Uonevu Mkubwa Tarime.....Barua Ya Wazi Kwa JOHN Magufuli ..... SerikaliYa JK Mko Wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uonevu Mkubwa Tarime.....Barua Ya Wazi Kwa JOHN Magufuli ..... SerikaliYa JK Mko Wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Mar 4, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Sisi wakazi wa sirari na wilaya ya tarime kwa ujumla tumepatwa na tatizo la bomoa bomoa na zoezi hili limeanza 2march mwaka huu baada ya tangazo la kupewa siku saba tuwe tumebomoa makazi yetu pasipo fidia yoyote,naamini mnajua ugumu wa maisha uliyo kwa sasa .Hawa wakubwa wanatumia umasikini wetu na uelewa mdogo tulionao kutunyanyasa kwa kutumia mabafu kuvunja nyumba zetu na kutufanya tuwe wakimbizi ndani ya nchi yetu,kibaya zaidi wanaziacha nyumba za viongozi wetu kama madiwani na baadhi ya maafisa .Ombi letu ni kuwaomba ndugu zetu wenye uelewa wa haya mambo mtusaidie na kikubwa zaidi tutafurahi ujumbe wetu huu ukiwafikia wakubwa hata kwa njia ya blog zetu na kokote pale mnapokutana nao ili wajue kwamba ,vijana wao wanaosimamia zoezi hili hawatutendei haki na kama kuna fedha ziliwahi kutolea na serikali kufidia hasara hizi kwa raia basi hawa watu waoa watakuwa wamekula na kinachofanyika sasa ni kutimiza wajibu wao kwa kunyanyasa rai.Tunaomba msaada wenu kutuwekea file tuliloambatanisha kwenye hii thread muisambaze ili wakizipitia walione na raia wote wapenda haki wajue kuwa kuna ndugu zao wanateseka huku vijijini.kama mtaguswa mnaweza kutufikishia ujumbe wetu kwa wahusika pia. Samahani tumewatumia nyie kama kaka zetu na kwa kuwa tunatambua msaada wenu katika kutetea hazi zetu,tuliowanyonge.Aksanteni

  attachment

  View attachment 24321
   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  ujinga kichwani sishangai

  serikalii hii waliojaa
   
 3. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Duh! Jamani poleni ila hawa jamaa wamezidi, uonevu wa jinsi hii af watu wasiandamane. Jamani watalaamu wa sheria Jf wasaidieni hawa ndugu zetu
   
 4. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ......ngoja nihabarike zaidi kuhusu hili
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Poleni sana mkuu na wote mliokumbwa na masahibu haya, serikali ya kulindana taabu tupu!!!
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ''...kutumia mabafu kuvunja nyumba zetu na kutufanya tuwe wakimbizi ndani ya nchi yetu....'' Ukuryani huko.
  Poleni sana!
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ndugu wananchi wa Tarime

  Kama mnazo hati halali za umiliki wa nyumba zenu na mmekuwa mkilipa kodi ya ardhi na majengo
  katika halmashauri na pia kama hamjawahi kupewa fidia yeyote ya nyumba zenu.

  Mnachotakiwa kufanya kwanza ni kujikusanya nyote mkawa kitu kimoja. Umoja ni nguvu. Halafu baada ya hapo
  ni kumtafuta mwanasheria. Mkishampata mwanasheria atakwenda mahakamani kuweka Court Injuction. Akishaweka CI
  bomoa bomoa itasitishwa, halafu atafungua kesi ya msingi. Kama kweli mna haki basi mahakama itaamua mtalipwa fidia
  kulingana na sheria na taratibu za nchi huu ndio ushauri wangu. Mimi nilishaona ukifanya kazi.
   
Loading...