu,
Hivyo mungu anisamehe kwa nitakalo sema chini Hapa natubu mapema.

Mkuu, Kuna watu wamezidi kuwazoea wananchi ambao ndo wenye nchi, Kama mbwai mbwai ,WABONDENI pia, WAWE NA ADABU ,Mungu nisamehe ila binadam uliotuumba tunafanya unyama kwa binadam wenzetu,Kama vile yupo mwenye passport yakuja kwako ,
 
Kumekuwa na mchango wa shilingi elfu 10 kwa kila kaya ambayo imeelezwa na wadai kuwa ni fedha zinazo changishwa kwa ajili ya kujenga shule ya kata nyamplukano shida sio wananchi kuchangia maendeleo yao hapana, tatizo ni force inayotumika kukusanya michango hiyo...
toa pesa kijana acha kulalamika,

mwenyekiti na huyo mtendaji wanatekeleza maagizo/maazimio mliyowaagiza kwenye mkutano mkuu, mchango huo mlikubaliana na sio maamuzi binafsi ya mtendaji na huyo mwenyekiti
 
Tumefikia hatua hata ya kuoneana huruma inaonekana kuwa ni ujinga.

Kuwaonea huruma watu kama hao wa Kata ya Nyamlukano ifike mahala ionekane kuwa ni upumbavu! Inaudhi.
 
Nyamlukano mnyukano mpambano n Kama vituvinavyoendana vilee mleta mada hujaona shida ipo sehemu? Badilishen jina labda mtapata Aman
 
toa pesa kijana acha kulalamika,
mwenyekiti na huyo mtendaji wanatekeleza maagizo/maazimio mliyowaagiza kwenye mkutano mkuu, mchango huo mlikubaliana na sio maamuzi binafsi ya mtendaji na huyo mwenyekiti
Hoja sio kutoa pesa maalim ni wapi mwenyekiti wa mtaa na mtendaji wanapata nguvu ya kukamata wananchi na kwenda kuwafungia kwenye office ya mtendaji kama mahabusu sheria ya wapi hii
 
Hoja sio kutoa pesa maalim ni wapi mwenyekiti wa mtaa na mtendaji wanapata nguvu ya kukamata wananchi na kwenda kuwafungia kwenye office ya mtendaji kama mahabusu sheria ya wapi hii
huo mchango ni makubaliano ya wananchi na mtekelezaji wa kukusanya ni mtendaji na mwenyekiti.

wasipokusanya huoni kama wananchi watawaona viongozo hao hawawajibiki.

kama wewe ndio mwenyekiti wananchi waliokaidi kuchangia ungefanyeje?

msiwe mnachagua watu na kuwajalibu
 
Kumekuwa na mchango wa shilingi elfu 10 kwa kila kaya ambayo imeelezwa na wadai kuwa ni fedha zinazo changishwa kwa ajili ya kujenga shule ya kata nyamplukano shida sio wananchi kuchangia maendeleo yao hapana, tatizo ni force inayotumika kukusanya michango hiyo.

Mwenyekiti ajulikanae kwa jina la Jeni Msoga anazunguka na migambo kukusanya michango hiyo na ni lazima utoe elfu 15 elfu 10 mchango elfu 5 usumbufu na kama mtu hana anakamatwa na mgambo na kupelekwa office ya mtendaji wa kata na kufungiwa ndani na anawekwa chini ya ulinzi wa mtendaji na migambo wake.

Hii sio sawa kabisa nchi yetu ina sheria ambazo hutungwa bungeni na kusainiwa na mhe Rais hivyo wanao husika likemeeni hili kabla amani haijapotea hapa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza hususani kata ya Nyamplukano hakuna anae kataa kushiriki kwenye swala la maendeleo.
Sio huko tu,viongozi wa serikali za kitaa,ni Kama miungu watu,Kuna sehemu moja geita,nilienda kutoa taarifa za wizi wa vifaa vya mnara wa simu,
Mkuu wa kata,WEO,akaitisha mkutano,vijana wanaoisiwa kuwa wezi wakakamatwa,walikula fimbo mpaka huruma,mmoja,alitoroka,wakatumwa,mgambo wakamchukue mke wake,hako kabinti,kalipigwa fimbo kwenye magoti na miguu,Ili kaseme,mume wake kaficha wapi vitu.
Hicho Kijiji,ukifsnya kosa,unapigwa faini ya mbuzi,au Ngombe,anachinjwa,na viongozi wa kiume ndio wanakula nyama,
Huyo Katibu kata,anaogopwa anaitwa Trump,kwa ukatiri wake

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom