Uonevu dhidi ya Waislam UDOM: Msikiti wavunjwa, wafanyakazi wanataaluma 11 wahamishwa

Waislamu wakipata kazi mahali wakionekanaonekana japo ni wengi wengi kidogo hata kama Over all majority bado sisi Wakiristo ni wengi zaidi kuna Wakiristo wenzetu huanza kuona nongwa, hii sijui kwa nini!. Maneno ya humu JF kuwa eti waislamu walijazana mahali fulani ni ushahidi wa hili ninalolisema!

Hivi leo hii hizi teuzi zinazofanyika nchini ambapo Majority ni Wakiristo wanateliuwa kila teuzi laiti ingekuwa reversed na waislamu wakawa ndio wenye kuteuliwa kwa wingi zaidi humu JF zingejaa mada za kulia udini udini

Mimi huwa siwaelewi kabisa Wakiristo wenzangu kwa kuleta madai ya udini pindi waislamu wakiwa angalau wengiwengi katika taasisi fulani

Yesu Kristo wa Nazareti hakutufundisha hivi, alitufundisha mpende Jirani yako!
Pia mpende adui yako

Kwahiyo la uadui halipingiki ila tuwapende
 
Ningependekeza uzi huu sasa ufike mwisho kwa faida ya maelewano ya wananchi wa Tanzania ambao tumekuwa nayo kwa miaka mingi. Hiz dini zilikuja na meli zisitufikishe sehemu ambayo tutakuja kujuta huko mbele. Tuagalie maslahi mapana ya vizazi vijavyo.
Huu ndo unafiki wetu watanzania. Tukishafika mahala jambo nyeti na muhimu la dini watu wansema ya moyoni basi tunajifanya eti tuacheni kuongelea mambo ya dini.
Dini ni mwenendo wa maisha hasa kwa sisi waislamu. Huwezi tenganisha dini yetu na maisha ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ndo unafiki wetu watanzania. Tukishafika mahala jambo nyeti na muhimu la dini watu wansema ya moyoni basi tunajifanya eti tuacheni kuongelea mambo ya dini.
Dini ni mwenendo wa maisha hasa kwa sisi waislamu. Huwezi tenganisha dini yetu na maisha ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila usisahau, kwenye hayo maisha ya kawaida ambayo waislamu hawawezi kuyatenganisha na dini,
1. Kuna wasio waislamu humo humo
2. Kuna aina nyingine ya maisha ambayo wasio waislamu wanaishi
3. Kuna maeneo kuna mchanganyiko wa waislamu na wasio waislamu
 
Hoja sasa ni kuvunjwa kwa jengo au kuhamishwa kwa watumishi wa umma ?
Hilo jengo lilikuwa linajengwa na nani mpaka livunje?
Mvunjaji kwa nini ameamua kulivunja ?
Je jengo linakibali chochote cha ujenzi ?
 
Mkristo au mwislamu wa kweli hawezi kubeza dini au imani ya mtu mwingine!!

Kubeza imani ya mtu ni dhambi ya kimaadili na nikukosa ustaarabu!!

Hii dunia ni ya kwetu wote na wote tunayo haki ya kuishi na kuamini tupendavyo na vilevile kuheshimu maamuzi ya imani ya wenzetu!!

We have to coexist!!

Sio lazima uipende imani yangu, kabila langu, nchi yangu, wazazi wangu n.k. Wala mimi silazimiki kufanya hivyo kwako!

La msingi ni kuheshimiana na kuvumiliana ili tuishi kwa amani na mtangamano!!

Mfano walioonyesha viongozi wa Umoja wa Falame za Kiarabu kule Abudhabi na Baba Mtakatifu Francisco ni mfano bora wa kihistoria!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huu ni wakati wenu wa kuisoma number m*wa nyie. Kipindi cha kikwete waislam walikuwa wanafanya vikao college ya education (ng'ong'ona) wanaalika wenzao wenye itikadi Kali na kuapiana ni lazima wasaidiane.

Masoud (muislam mwenzenu) pale informatics (akiwa examination officer) alikuwa anawapa paper waislam wanasolve msikitini Kesho yake wakiingia kwenye mtihani wanafaulu vizuri,(mbona hukuja kulalamika hapa kuwa waislam wanaonewa).

Bibie pambana na Hali yako(yenu). Hii mliianzisha wenyewe,sasa unalialia nn

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora amesepa yule jamaa(Dr. Masoud), kwanza alkuwa na dharau na majigambo kibao
 
Hii Ndio Option nzuri sana, Kama sikosei Dini zingine, wanachofanya ni Kutumia Hall zilizopo kufanya Ibada, Labda changamoto ya wenzetu waislamu Namna yao ya Ibada pengine inalazimisha Jengoo maalum la Kiibada? Kama Hivyo basi Busara inahitajika kuona namna ya kuhakikisha mambo yako sawa.
Mimi nawajua Vijana wa Chuo, utazuka Mtafaruku Mkubwa sana hapo, kama Busara zisipotumika
Wazushe wapigwe
 
Tatizo lenu hua mnaleta ubaguzi wa hovyo sana, kujitenga na kutengeneza ka_ uadui ka kijinga. Mimi naunga mkono kubomoa na ningekua karibu hapo ningeshiriki zoezi kikamilifu kabisa. Mkitaka kuswali nendeni sijui mnapaita Makulu au mjini. Shenzy kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena wanaubaguzi wa hali ya juu utakuta wanakusanyana wanaenda jifungia msikitini wanafanya discussion huko kama sio ubaguzi ni nn? Mbona vyuoni hukohatuoni makanisa yakajengwa? Kama umevunjwa well done

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninakaa Dodoma na Udom kila mara nipo kule kwa kiasi tunajua kitu gani kilikuwa kiktendeka wakati wa prof Kikula na prof Mlacha hakuna asiyejua hata Mkuu mwenyewe anajua kwamba kulikuwa na Udini ulio vuka mipaka.

Kama Waislamu wakitaka kujenga msikiti chuoni tena chuo cha Umma na Dini singine zikidai kujenga makanisa na mahekalu kuktakuwa kuna kusoma au kutangaza dini na madua.

Mbona chuo Kikuu cha st john hakuna msikiti na waislamu wamepewa sehemu nzuri tu ya kufanyia dua.

Mbona CBE hakuna msikiti wala makanisa na kila kitu kinakwenda vizuri bila shida.

Vyuo vyote dodoma havina misikiti wala makanisa isipokuwa chuo kikuu cha st johns na wao hilo kanisa lilikuwepo toka enzi za mkoloni kwa maana chuo hiko ilikuwa shule ya kanisa la Anglikani miaka za 1940 na baadaye kutaifishwa na kuwa shule ya sekondari mazengo na baadaye tena kurudishwa kanisa la Anglikani kwa St John university.

Haya yanayotokea UDOM ni dhambi ya prof Kikula na Prof Mlacha kuendeleza Uislamu katika Chuo hicho kikubwa Afrika mashariki na kati.

Narudia kusema Wailamu wengi walioajiriwa Udom waliajiliwa kimkakati wa kuwainua na kuwaendeleza Waislamu.

Sina uhakika lakini yalisemwa hapo Udom kwamba kuna fist lady mmoja naye anahusika sana na kupandikiza kwa makusudi/kimkakati Uislamu hapo Udom.

Ombi kwa serikali ni kuchuja na kufuatilia kikamilifu mienendo ya chuo kikuu cha Dodoma wakati wa prof kikula na Prof Mlacha (walikuwa ni zaidi ya Miungu watu Hapo chuoni kwa maana prof Mlacha alikuwa Mkuu wa Administration na Fedha na Kikula alikuwa ni Mkuu msaidizi wa chuo juu yake akiwepo Mh Mkapa).

Prof Mlacha ni Mpare. Wapare ni kabila dogo hapa nchini lipo kwenye wilaya moja tu. Lakini chunguza waajiriwa wapare hapo UDOM ndio utashangaa.

Sina chuki na mtu Ila ninachukia sana Ukabila na Udini unawafanya makabila na dini zingine kuwa wanyonge sana katika nchi yao.
Uko sahihi kabisa kwa waliosoma UDOM watakubaliana na ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyinyi au wewe unazungumza kitu usichoelewa, unasema waislamu wapewe Room ili wawe wakiswalia, tayari ukishakuwa na Room kwa ajili ya kuswalia huo ni Msikiti kwa istilahi ya dini ya kiislamu, kulingana na ukubwa wa UDOM, tujiulize ni Room ya ukubwa upi itakayoweza kuchukua hao Waumini wote kwa wakati mmoja mfano katika sikuu za Ijumaa??, na ikumbukwe waislamu wanatakiwa kuswali swala za lazima mara 5 kwa siku.

Kwa mazingira hayo, waislamu wanayo haki ya msingi ya kuabudu, hivyo kama waliomba eneo la kujenga msikiti, je wengine nao waliomba kujenga nyumba zao za Ibada wakanyimwa??!!,ni hapo sasa ndipo Udini unapokuja na sio kwa kujenga msikiti ndiyo udini.

Hao hao viongozi wa serikali utawasikia wakipaza sauti wakiwaomba Viongozi wa dini wawaase waumini wao ili wawe raia wema na wenye maadili, halafu hapohapo hawataki nyumba ya Mungu ijengwe na mbaya zaidi INABOMOLEWA bila khofu!!!, je mkishikwa na laana mtasema Waislamu wamewaroga?!!?.
Kwani Dodoma haina misikiti? Christian wanaabudu wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
63 Reactions
Reply
Back
Top Bottom