Uonevu huu unaoendelea katika shamba la mpunga Ex-NAFCO DAKAWA hauvumiliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uonevu huu unaoendelea katika shamba la mpunga Ex-NAFCO DAKAWA hauvumiliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Feb 20, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Shamba la Mpunga Ex-NAFCO Dakawa liko katika Wilaya ya Mvomero.Ni shamba lililo kuwa zuri na lililokuwa linazalisha vizuri, lakini ufisadi ndio ulio liua shamba hili pamoja na mashamba mengine yaliyokuwa yanamilikiwa na NAFCO.Hatimaye shamba hili lilikabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mvomero,lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida,uongozi wa juu kabisa wa Wilaya ukawa sehemu ya tatizo la shamba hili.

  Ugawaji mbaya wa maeneo,ukipendelea hasa viongozi mbalimbali wa serikali na matajiri kutoka mjini Morogoro,Dar es salaam na hata Dodoma na Mwanza umekuwa ndio utendaji wa kawaida wa awamu mbali mbali za uongozi wa shamba hili.Katika siku hizi za karibuni hali hii imekuwa mbaya zaidi.Wanachi wengi wamenyang'anywa mashamba yao bila aibu,huku wakipewa viongozi wa serikali na matajiri kwa kutoa rushwa.Wananchi hawa walionyang'anywa mashamba yao wamesogezwa mbali sehemu ambayo hata miundo mbinu ya maji hakuna.

  Katika hali ya kibinadamu na uungwana,kipaumbele kilipashwa kuwa kwa wakulima wadogo wadogo,kwa sababu hawa ndio tunaotaka kuwaondolea umaskini.Millenium Challenge Corporation core manadate ni kupunguza umaskini katika nchi maskini sana duniani through sustainable economic growth,ili ikifika 2015 watu wanaopata chini ya dola moja kwa siku wawe wame kuwa reduced by half.Katika hali hii, kweli nia yetu ya kuondoa umaskini itafikiwa?

  Katika shamba hili kumekuwa na awamu mbalimbali za uongozi kama nikivyo kwisha kusema,na hakuna hata moja iliyo jaribu kwa dhati kabisa ku address matatizo ya wakulima wadogo wadogo.Nimesema hapo awali kwamba uongozi wa Wilaya umekuwa sehemu ya matatizo ya shamba hili,kwa vile badala ya kukemea utendaji mbaya wa uongozi wa shamba,uongozi wa Wilaya umenyamaza kimya huku ukionekana kuwa sambamba na uongozi wa shamba,jambo ambalo linaleta hisia za rushwa kwa wanachi walio wengi.

  Kama kweli nia yetu nikuondoa umaskini kwa wanachi wetu,ni vema wakapewa kipaumbele na kuwezeshwa,vinginevyo wimbo wa kuondoa umaskini ambao umezoeleka sasa bila kupiga hatua yeyote,utaendelea kuimbwa, huku wananchi wetu wakizidi kuwa maskini.Ikumbukwe kwamba shamba hili ni la umwagiliaji,kwa hiyo kama serikali italisimamia vizuri kinyume na ilivyo sasa, wakulima wadogo wadogo wanaolima katika shamba hili wataondokana na umaskini kabisa.
   
  Last edited by a moderator: Feb 20, 2009
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hii ikae ktk Siasa!

  Dakawa tena?

  Sasa rushwa..kila mahali?
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtoa mada kuwa muwazi na mkweli. Kiongozi gani kapendelewa? Kivipi?
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Majina tunayahifadhi!lLakini swala lako linaelekea na wewe una asili ya ka ufisadi ndani.Soma nyakati.

   
 5. S

  Sumaku Member

  #5
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamii Forums ni Home of Great Thinkers!
  Companero ameuliza,nami namuunga mkono,uwe muwazi,nani aliyependelewa?
  Bwana Mkubwa mmoja alipata kusema:Mtu mwenye akili zake akikuambia mambo ya kipuuzi,huku akijua kuwa wewe una akili,nawe ukamsadiki,ATAKUDHARAU!
  Tupe maelezo ya ziada,usihifadhi majina,kipi kinakuzuia kuhifadhi majina hayo na facts nyingine?
   
Loading...